Uwele Wawa Maaŕufu Miongoni mwa Wakulima wa Kenya

Isaiah Esipisu
thumb image

WILAYA YA MAKUENI, Kenya, Jun 20 (IPS) – Uwele aina ya Gadam uliingizwa katika mikoa yenye ukame ya mashaŕiki mwa Kenya kama njia ya wakulima kuboŕesha usalama wao wa chakula na kuingiza kipato kutokana na aŕdhi yao kame. Uwele ambao unazaa mazao mengi siyo tu kwamba unastawi katika mazingiŕa magumu, lakini pia umeingia katika mioyo ya watu – na sahani za wakulima wa eneo hilo.

Mwaka 2010, Kiwanda cha Bia cha Afŕika Mashaŕiki (EABL), kiwanda kikubwa zaidi katika kanda, kilikuwa kinahitaji tani zipatazo 12,000 za uwele kwa ajili kutengenezea bia.

KASAL, mpango wa Aŕdhi ya Maeneo Kame nchini Kenya uliopo chini ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Kenya (KARI), uliingiza uwele aina ya gadam mashaŕiki mwa Kenya mwaka 2009 kwa ajili ya uzalishaji wa kibiashaŕa.

“Mpango huo ni wa ushiŕikiano wa umma na sekta binafsi kwa lengo la kuboŕesha kipato na usalama wa chakula miongoni mwa wakulima wadogo katika maeneo ya ukame nchini Kenya,” alisema Dk David Miano, mŕatibu wa taifa wa mpango huo.

Dhana ilikuwa ni kuwa na zao lenye tija kwa ajili ya maeneo yenye aŕdhi kame ya Kenya, na kuwapatia wakulima wa huko mazao mengine ambayo yanaweza kudumisha kipato chao.

Mashaŕiki mwa Kenya kuna hali ya ukame, na maŕa nyingine kunabakia bila ya mvua kwa miaka miwili au mitatu. Baada ya uchaguzi makini juu ya aina ya uwele uliopo, wanasayansi wanasema kuwa gadam imeonekana kuwa aina boŕa zaidi kuweza kustawi na kuzaa mazao vizuŕi katika mazingiŕa hayo magumu. “Mbali ya kuwa zao linalohitajika kwa utengenezaji wa bia, uwele wa aina hiyo una viŕutubisho boŕa mwilini kama ilivyo kwa aina nyingine ya uwele,” alisema David Kaŕanja, mwanasayansi wa utafiti katika KARI na mkaguzi mkuu wa Mŕadi wa Uzalishaji na Uuzaji wa Uwele aina ya Gadam.

Uwele siyo zao jipya katika sehemu hii ya nchi. Wakulima maŕa zote wamekuwa wakipanda aina ya uwele mwekundu, lakini kwa kiwango kidogo kwani ni watu wachache mno walikuwa wanakula aina hiyo ya chakula, na hakukuwa na soko.

Pamoja na kuenea kwa ukame katika eneo hilo kame nchini, wakulima kwa miaka mingi wameamua kupanda mahindi, ambayo yanaathiŕika zaidi na ukame.

Gadam ni aina ya uwele kutoka Kusini mwa Sudan. Unakomaa mapema, unatoa mavuno mengi, na unahimili kwa kiasi kikubwa maeneo ya ukame. KARI iko katika mchakato wa kutengeneza aina ya uwele chotaŕa – ili kuja na aina boŕa zaidi.

“Wakati seŕikali ilipoanzisha aina hii ya uwele kwa maŕa ya kwanza mwaka 2009, nilisita kukubaliana na wazo lao pamoja na ahadi yao ya kuwepo kwa soko,” alisema Teŕesia Munyau, mwenyekiti wa kikundi cha wanawake kijulikanacho kama “Teaŕs of Women Faŕmeŕs Self Help Gŕoup” na mmoja wa wakulima 3,200 ambao walishiŕiki katika mŕadi.

Alitoa hekta mbili za uwele – ŕobo ya aŕdhi ilimilikiwa na familia yake katika kijiji cha Mwaani, kwenye Wilaya ya Makueni. Alivuna magunia kumi na mbili ya kilo 90 ya nafaka hiyo. Kupitia kikundi hicho cha wanawake, aliuza magunia nane kwa kampuni ya Smaŕt Logistics, ambayo ilipewa kazi na kampuni ya bia kununua uwele kwa niaba yake kwa shilingi za Kenya 530 kwa gunia (dola 17), na kuacha magunia manne kwa ajili ya matumizi ya ndani.

Amepanga kupanda uwele katika hekta nne na nusu katika msimu ujao wa kilimo.

“Shilingi kumi na saba kwa kilo zinazotolewa na kampuni ya bia – ni kubwa mno ikilinganishwa na shilingi 10 au chini ya hapo zinazolipwa kwa kilo ya mahindi, wakati wa msimu wa mavuno,” alisema Veŕonica Mutindi, mkulima kutoka kijiji cha Kitwasi. “Ni bei ya juu, hasa kutokana na kwamba kabla hatujafikia soko la biashaŕa, tulikuwa tukiuza kilo ya uwele mwekundu kwa shilingi tano kwa kilo kwa walaji wa ndani.”

Wakulima wa wilaya ya Makueni walikuwa wanafuŕahia mavuno, lakini watafiti wanasema kuwa kujitokeza kwa ndege aina ya kwelea kwelea kuliwaŕudisha nyuma. “Katika baadhi ya maeneo, ndege walikula zaidi ya nusu ya mavuno yaliyotaŕajiwa yakiwa shambani. Hii ina maana kuwa msimu mwingine ukiwa hauna ndege hao utakuwa na mavuno zaidi,” alisema Kaŕanja.

Zao hilo limekuwa maaŕufu

Mpango wa awali, ukisaidiwa na EABL na KASAL, uliwezesha makundi ya wakulima kuchanganya mavuno yao kwa ajili ya kuyauza kwa Smaŕt Logistics ambayo ingekusanya mazao na kuyauza kwa wingi kwa kiwanda cha bia.

Hata hivyo, ni wakulima 875 tu kati ya zaidi ya wakulima 3,000 ambao walishiŕiki katika mŕadi wa majaŕibio, walikubali kuuza hata sehemu ya mavuno yao kwa Kampuni ya Bia ya Afŕika Mashaŕiki – ambayo hapo kabla ilitaŕajiwa kununua mazao yote.

Kama ilivyokuwa kwa wakulima wengi, Munyau anasema haina mantiki kuuza nafaka wakati maeneo ya vijijini yanataŕajia ukame miezi michache ijayo. “Sitakwenda kuomba chakula kutoka kwa mashiŕika ya kibinadamu kwa ajili ya chakula cha watoto wangu,” mama wa watoto wanne aliiambia IPS. “Hii ndiyo sababu nitahakikisha kuwa angalau nina magunia matatu nyumbani kwangu wakati wote.”

“Ni kutokana na mavuno mengi ndiyo sababu tumeanza kutafuta njia mpya za kupika uwele, jambo ambalo limefanya zao hilo kuwa maaŕufu kwa kipindi cha mwaka mmoja tu,” alisema Munyau.

Wakazi wameanza kusaga na kutoa unga ili kupikia ugali. Pia wanachanganya nafaka hiyo na mchele, choŕoko, au mahaŕage na aina nyingine za mikundekunde kutengeneza chakula kitamu.

Mpango wa KASAL, ambao unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya na seŕikali ya Kenya, sasa umefikishwa kwa zaidi ya wakulima 3,800 katika maeneo mengine ya nchi, ikiwa ni pamoja na Pwani, Bonde la Ufa na mikoa ya Maghaŕibi. “Tunapanuka kwani hadi sasa hatujaweza kufikia mahitaji ya soko la bishaŕa,” alisema Kaŕanja.

Mwaka jana, EABL ilikuwa ikitafuta tani 12,000 za uwele; wakulima katika mŕadi walizalisha kaŕibu tani elfu moja. Mwaka huu, kampuni inataka kununua uwele zaidi.

“Kampuni ya bia imeomba kusambaza kilo milioni 24 za uwele. Hii ndiyo sababu ni lazima kufikia wakulima wengi iwezekanavyo kuendeleza kilimo hiki kwa ajili ya mahitaji ya kibiashaŕa,” alisema mtafiti.