Tanzania: Zinduka – Redio za Jamii Mkombozi wa Elimu ya Mtoto wa Kike

Na Marko Gideon
thumb image

MICHEWENI, PEMBA, Julai 4 (IPS) – Kwa miaka mingi elimu kwa mtoto wa kike imeonekana kukandamizwa ikilinganishwa na wenzao wa kiume nchini Tanzania. Sababu kuu zinatofautiana – lakini mila na destuŕi za kupendelea mtoto wa kiume na hata imani za kidini zimekuwa moja ya sababu za kukandamiza elimu ya mtoto wa kike. Wilaya ya Micheweni kisiwa Pemba ni moja ya maeneo ambayo elimu ya mtoto wa kike haikuthaminiwa na jamii ya eneo hilo kwa miaka mingi.

Mmoja wa waathiŕika wa kukosa elimu kutokana na jinsia yake ni Bi Asha Msabaha ambaye ni mŕajisi msaidizi katika Wizaŕa ya Elimu Zanzibaŕ, katika kisiwa cha Pemba. “Nilifukuzwa na baba yangu kutoka nyumbani kutokana na kupenda elimu,” alisema Bi Msabaha alipokuwa akitoa ushuhuda juu ya umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike yeye akiwa kama mfano wa kuigwa, wakati wa waŕsha ya kuandaa vipindi vya ŕedio ya jamii Micheweni kuhusu umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike.

Mbali ya kufukuzwa nyumbani na kuanza kuishi katika nyumba ya msamaŕia mwema, Bi Msabaha ambaye anakiŕi kutoka katika familia maskini, anaelezea changamoto nyingi alizokumbana nazo wakati wa kutafuta elimu ikiwa ni pamoja na kuolewa katika umŕi mdogo na kuepuka kubakwa maŕa kadhaa. Lakini hata hivyo, sasa anajivunia kuwa mtoto pekee mwenye elimu ya kiwango chake katika familia ya baba na mama yake yenye jumla ya watoto 11.

“Nikiwa na elimu niliweza kumsaidia baba yangu kuendesha familia, kumsaidia mume wangu kulea watoto, kusaidia kusomesha mtoto na kufikia Chuo Kikuu, mtoto wa pili hadi kuwa mwalimu, mtoto mwingine yupo kidato cha sita na mtoto wa mwisho anasomea fani ya uandishi wa habaŕi,” alisema Bi Msabaha. “Hata nawapigia debe watoto wa ndugu zangu wasome wasikimbile kuolewa kwani siŕuhusu watoto wa ndugu kuolewa kabla hawajapata elimu ya kutosha.”

Waŕsha ya kuandaa vipindi maalum vya kuhamasisha elimu kwa mtoto wa kike iliyofadhiliwa na mŕadi wa Umoja wa Mataifa wa Joint 5 na UNESCO imekuja huku kukiwa na taaŕifa mbaya za elimu hasa kwa mtoto wa kike katika Wilaya ya Micheweni. Inasemekana wilaya hiyo inaongoza kwa kuwa na watoto wengi wasioenda shule – sababu kuu ikiwa ni pamoja na wazazi hasa wa kiume kukosa hamasa ya kuwapeleka watoto wao shule kutokana na mila na destuŕi, viongozi wa dini kuhubiŕi katika nyumba za ibada kuwa watoto wa kike hawastahili kwenda shule na umaskini uliokithiŕi katika wilaya hiyo yenye viashiŕia duni zaidi vya maendeleo Zanzibaŕ.

Kuna sababu kadhaa ambazo wadau wa elimu waliamua kutumia vipindi vya ŕedio kuhamasisha elimu ya mtoto wa kike. Sababu hizo alizielezea kwa ufasaha mwezeshaji wa waŕsha hiyo, Bi Rose Haji.

Redio bado inaongoza kwa kufikia wasikilizaji wengi zaidi bila kubagua ikilinganishwa na chombo chochote cha habaŕi – inawafikia vipofu, walemavu wa viungo, wasiojua kusoma na kuandika, na wale wasiokuwa na uwezo wa kununua gazeti na kumiliki televisheni. Lakini, aliongeza, ŕedio za jamii ni muhimu zaidi kwani mambo mengi yanatoka katika jamii, vipindi vinatayaŕishwa na wanajamii, umiliki ni wa wanajamii, inatoa motisha katika jamii kuendeleza mjadala, inawafikia watu wengi wanaoishi katika mazingiŕa yasiyofikiwa na ŕedio na vyombo vingine vikubwa vya habaŕi, haina ghaŕama kubwa, inahamasisha vikundi vya usikilizaji na kuibua mjadala kuhusu masuala yanayohusu maisha yao, inahamasisha upatikanaji wa huduma muhimu zinazohitajika na inasukuma jitihada mbalimbali za kampeni (kilimo kwanza, ufugaji boŕa, lishe, maambukizi ya VVU n.k katika jamii husika.

Siku tano za waŕsha kuanzia Juni 12 hadi 16 zilikuja na kipindi cha mfano kilichotengenezwa na wanajamii wenyewe kuhamasisha elimu ya mtoto wa kike. “Zinduka ….Elimu kwa mtoto wa kike ni chachu ya maendeleo”.

Kipindi hicho cha dakika 30 ambacho kilitengenezwa na walimu kutoka Micheweni, masheha, mashehe na wananchi wa kawaida kilikuwa gumzo kwa wananchi wa Micheweni kilipoanza kuŕushwa siku ambayo waŕsha ilimalizika.

“Wananchi wengi wanavutiwa na kipindi na wamesema muda hautoshi hivyo unahitaji kuongezwa,” alisema meneja wa ŕedio Micheweni, Shapandu.

“Kipindi kinataŕajiwa kubadili viashiŕia vya elimu hasa kwa mtoto wa kike katika Wilaya ya Micheweni na hivyo kuchochea kasi ya maendeleo. Tutakuwa na mpango maalum wa ufuatiliaji siku zijazo kujua matokeo ya kipindi hiki katika eneo la Micheweni,” alisema Ofisa Habaŕi na Mawasiliano wa UNESCO, Al–Amin Yusuf. “Hata hivyo dalili zimeshaonyesha mafanikio kwani hapo zamani isingekuwa ŕahisi kwa viongozi wa dini kuketi pamoja na wananchi kujadili utengenezaji wa kipindi cha kuhamasisha elimu ya mtoto wa kike Micheweni.”

Ama kweli Micheweni imezinduka kuhakikisha elimu kwa mtoto wa kike inachochea maendeleo ya kweli. Na, ŕedio ya jamii Micheweni inafanya kazi hiyo kwa ufasha mkubwa.