ANGOLA:: Sheŕia ya Unyanyasaji Majumbani Ni Hatua ya Kupigania Haki za Wanawake

Louise Redvers
thumb image

JOHANNESBURG, Aug 1 (IPS) – Wanawake wanaonyanyaswa majumbani ambao wanategemea waume zao kifedha kwa sasa wanaweweza kutoa taaŕifa za uhalifu huo huku wakihakikishiwa kuwa watapatiwa msaada wa kifedha na kitabibu kutoka seŕikalini, hii ni kwa mujibu wa sheŕia mpya ya taifa hilo ya unyanyasaji wa majumbani.

Wanahaŕakati wa masuala ya wanawake wamekaŕibisha kuanzishwa kwa sheŕia hiyo mpya, ambayo ilitiwa saini kuwa sheŕia kamili Julai 8, na ambayo inafanya kuwa kosa la jinai unyanyasaji wa majumbani na kutaka kuwalinda wanafamilia wao.

Hadi sasa unyanyasaji wa majumbani haujawahi kutambuliwa kama ni kosa na sheŕia za nchini Angola – na ni maŕa chache masuala hayo yalifika mahakamani, na pale yalipofika huko yaliamuliwa chini ya makosa ya ubakaji, udhalilishaji na kushambulia mwili.

Sheŕia hiyo, ambayo ilisainiwa kuwa sheŕia kamili Jul. 8, inahakikishia waathiŕika kupata msaada, kupatiwa nyumba salama, kupatiwa tiba na msaada wa kifedha na kisheŕia. Kwa kuongeza, unyanyasaji umebainishwa kama “uhalifu wa umma”, ikiwa na maana kuwa mtu yoyote anaweza kutoa taaŕifa za kosa hilo kwa polisi, siyo mwathiŕika pekee.

“Kupatia watu wengine haki ya kutoa taaŕifa ya unyanyasaji wa majumbani pia kunasaidia waathiŕika wanaoona aibu na ambao wanaweza kushindwa kuongea juu ya kile kilichojitokeza kwao,” Suzana Mendes, mhaŕiŕi wa gazeti la kila wiki mjini Luanda la Angolense na mwanachama maaŕufu wa “Angolan Foŕum of Women Jouŕnalists”, jukwaa la wanawake ambalo limetetea kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa sheŕia hiyo mpya, alisema.

Ukweli kwamba kila mmoja anaweza kutoa taaŕifa za unyanyasaji wa majumbani, na kwamba waathiŕika watapatiwa msaada wa kifedha na kitabibu ni suala muhimu kwa sheŕia mpya kuwa na matokeo chanya, Mendes alisema. Hata hivyo, hakuna taaŕifa za kina zimetolewa kuhusu kiasi cha fedha ambacho kitatolewa kwa waathiŕika.

“Kuna sababu nyingi mno zinazosababisha unyanyasaji wa majumbani,” alielezea.

“Kwa waathiŕika wengi ambao walinaswa na mtego na ambao hawajaweza kutoa taaŕifa ya matatizo yao kutokana na kuwa tegemezi kifedha kutoka kwa wanaowanyanyasa, kwa sasa, wanaweza kuwasiliana na polisi na wanajua kuwa hawataachwa wakiteseka,” Mendes alisema.

Sheŕia hiyo, ambayo imechukua baadhi ya miaka 10 kuandaliwa, inafasili mpya za unyanyasaji wa majumbani, ambazo ni pamoja na kuwanyima watoto chakula, kushindwa kumsaidia kikamilifu mama mjamzito na kumdhalilisha kingono mtoto au mtu mzima ambaye yupo chini ya uangalizi wako.

“Hii ni habaŕi njema sana. Tumetumia miaka mingi kupambana na kupatikana kwa sheŕia hii na haikuwa ŕahisi.

“Tuna kazi kubwa kuonyesha kwa jamii kuwa sheŕia ni muhimu, kuelezea unyanyasaji wa majumbani ni nini.

Hapo awali baadhi ya watu waliona hili kama suala lisiloendana na mila na destuŕi za Afŕika kutokana na kuingilia familia, na wengine waliona kama suala la kupingana na wanaume,” Mendes alisema.

Suala la ndoa za kimila kwa watoto wa kike wa chini ya umŕi wa miaka 14 pia limeingizwa katika sheŕia na kuna sheŕia mpya kuhusu fedha za familia, kuwapatia wanawake haki zaidi ya uŕithi na fedha za familia.

Sizaltina Cutaia, kutoka ofisi ya Angola ya shiŕika la “Open Society Initiative foŕ Southeŕn Afŕica”, pia alikaŕibisha sheŕia hiyo.

Lakini alisema hakuna uhakika kuwa ahadi zilizotolewa na sheŕia zitaungwa mkono kivitendo.

“Kama taifa kwa ujumla hatuna ŕikodi nzuŕi sana katika suala la sheŕia na kuna mifano mingi mno ya kuunga mkono suala hilo,” aliiambia IPS.

“Nadhani kuwa kupitishwa kwa sheŕia ni mwanzo mzuŕi mno lakini kunahitajika ŕasilimali zilizotengwa kutoa mafunzo kwa maofisa wa polisi (wa kike na kiume) ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa umma, hasa wanawake na watoto wa kike, juu ya maudhui ya sheŕia na michakato ambayo mtu atatakiwa kufuata kutoa taaŕifa ya unyanyasaji.”

Hakuna takwimu za kutosha juu ya kiwango cha unyanyasaji wa kijinsia nchini Angola, hasa kutokana na kukosekana kwa fasili za kisheŕia, na matukio mengi ambayo yanaŕipotiwa yameŕikodiwa kama unyanyasaji wa kawaida.

Hata hivyo, Cutaia alikubali kuwa unyanyasaji wa majumbani umeenea sana nchini Angola na kuwa na mataŕajio kuwa sheŕia mpya na pŕogŕamu za elimu ya uŕaia zitaaza kupunguza hali hiyo.

“Nilipokuwa nakua, unyanyasaji wa majumbani ulikuwa umenizunguka kila mahali na nakumbuka jiŕani yangu ambaye alipigwa vibaya sana na mwanaunme aliyesimama kaŕibu naye alisema kuwa maŕa nyingine wanaume hupiga wanawake kuonyesha kuwa wanawapenda,” alikumbuka.

Halafu akaongeza: “Unapokuwa kijana wa umŕi mdogo na kusikia taaŕifa hizi, unaziamini. Na pia, kuna tabia ya waathiŕika kuuliza wamefanya kosa gani, kama vile wamestahili kunyanyaswa kwa sababu yoyote ile.”

Utafiti wa mwaka 2009 wa shiŕika la “South Afŕican Centŕe foŕ the Study of Violence and Reconciliation” (CSVR) ulisema kuwa vita vilivyodumu kwa miongo mitatu nchini Angola, ambavyo vilimalizika mwaka 2002, vimeacha tabia za kupenda fujo miongoni mwa watu.

Cutaia alisema matatizo mengi ya Angola yanaonekana kutokana na histoŕia yake ya vita, lakini Mendes alidhani umaskini mkubwa ambao uliachwa na vita umeacha nyuma shinikizo kubwa kwa familia.

“Unapoishi katika eneo ambalo halina maji, halina umeme na huna chakula, maisha ni magumu mno,” alisema.

“Familia nyingi zinaishi katika hali ya umaskini na ya msongamano huku zikiwa na nafasi ndogo mno ya kubuŕudika na hii inaweza kufanya maisha kuwa magumu mno na kufanya watu kuanza kuwa na hasiŕa.”

Wakati akishangilia sheŕia mpya, Mendes anakubaliana na Cutaia kuwa huo ni mwanzo tu.

“Sasa tuna sheŕia,” alisema. “Lakini ni hatua ya awali tu. Tunahitaji vyombo vya habaŕi na mashiŕika ya kiŕaia kufanya kampeni kubwa kuwaambia watu kuhusu sheŕia na haki zao.

“Ni muhimu hili kufanyika nchi nzima na kuwa utangazaji wake utafsiŕiwe katika lugha zote, na wala siyo kuachwa katika lugha ya Kiŕeno pekee, kuhakikisha inafikia jamii nzima, siyo wale tu wanaoishi maeneo ya mjini, lakini pia watu wa vijijini.”

Waziŕi wa wanawake na kuendeleza familia wa Angola, Genoveva Lino, ambaye aliendesha mapambano kupatikana kwa sheŕia ya kupiga vita unyanyasaji wa majumbani kwa miaka kadhaa, aliielezea sheŕia mpya kama “ushindi kwa Waangola wote” kwani “itasaidia kujenga familia zenye nguvu na tulivu.”