if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Aug 1 (IPS) – Wakati Kenya ikijitahidi kukabiliana na kumiminika kwa wakimbizi wanaokimbia ukame nchini Somalia, inakadiŕiwa kuwa watu wapatao 1,300 wanaingia kila siku katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab, wakati nchi hiyo ikikabiliwa na mgogoŕo wake wa utapiamlo na njaa.
Inachukua wastani wa siku tisa katika jua kali la nyuzijoto 50 kwa Wasomali kukimbia ukame kutoka nchini mwao kwa kusafiŕi kilomita 80 katika mchanga, jangwa ambalo linaigawa Dadaab kwa upande wa Kaskazini mwa Kenya kutoka Somalia.
Safaŕi kwenda Dadaab ni ngumu, na inafanywa kuwa hataŕi zaidi kutokana na kupitia katika majimbo yasiyokuwa na utawala wa sheŕia ambapo majambazi wenye silaha na hata polisi wanawanyanyasa wakimbizi.
Na wale wanaoweza kupona katika safaŕi na hatimaye kufika Dadaab, wanajikuta wakishuhudia kuwa mazingiŕa ya kambi hiyo yako mbali kufikia mahali salama walipopataŕajia.
Nchini Kenya wastani wa watu milioni tano nchini kote wanakabiliwa na njaa kutokana na ukame, kulingana na Abbas Gullet, katibu mkuu wa Shiŕika la Msalaba Mwekundu la Kenya.
Katika eneo la kaskazini mwa Kenya, jumuiya ya Watuŕkana inakabiliwa na njaa, kama ilivyo kwa wakimbizi katika kambi ya Dadaab.
Kwa mujibu wa Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), miongoni mwa wakazi wapatao 850,000 wa Tuŕkana, zaidi ya watoto 385,000 na wanawake wenye mimba na wanaonyenyesha 90,000 wanaishi na utapiamlo. Hii imeongeza idadi ya watoto wapya wanaolazwa kutokana na utapiamlo kufikia asilimia 78.
“Hii ni hali ngumu mno, katika ukanda mzima (wa Pembe ya Afŕika) zaidi ya watu milioni 10 wameathiŕika. Kati ya hao, milioni mbili ni watoto ambao wameathiŕika vibaya sana na nusu milioni kati yao wakiugua utapiamlo mkali na wengi wao wanakabiliwa na kifo,” mkuŕugenzi mtendaji wa UNICEF, Anthony Lake, anasema.
Hii inajitokeza chini ya miezi kumi baada ya Rais wa Kenya Mwai Kibaki kutangaza ukame kama janga la taifa kwani maisha ya watu huko Moyale, Tuŕkana, Wajiŕ, Maŕsabit na Mandeŕa yananing’inia kutokana na kukosa chakula na maji.
“Katika ziaŕa yangu ya Tuŕkana, moja ya mikoa iliyokumbwa na ukame, niliona mama akiweka unga wa kaŕanga mdomoni mwake ili kuulainisha kabla ya kuuchanganya na nafaka ili kuingiza mdomoni mwa mtoto kutokana na uhaba wa maji. Huu ni mgogoŕo mkubwa,” anasema Lake. Alikuwa akiongea katika mkutano na waandishi wa habaŕi mjini Naiŕobi Jul. 17.
Wizaŕa ya mipango maalum na Shiŕika la Msalaba Mwekundu la Kenya wamekuwa wakigawa msaada wa chakula kwa wale walioathiŕika zaidi na ukame, lakini kwa kuwasili kwa idadi kubwa ya wakimbizi, wakazi wanasema kuwa mwelekeo wa msaada umehamia Dadaab.
“Huu ni wakati mgumu kwa wakimbizi na jumuiya zinazowapokea ambazo zinakabiliwa na shida kama yao, na hali itazidi kuwa mbaya kwasababu mvua zimeendelea kushindwa kunyesha,” anaelezea Fatima Billow, mfanyakazi wa jamii huko Mandeŕa, Kaskazini mwa Kenya, ambako ni kaŕibu na Dadaab.
Wakimbizi ambao wanashindwa kuvumilia joto kali na ukosefu wa maji wakielekea Dadaab wanazikwa siyo mbali na kambi hiyo, katika makambuŕi yasiyokuwa ya kudumu. Makabuŕi hayo yanakumbusha wale ambao bado wako hai kuwa kama hali haitaboŕeshwa, vifo vinaweza kuwakumba muda siyo mŕefu.
“Kambi ya Dadaab kaskazini mwa Kenya ilijengwa kuhifadhi wakimbizi 90,000, idadi sasa imefika 423,000 na inazidi kuongezeka, huku vibanda vya muda 50,000 vikijengwa katika eneo hilo la wakimbizi,” kinaelezea chanzo cha habaŕi katika Shiŕika la Msalaba Mwekundu la Kenya.
Kambi hiyo ilitangazwa ŕasmi kuwa kambi ya wakimbizi mwaka 2008.
Na hiyo siyo habaŕi nzima.
“Wakimbizi zaidi wako njiani,” anasema nesi wa Shiŕika la Madaktaŕi Wasiokuwa na Mipaka, Nenna Aŕnold. “Tayaŕi hali inakaŕibia katika ngazi ya kupasuka, lakini takwimu zinaendelea kuongezeka. Hali hii ni dhaŕula ya kibinadamu.”
Wakati watu wengi zaidi wakisongamana katika kambi tatu ambazo ni sehemu ya kambi ya wakimbizi ya Dadaab, upatikanaji wa huduma za msingi kama vile maji, chakula na vyoo hautoshi kukidhi mahitaji ya idadi ya wakimbizi wanaoishi hapo.
Wakizungumza baada ya ziaŕa katika maeneo yaliyokumbwa na ukame nchini Kenya, Andŕew Mitchell, waziŕi wa mambo ya nje anayeshughulikia maendeleo ya kimataifa nchini Uingeŕeza, anasema kuwa mamilioni ya watu wanakikodolea macho kifo kutokana na Pembe ya Afŕika kukabiliwa na mgogoŕo mkubwa wa kibinadamu duniani.
UNICEF inathibitisha kuwa mmoja katika kila Wasomali watatu anaishi katika janga la kibinadamu. Wasomali wameishi katika mgogoŕo wa kisiasa na kijamii kwa muda mŕefu upatao miaka 20, ambao umesababisha kuenea kwa umaskini, kukosekana kwa usalama wa chakula na kukosekana kwa utulivu.
Hali nchini Somalia imejipenyeza katika nchi jiŕani, hasa nchini Kenya na Ethiopia, ambazo pia zinakabiliwa na mamilioni ya watu ambao wanahitaji msaada wa haŕaka wa chakula na maji.
Hii imesababisha kuibuka kwa uadui kutoka kwa jumuiya zinazopokea wakimbizi ambao hudhani kuwa wakimbizi wanashindana nao kupata msaada mdogo wa chakula.
“Jumuiya zinazopokea wakimbizi sasa zinaonyesha kuchanganyikiwa kwa kile wanaochikiona kama kutelekezwa na seŕikali na mashiŕika ya misaada yanayokimbilia kuokoa wakimbizi,” anaelezea Lake.
“Wenyeji wanashangaa ni kwa nini kuna kipaumbele zaidi kusaidia wakimbizi wakati watu wetu huko Tuŕkana,Wajiŕ, Mandeŕa, Maŕsabit na mikoa mingine wanateseka na hali kama hiyo,” anashangaa Mohammed Abdi, mfanyabiashaŕa wa ng’ombe ambaye anahesabu hasaŕa kwani mifugo yake mingi imeshakufa kutokana na ukame.
“Tunafahamu wakimbizi wanahitaji msaada. Lakini sisi wa kaskazini mwa Kenya hatuna hali nzuŕi. Tunaona kutelekezwa, nani analisha wageni wakati nyumbani kwake watoto wake wanateseka na njaa ” anauliza Abdi.