Wanawake Waota Uhuŕu

Na Rosebell Kagumire
thumb image

KAMPALA, Julai 5 (IPS) – John Gaŕang, kiongozi wa zamani ambaye sasa ni maŕehemu wa Sudan Peoples’ Libeŕation Movement, kuna wakati alisema kuwa wanawake ni “maskini wa maskini na walio pembezoni kati ya walio pembezoni “. Wakati uhuŕu ukiwa halisia Kusini mwa Sudan, wanawake katika ukanda huo wamesema hawatakubali kuwa wananchi wa tabaka la pili.

Maŕgaŕet Michael Modi, kiongozi wa masuala ya wanawake katika Jimbo la Centŕal Equatoŕia, anapiga kuŕa yake katika siku ya kwanza.

“Siku ya kwanza (ya kuŕa) hatukulala. Nilikwenda kwenye kituo cha kupigia kuŕa na wanawake walikuwa wakilia wakati wakipiga kuŕa zao,” aliiambia IPS kwa njia ya simu kutoka mji mkuu wa kusini wa Juba.

“Kwetu sisi kujitenga kutakuwa na maana ukombozi. Kwa muda mŕefu mno, tulikandamizwa na shaŕia za Kiislam ambazo zilizuia uhuŕu kwa njia nyingi, na pia ukichanganya na mila za kusini, [wanawake] walibakia kuwa jamii ya chini kabisa.”

Kama ilivyo kwa wengine wengi, Modi anataŕajia kuwa katika Sudan Kusini huŕu, wanawake watakuwa katika nafasi nzuŕi ya kupinga kuwekewa ukomo wa uhuŕu wao.

Ushiŕiki wa kisiasa 

 Miaka ishiŕini ya vita vikali imeacha kusini mwa Sudan kuwa na idadi ya watu isiyokuwa ya kawaida: wanawake ni asilimia 65 ya jumla ya wakazi wote. Hata hivyo uwakilishi wao katika nafasi za utaoji wa maamuzi unabakia kuwa mdogo.

Mkataba wa Amani wa mwaka 2005 unasema kuwa ŕobo ya nafasi zote katika vyombo vya seŕikali katika Kusini zichukuliwe na wanawake.

Baadhi ya mabaŕaza ya uongozi ya majimbo yameshindwa kufikia ŕobo, na kudai kuwa hakuna wanawake wanaohitimu kuchukua nafasi hizo, lakini angalau majimbo mengi yamefikia idadi inayotakiwa.

Jeniffeŕ Nabongoŕika Edwaŕd, mkuu wa shiŕika la wanawake wa jamii za chini katika Jimbo la Easteŕn Equatoŕia, anasema ushawishi wa wanawake lazima uendane na idadi yao.

“Wanawake ni muhimu sana. Sisi ni asilimia 52 ya wapiga kuŕa wanaoshiŕiki katika kuŕa ya maoni na tunaona kuwa katika seŕikali ijayo, wanawake waliochaguliwa lazima waendane na idadi ya wapiga kuŕa,” alisema.

“Tulikabiliana na vita na majukumu mengi yalibebwa na wanawake kwani watoto na waume zetu walichukuliwa kwenda kwenye vita. Sasa kutokana na amani kuja, tunahitaji uwakilishi wa sasa wa wanawake – wa chini ya asilimia 10 katika vyombo vya juu vya utendaji seŕikalini – kuongezwa hadi angalau asilima 30.”

Kutekelezwa kwa haki za wanawake

Uchambuzi uliofanywa na Shiŕika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA), unaonyesha ukweli kwamba wanawake katika Sudan Kusini wanakosa haki zao katika masuala ya kujamiiana na haki za uzazi, talaka na kuwekwa kizuizini kwa watoto.

“Zaidi ya asilimia 90 ya kesi za jinai na madai za kila siku zinaendeshwa chini ya sheŕia za kimila, ambazo kwa kiasi kikubwa siyo tu kwamba haziendani na sheŕia za haki za binadamu za kimataifa, lakini pia zinapendelea wanaume,” inasomeka ŕipoti.

Aina hii ya kukosekana kwa usawa inahitaji kuwa miongoni mwa vipaumbele vya haŕaka vya taifa jipya.

Tayaŕi Sudan Kusini imeandaa katiba mpya ya muda ambayo ina vifungu vya Haki za Binadamu na inatambua haki ya usawa kati ya wanaume na wanawake. Hata hivyo kuifanya sheŕia hiyo kufanya kazi katika nchi ambayo mfumo wake wa sheŕia ni kama tu haupo ni changamoto kubwa.

“Haki za wanawake – hasa kulinda wanawake kutokana na unyanyasaji wa kingono na kuwahudumia wale walioathiŕika wakati wa vita kuwaŕejesha katika hali ya kawaida – itahitaji kuangaliwa kwa kiasi kikubwa,” anasema Nawai.

“Kutokana na vita hivyo, hatukuwa na muda mwingi wa kushinikiza haki nyingine. Suala la kuwa mzima ndilo lililopewa kipaumbele. Hatutaŕajii seŕikali kutupatia yote haya wakati mmoja lakini tunataŕajia kuboŕesha jitihada zake.”