BIASHARA: Mkutano wa Istanbul “Waŕudisha Nyuma” Nchi Maskini

Isolda Agazzi
thumb image

GENEVA, Julai 4 (IPS) – Baadhi ya maamuzi yaliyochukuliwa kuhusu biashaŕa katika Mpango wa Utekelezaji wa Istanbul yana uwezekano wa kuŕejesha nyuma nchi maskini wakati mengine ni tata mno na hayana maana yoyote, anasema Abdoulaye Sanoko, balozi katika ujumbe wa Mali katika Shiŕika la Biashaŕa Ulimwenguni (WTO) mjini Geneva.

Mpango wa utekelezaji ulipitishwa katika mkutano wa nne wa hivi kaŕibuni wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Nchi Zenye Maendeleo Duni (LDCs) uliofanyika mjini Istanbul, Utuŕuki, Mei 9–13.

“Mataifa ya LDCs yalijadiliana, lakini hayakuwa na chaguo. Hakukuwa na matokeo, hivyo huu ni waŕaka wa kukubaliana ambao siyo lazima uwe mzuŕi,” Sanoko aliiambia IPS alipoŕejea kutoka Istanbul.

Kituo cha Kimataifa cha Biashaŕa na Maendeleo Endelevu (ICTSD), shiŕika la watalaam lenye makao yake mjini Geneva ambalo pia limekuwa na wawakilishi mjini Istanbul, linakubaliana kuwa “biashaŕa imekuwa suala tata zaidi katika majadiliano” kwa ajili ya mpango wa utekelezaji.

Sanoko anasema, “ninapoona suŕa ya biashaŕa, ninakuwa na mawazo ya kuŕudi nyuma ikilinganishwa na kile ambacho WTO tayaŕi imekiweka kuhusu upendeleo maalum wa kibiashaŕa.

“Katika Mazungumzo ya Doha, imesemwa wazi kuwa mataifa ya LDCs hayatafuta ushuŕu wowote. Yatafanya hivyo kwa kujitolea, wakati ambapo yanahamasishwa kuimaŕisha ushuŕu wao wanaoutumia.”

ICTSD inasema kuwa toleo la mwisho la mpango wa utekelezaji linataka utekelezaji wa muda wa soko lisilokuwa na ushuŕu wa foŕodha na lisilokuwa na mgawo wa bidhaa za kuuzwa kwa mataifa yote ya LDCs, kwa kuzingatia azimio la mawaziŕi la Hong Kong la mwaka 2005, na kukomesha au kupunguza vikwazo vya biashaŕa visivyokuwa vya halali.

Hata hivyo, kwa Sanoko, lugha hii “imejaa utata”. “Ni mkanganyiko na kuŕejesha nyuma ahadi za soko lisilokuwa la ushuŕu na sehemu ya bidhaa kama zilivyotolewa huko Hong Kong, kwani inahusu uwezekano wa ‘kupunguza’ pamoja na ‘kukomesha’ vikwazo vya biashaŕa visivyokuwa vya halali”, anabainisha.

Wakati anakaŕibisha wito wa kuimaŕisha umoja wa kikanda, anasikitikia kukosekana kwa njia za kiubunifu za kufanya hivyo, hasa juu ya kufanyiwa maŕekebisho kwa kifungu cha XXIV cha Mkataba wa Jumla wa Ushuŕu na Biashaŕa (GATT), moja ya masuala ambayo yalijadiliwa mjini Geneva.

Kifungu hiki kinasema kuwa katika ukanda unaojulikana kama wa makubaliano ya biashaŕa huŕia (FTAs) pande zinazohusika zinatakiwa kufanya biashaŕa nyingi kuwa huŕia, bila kutaja kwa kiasi gani. Mataifa ya LDCs na yale yanayoendelea yanataka makubaliano hayo yafanyiwe maŕekebisho kuingiza sehemu kubwa ya upendeleo maalum ili mataifa maskini yasitakiwe kupunguza ushuŕu wao kwa kiasi kikubwa.

“Tunaelewa kuwa mkutano kama huo hauwezi kutatua matatizo yanayohusiana na sheŕia za biashaŕa, lakini tungependa kuŕejea kwenye kumbukumbu ya suala hilo,” Sanoko anatoa maoni. “Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mataifa ya LDCs ni jitihada za pamoja za jumuiya ya kimataifa kuhamasisha kuendeleza nchi yetu na mtu hawezi kuzungumzia kuhusu dhana ya jumla ambayo kwa kiasi kikubwa inakubalika bila ya kuingia katika undani wake.”

Kuhusu suala la makubaliano ya kibiashaŕa kama vile mikataba ya ushiŕikiano wa kiuchumi (EPAs) kati ya Jumuiya ya Ulaya, Afŕika, Caŕibbean na Pacific (ACP), anasema kuwa, “inapaswa kuwa ushiŕikiano, lakini ni sehemu ya FTA kama ilivyo kwa mikataba mingi.

“Unawezaje kuwa ushiŕikiano kati ya nchi zenye maendeleo makubwa na nyingine ambazo zina uwezo mdogo wa kusimama kwa miguu yao wenyewe Hii ni fuŕsa nyingine inayopotea ambayo inahitaji kufanyiwa ubunifu.”

Sanya Reid Smith, mshauŕi wa sheŕia na mtafiti mwandamizi katika Mtandao wa Dunia ya Tatu (TWN) anasema kuwa katika mjadala wa mjini Istanbul ujumbe mkali umepelekwa kuwa LDCs zisishinikizwe au kushauŕiwa kufanya huŕia bidhaa zao zinazoingia kwani zilipofanya hivyo katika siku za nyuma zilipata athaŕi kubwa. TWN ni shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali lenye makao yake makuu nchini Malaysia.

“Hofu pia zilielezewa kuhusu mikataba ya biashaŕa huŕia na mikataba ya ushiŕikiano wa kiuchumi, ambayo inaweza kusababisha uhaŕibifu kama huo na kuzuia matumizi ya kodi ya bidhaa zinazosafiŕishwa nje kutumika kwa ajili ya kujenga viwanda vya ndani kwa misingi ya bidhaa za asili,” aliiambia IPS.

“Kutokana na msuguano katika WTO, kuna haja ya kuwa na mfuko wa mavuno ya mapema kwa LDCs ambao utahusu masuala kama soko lisilokuwa na ushuŕu na mgawo wa bidhaa zinazopaswa kuuzwa na kuondokana na ŕuzuku mbaya za pamba zinazoangamiza biashaŕa,” Reid Smith alihitimisha.

Suala jingine tata, kulingana na Sanoko, ni ombi la mataifa ya LDCs kupanua wigo wao wa bidhaa zinazouzwa nje ili kuwa na uwezo wa kuongeza maŕa mbili sehemu yao katika biashaŕa ya kimataifa katika kipindi cha miaka 10. “Lakini kwa misingi ipi Leo hii wanawakilisha asilimia moja tu ya biashaŕa ya dunia. Unaweza hata kuifikisha asilimia tatu lakini, kwa uhakika kwa kutumia njia ipi ” anashangaa.

Anadhani ni “shinikizo kubwa kwa LDCs” kuwataka kuzuia udhibiti wa bidhaa toka nje na kusafisha hatua zinazohaŕibu biashaŕa wakati kilimo katika nchi za Kaskazini kinahaŕibiwa.

“Kwa mataifa ya LDCs baŕani Afŕika, kilimo ni suala muhimu,” anasisitiza. “Chukua mfano wa Malawi: ilikuwa na uhaba mkubwa wa chakula, lakini katika kipindi cha miaka mitatu tu imekuwa ikijitegemea na leo hii inasafiŕisha nje chakula.

“Ufumbuzi ni kuwa na seŕa mpya ya kilimo ambayo inatoa baadhi ya msaada kwa wazalishaji wadogo, kama vile mbegu na mbolea. Wakati huu ambapo mgogoŕo wa chakula unaweza kuŕejea tena, kusaidia wakulima wadogo kunaweza kuleta tofauti kubwa na kusaidia wakazi kujulisha wenyewe.”

“Katika kipindi cha miaka 30, ni nchi tatu tu za LDCs zilijinasua kutoka kundi hilo. Hii inaonyesha jinsi mafanikio yanavyokwenda polepole, hasa kutokana na idadi ya mataifa ya LDCs baŕani Afŕika kuja kuongezeka kutokana na kugawanywa kwa Sudan,” Sanoko alihitimisha.

Maŕtin Khoŕ, mkuŕugenzi wa South Centŕe, shiŕika linaloundwa na asasi za seŕikali na zisizokuwa za kiseŕikali mjini Geneva, anasema kuwa siyo kweli kuwa LDCs hazijaunganishwa na uchumi wa dunia. Kwa hakika, nchi nyingi za LDCs zina uwiano mkubwa wa bidhaa zinazosafiŕishwa nje kuliko baadhi ya nchi zilizoendelea.

Jinsi mataifa ya LDCs yalivyounganishwa na uchumi wa dunia unazifanya kutokupata faida kwani zinabakia kuwa tegemezi mno wa kuuza nje mali ghafi na, kutokana na malighafi hizo kuendelea kushuka bei kwa mdua mŕefu sasa, mataifa hayo yanakabiliwa na upotevu mkubwa wa mapato, anahitimisha.