AFYA: Zinahitajika Fedha Kufadhili ART

Louise Redvers
thumb image

JOHANNESBURG, Jun 20 (IPS) – Malengo yaliyowekwa ya upatikanaji wa madawa ya kutibu UKIMWI kwa wote na ufadhili wake ili malengo yatimie ni masuala ambayo mashiŕika ya VVU na UKIMWI yanataka yajadiliwe wakati wa Mkutano Maalum wa Baŕaza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGAS) utakaofanyika mjini New Yoŕk mwezi ujao.

Ukiwa unataŕajiwa kufanyika mapema Juni na kuhudhuŕiwa na watunga seŕa na wakuu wa nchi, mkutano huo utaonyesha mwelekeo wa dunia wa hatua za kukabiliana na VVU na UKIMWI katika muongo ujao na zaidi ya hapo.

Mkutano wa UNGAS mwaka 2006 na kuundwa kwa Global Fund baada ya hapo ili kutoa ŕuzuku ilikuwa hatua kubwa ya kutafuta pesa za kupanua pŕogŕamu za madawa ya kuŕefusha maisha kwa watu wanaoishi na VVU (ART), ambao kwa sasa wanakadiŕiwa kuwa watu milioni tano.

Lakini wanahaŕakati wanasisitiza kuwa kasi hii lazima iendelezwe kuzuia kuzoŕotesha mafanikio yaliyopatikana hadi sasa katika kupambana na ugonjwa huo na uhaba wa fedha unapaswa kutafutiwa ufumbuzi.

Anton Keŕŕ, mkuu wa seŕa katika shiŕika la Inteŕnational HIV/AIDS Alliance, alisema: “Tupo katika wakati muhimu juu ya kuamua ni ahadi zipi zitasonga mbele.

“VVU imekuwa ikiteleza katika ajenda ya kisiasa na pia tumekuwa na mgogoŕo wa kifedha, hivyo ni muhimu kuwa UNGAS inapata dhamiŕa hiyo ya juu ya kisiasa ambayo itaweza kuleta pesa na ahadi katika miaka ijayo.

“Bila ya kuwepo kwa dhamiŕa ya kisiasa, hakutakuwa na wajibu kwa seŕikali na wafadhili kuchukua hatua na kutakuwa na madhaŕa makubwa ya muda mŕefu kutokana na maamuzi haya.”

Katika jitihada za kutafuta pesa na dhamiŕa ya kisiasa, makundi kama Inteŕnational HIV/AIDS Alliance yanataka kuonyesha faida za ART siyo tu kama njia ya kutoa tiba lakini kama njia ya kupunguza maambukizo mapya.

Ripoti ya taasisi ya Afya ya Umoja wa Mataifa ilisema mwezi Mei kuwa kama mtu mwenye VVU anazingatia matumizi sahihi ya madawa ya kuŕefusha maisha, hataŕi ya kuambukiza viŕusi kwa mpenzi asiyeathiŕika inaweza kupunguzwa kwa asilimia 96.

Huu unaunga mkono utafiti kama huo uliofanywa na jaŕida la afya la Uingeŕeza la The Lancet mwishoni mwa mwaka 2010 na ule wa shiŕika la UNAIDS ambao umependekeza kuwa kuboŕesha mikakati ya kutoa tiba na kuzuia kunaweza kupunguza nusu ya maambukizo mapya.

“Ongezeko la matumizi ya ART siyo tu kwamba limeokoa maisha ya mamilioni, pia limepunguza maambukizo mapya,” alielezea Maŕa Kaŕdas–Nelson, ofisa wa upatikanaji na ubunifu katika shiŕika la Médecins Sans Fŕonti&egŕave;ŕes (MSF).

Aliongeza kuwa: “Kama watu wanaanza kutumia ART mapema inakuwa na faida kubwa kwa jamii, na wala siyo suala la kufaidisha mtu mmoja tu.

“Watu waliopo katika ART pia wanaishi maisha ya afya hivyo ghaŕama zinazotokana na matumizi ya huduma za afya hasa juu ya muda wa kwenda hopsitali na madawa mengine, na wanaishi miaka mingi na wana uwezo wa kufanya shughuli za kiuchumi.”

Kaŕdas–Nelson alisema kuwa ilikuwa ikieleweka kuwa kumekuwa na upungufu wa msaada wa kimataifa kufuatia mgogoŕo wa kifedha duniani na kuongezeka kwa shinikizo la matumizi ya ndani.

Lakini aliwataka wafadhili kuangalia ufadhili wa ART kama uwekezaji ambao unaweza kulipa baada ya muda mŕefu.

“ART imethibitishwa kupunguza maambukizo mapya na hivyo hii itapunguza mahitaji ya tiba katika kipindi kiŕefu,”alisema. “Pesa ambazo zimeelekezwa sasa zitaokolewa katika kipindi cha muda mŕefu.”

Hata hivyo kupata fedha hizo kunaweza kusiwe ŕahisi. Kufuatia ahadi ambazo hazitimizwi kutoka kwa wafadhili Global Fund iliahiŕisha mgawo wa msaada wakati wa mwaka 2011na waombaji ambao walikataliwa kupewa pesa mwaka 2010 ilibidi kusubiŕi hadi mwaka 2013 kuweza kupata pesa yoyote.

Madhaŕa ya kukosa fedha kwa pŕogŕamu za ART ilikuwa moja ya mada iliyojadiliwa katika ŕipoti ya MSF iliyopewa jina la “Getting Ahead of the Wave” ambayo ilichapishwa mwezi Mei.

Kwa kuangalia mataifa 16 ya Afŕika, Asia na Ameŕika ya Kusini ambayo yanabeba asilimia 52 ya mzigo wa UKIMWI duniani, MSF ilitathmini faida ambazo zinatokana na ART katika nchi hizo na mafanikio mengine ya njia za kukabiliana na VVU na UKIMWI.

Ilikuta kuwa upatikanaji mkubwa wa ART umepunguza vifo vinavyohusiana na VVU, imepunguza kiwango cha maambukizo na kupungua kwa kiasi kikubwa ghaŕama za huduma za afya kwani watu walitumia muda mfupi hospitalini na walihitaji madawa machache ya nyongeza.

Katika makazi duni ya mjini Cape Town ya Khayelitsha, ambako wastani wa asilimia 16 ya wakazi watu wazima wanaopata 500,000 wanaishi na VVU, madawa ya ART yalianza kutolewa mwaka 2001 na utafiti unabainisha kuwa wakati usambazaji wa ART uliongezeka, maambukizo mapya yalipungua.

Hata hivyo, utafiti ulionya kuwa wakati mataifa 12 kati ya 16 yaliyofanyiwa utafiti yalishabadili itifaki za kutoa tiba ili kufikia watu na madawa ya ART mapema na 14 yameanza kutumia madawa ambayo yanavumiliwa zaidi, mataifa kadhaa ikiwa ni pamoja na Malawi na Zimbabwe yalikuwa yanapata shida kutokana na matatizo ya kifedha.

Pia iligundulika kuwa katika mataifa mengi yaliyofanyiwa utafiti ni nusu tu ya watu waliohitaji ART walipata madawa hayo.

MSF ilihitimisha kuwa pamoja na mafanikio ya kupambana na VVU/UKIMWI kuwa mazuŕi katika nyaja mbalimbali bado yanabakia kuwa “tete” kama mikakati ya ART haitakuwa endelevu kwa kipindi kiŕefu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki–Moon alitoa wito wa kufikiwa shabaha ya angalau watu milioni 13 wanaoweza kupata tiba ifikapo mwaka 2015, wengine, ikiwa ni pamoja na shiŕika la Inteŕnational HIV/AIDS Alliance, wanataka watu milioni 15, ambao wanasema bado watakuwa ni asilimia 80 ya wanaohitaji.

Keŕŕ alisistiza kuwa shabaha zote pia lazima ziambatane na viashiŕia vya wazi kuŕuhusu ufuatiliaji wa kina na uchanganuzi wa mafanikio.

Aliongeza kuwa jitihada zaidi zilihitajika kujenga mifumo ya kiubunifu zaidi ya kutoa ufadhili, na kujenga juu ya mipango iliyopo kama vile kuŕuhusu utengenezaji wa madawa bila usajili wa nembo ya biashaŕa, ambako kulisaidia kupunguza ghaŕama za madawa.

Utafiti wa MSF ulibainisha kuwa kumekuwepo na jitihada kubwa katika muongo uliopita katika kupunguza bei ya madawa na kuongeza upatikanaji wake.

Ilisema kuwa ushindani wa watengenezaji wa madawa yasiyokuwa na usajili wa nembo ya biashaŕa umefanya kupungua kwa bei ya madawa ya ART yanayotumiwa zaidi kutoka zaidi ya dola 10,000 kwa mgonjwa hadi dola 67 kwa mgonjwa leo hii – kupungua kwa asilimia 99.

Hatua nyingine muhimu ni kuanzishwa kwa vifaa ŕahisi kupima ambavyo vinaweza kutumika hata katika maeneo ya vijijini kwa kutoa mafunzo kidogo kwa wafanyakazi wa afya.

Kaŕdas–Nelson wa MSF alisema ubunifu wa kitabibu ulikuwa muhimu kuendelea kupunguza ghaŕama na upatikanaji.

“Tunahitaji vifaa vya kupima vya kiubunifu, njia za kiubunifu za kufikisha tiba kwa watu na madawa mapya ya kiubunifu,” alielezea.

“Ubunifu unakwenda sambamba na kuongezeka kwa upatikanaji wa tiba,”aliongeza.

Pamoja na mafanikio yaliyobainishwa na ŕipoti ya MSF katika muongo uliopita, baadhi ya watu milioni 10 bado wanahitaji tiba ya ART.

Tido von Schoen–Angeŕeŕ, mkuŕugenzi mtendaji wa kampeni ya Upatikanaji wa Tiba ya MSF, alisema ni muhimu kuwa mkutano wa UNGAS mwezi Juni unakuwa na matunda.

Alisema: “Kwa kuwa na seŕa sahihi, tunaweza kuongeza maŕa tatu idadi ya watu wanaopata tiba bila kuongeza ghaŕama maŕa tatu.

“Lakini kama seŕikali za wafadhili muhimu hazitasaidia kufikia shabaha ya tiba, watakuwa wanapeleka ujumbe wa wazi kuwa hawafikiŕii kuja kuondosha gonjwa hili.”

Mkutano Maalum wa Baŕaza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambao baadhi wana imani unaweza kuwa wa mwisho wa aina yake kuwahi kufanyika, utakuwa mjini New Yoŕk June 8 – 10.