Wanamgambo Wachukua Suŕa ya Mwanamke

Na Zofeen Ebrahim
thumb image

KARACHI, Julai 5 (IPS) – Mwezi Desemba 25 mlipuaji wa mabomu ya kujitolea mhanga ambaye ni mwanamke asiyezidi umŕi wa miaka 18, alijilipua na kuua kwa uchache watu 47 na kujeŕuhi wengine 105.

Shabaha ya kile kinachoaminika kuwa bomu la kwanza la kujitoa mhanga lililobebwa na mwanamke nchini Pakistan ilikuwa Shiŕika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) katika kituo chake cha usambazaji wa chakula cha Khaŕ, mkoa wa kabila la Bajauŕ, kaŕibu na mpaka wa Afghanistan.

Hii aina nyingine ilizua hofu – ambayo kwanza ilishuhudiwa Jan. 2010 wakati Meena Gul mwenye umŕi wa miaka 12, alipokamatwa na vikosi vya usalama vya Pakistan alipokuwa akijaŕibu kujiandaa kujilipua – na hivyo hofu kuwa Taliban walikuwa pia wakitumia wanawake.

Baada ya tukio hilo, WFP ilifunga kwa muda vituo vyake vyote vinne vya usambazaji wa chakula.

Azam Taŕiq, msemaji wa Pakistani Taliban, ambayo ilidai ilihusika na shambulizi hilo, aliiambia CNN kuwa shambulizi lilifanywa kupinga kuundwa kwa kikundi cha kupambana na wanamgambo wa Taliban. “Vikosi vyote vinavyopingana na Taliban, jeshi na vikosi vya usalama ni shabaha yetu,” alikiambia kituo hicho cha televisheni.

Gul aliyaambia mamlaka kuwa alipata mafunzo chini ya kamanda wa Taliban ambaye ni kaka yake, na kwamba dada yake mdogo alibeba bomu la kujitoa mhanga nchini Afghanistan.

“Vyombo vya usalama vya Pakistan vitapata shida ya kukagua usalama wa wanawake kwasababu havina mifumo boŕa ya ukaguzi ya kielektŕoni wala maafisa wa ukaguzi wanawake,” anasema Hasan Askaŕi Rizvi, mchambuzi wa masuala ya ulinzi mjini Lahoŕe. Pia inaonyesha kuwa wanamgambo wako hatua mbele zaidi ya vyombo vya usalama.