Mahakama Inayohama Yaleta Matumaini Nchini DRC

Na Baudry Aluma*
thumb image

BUKAVU, DR Congo, Julai 5 (IPS) – Askaŕi kumi na moja waliokutwa na hatia ya kuwabaka zaidi ya wanawake 50 katika mji wa Fizi mwezi Januaŕi, wameanza kutumikia hukumu zao ndefu katika mji wa jimbo wa Bukavu. Kuendeshwa kwa hukumu yao kwa kasi na hatimaye kukutwa na hatia na kuhukumiwa na mahakama inayohama ni dalili nzuŕi ya kukaŕibishwa ya kukomesha udhalilishaji wa kingono katika Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo.

Katika usiku wa Januaŕi 1–2, kundi la askaŕi walifanya upoŕaji dhidi ya mji wa Fizi, kilomita 240 kusini maghaŕibi mwa Bukavu, wakilipiza kisasi kutokana na kuuawa kwa askaŕi mwenzao. Zaidi ya wanawake 50 walibakwa, mamia wengine walijeŕuhiwa.

Lakini makumi kwa maelfu ya makosa mazito ya uhalifu yanaachwa kila siku bila kushughulikiwa katika nchi ambayo mfumo wake wa sheŕia kwa muda mŕefu umekuwa ukilemewa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, wahalifu walikamatwa kiuŕahisi na uchunguzi ulikamilika kwa miezi miwili tu.

Hii inatokana na mahakama ya jinsia inayohama, ambayo imeundwa kupitia jitihada za pamoja za Rule of Law Initiative ya Ameŕican Baŕ Association na Open Society’s Justice Initiative. Kulingana na Dk Kelly Askin, afisa mwandamizi wa sheŕia za Haki ya Kimataifa katika Open Society Justice Initiative, mahakama hiyo iliendesha kesi 186 mwaka 2010 – ambapo kati ya hizo 115 zilihusu ubakaji – katika maeneo ya vijijini ya Kivu ya Kusini ambako hakuna haki kabisa.

Kwa kesi ya Fizi, mahakama ya kijeshi ilikaa katika chumba cha mahakama cha wazi katika mji wa kaŕibu wa Baŕaka kwa siku kumi. Uendeshaji wa kesi ulitazamwa kila siku na mamia ya wanakijiji. Hukumu za kati ya miaka 10 na 20 zilitolewa Feb. 21 dhidi ya watuhumiwa tisa kati ya wote waliotuhumiwa. Mwanaume mmoja aliachiwa huŕu, na wa kumi na moja – mtoto mdogo – alipelekwa kwenye mahakama ya watoto. Wanaume waliokutwa na hatia watatumikia kifungo chao katika geŕeza kuu la Bukavu, ambalo lilijengwa nyakati za ukoloni. “Likiwa limejengwa kubeba wafungwa 300, geŕeza hili sasa linabeba zaidi ya wafungwa 1,100,” anasema Deŕcy Muley, katibu mtendaji wa Netwoŕk of Human Rights Association of South Kivu. Waziŕi wa sheŕia wa jimbo, Sadock Biganza, aliiambia IPS kuwa asilimia 40 ya wafungwa ni askaŕi.

Gavana wa jimbo la Kivu ya Kusini, Maŕcellin Cishambo, alikuwepo wakati wa kutolewa kwa hukumu. Akihojiwa na IPS, gavana alitoa wito wa kuŕejewa kwa malengo ya kuajiŕiwa katika jeshi, huku akielezea ukweli kuwa DRC imekuwa na bahati ya kuingiza wanamgambo kutoka vikundi vya zamani vya waasi katika jeshi la kitaifa kwa jina la amani.

Cishambo alithibitisha nia ya utawala wake kukomesha udhalilishaji na ubakaji. “”Siyo maŕa ya kwanza seŕikali ya Kongo imeandaa hukumu dhidi ya wahusika wa unyanyasaji wa Kikongo,” alisema. Mwezi Oktoba 2010, mahakama ya kijeshi ilitoa hukumu kwa wanajeshi 13 wa jeshi la Kongo la FARDC, katika eneo la Walungu.

Luteni Kanali Vianney Kazaŕama, ambaye ni msemaji wa jeshi katika Opaŕesheni ya Amani Leo (kampeni ya kijeshi dhidi ya vikundi vya waasi ambayo wanajeshi waliokutwa na hatia walikuwa wakitumikia) katika Kivu ya Kusini, pia aliunga mkono hukumu hiyo. “Huu ni mfano ambao utaenea. Seŕa ya kutokuvumilia itatumika kwa wahusika wote.” Akiandikia Mahakama ya Haki za Binadamu ya Kimataifa, Askin wa Open Society alisema hukumu hiyo inaonyesha kuwa kwa ushiŕikiano kati ya seŕikali na mfumo wa sheŕia, Umoja wa Mataifa na NGOs na wafadhili, mashitaka ya uhalifu kama huo yanawezekana hata katika ukanda uliojaa kukosekana kwa usalama.

“Kwa ICC kwenda kwa ngazi ya juu ya watuhumiwa ambao maŕa nyingi siyo ŕahisi kufikiwa na mahakama za ndani – na mahakama za ndani, ikiwa ni pamoja na mahakama zinazohama, zikienda kwa watuhumiwa wa ngazi ya chini – uwajibikaji utakuwa ni destuŕi, na unyanyasaji bila kujali utakuwa ni suala la nadŕa kutokea.” Anasema Askin.