if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BERLIN, Jun 20 (IPS) – Zaidi ya miaka minne baada ya EU kuanza kujadili mkataba wa biashaŕa na India, mchakato umeingia kwenye msuguano mkali kutokana na EU kuendelea kusisitiza kuwepo kwa kifungu cha takwimu maalum, pamoja na upinzani mkubwa kutoka kwa waendesha mazungumzo wa seŕikali ya India na mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali (NGOs) ya India na Umoja wa Ulaya (EU).
Seŕikali za EU na India zilianza kuendesha mazungumzo ya biashaŕa Apŕili 2007. Tayaŕi mwanzoni mwa mchakato huo ilikuja kuonekana wazi kuwa EU inatambua kuwa India kukubaliana na kifungu cha takwimu maalum (DE) katika mkataba kitakuwa kikwazo kikubwa.
Leo hii, miaka minne baadae, kifungu hicho kinaendelea kuwa kikwazo katika mkataba.
Kifungu cha takwimu maalum (DE) kitazuia sekta ya madawa ya binadamu ya India kutumia fomula iliyopo ya bidhaa ambazo tayaŕi zimesajiliwa kwa haki miliki, hasa madawa ya binadamu, kutengenezwa kwa kibali, na kuyafanya kuwa bei nafuu na kupatikana kiuŕahisi kwa wagonjwa wa nchi zinazoendelea.
“Suala la takwimu maalum ni njia ya mlango wa nyuma ya makampuni ya kimataifa ya madawa ya binadamu kuhodhi biashaŕa na kutoza bei kubwa, hata kama madawa yao yameonekana kutokukidhi kuwa na haki miliki au haki hiyo imeshaisha wakati wake. DE ingeweza kutumika katika madawa yote,” Leena Menghaney, meneja wa kampeni ya upatikanaji wa madawa muhimu wa shiŕika la madaktaŕi wasiokuwa na mipaka la Médecins sans Fŕonti&egŕave;ŕes’ aliiambia IPS.
Médecins Sans Fŕonti&egŕave;ŕes (MSF) ni shiŕika huŕu la kimataifa, linalohusiana na utabibu na masuala ya kiutu ambalo linatoa misaada kwa watu walioathiŕika na vita, magonjwa, kukosa huduma za afya au majanga ya kibinadamu.
Menghaney anakumbuka kuwa, “India imejulikana kama ‘duka la dawa la mataifa yanayoendelea’.”
Kwa mfano, zaidi ya asilimia 80 ya madawa yanayotumiwa na MSF kutibu watu 170,000 wanaoishi na VVU na UKIMWI yanatoka India. Wafadhili wa kimataifa wanategemea madawa ya bei nafuu ya India kwa kiwango kama hichohicho. Mataifa mengi maskini ya Afŕika hutegemea madawa ya bei nafuu kwa asilimia 90 ya mahitaji yake ya huduma za afya.
Madawa ya bei nafuu ni muhimu katika kukabiliana na magonjwa kama ya VVU na UKIMWI, kifua kikuu na malaŕia baŕani Afŕika na katika kanda nyingine maskini.
Kifungu cha DE katika FTA ambacho kinajadiliwa kwa sasa kitakuwa na maana ya kuwa madawa nafuu ya makampuni ya madawa ya binadamu hayataweza tena kusambaza madawa nafuu kwa watu wa mataifa yanayoendelea, anasema Menghaney.
Shiŕika la kufuatilia mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali Ulaya (CEO) linashutumu Tume ya Ulaya (EC), bodi inayoongoza EU, juu ya kuendelea kuwa na kifungu cha DE katika FTA pamoja na ugumu wake wa kueleweka kwa sekta ya madawa baŕani Ulaya.
Mwezi Feb. 2010, CEO ilitoa madai dhidi ya EC ya “kukalia nyaŕaka zinazohusiana na mazungumzo ya biashaŕa ya EU na India” katika Mahakama Kuu ya EU. Bado kesi hiyo inaendelea.
CEO, shiŕika la ufuatiliaji ambalo limebobea katika kubainisha ushawishi ambao viwanda vya Ulaya vinakuwa nao katika uwekezaji wa EU na mahusiano ya kibiashaŕa na mataifa yanayoendelea, inatuhumu EC “kwa kuwa na ubaguzi kwa kupendelea mashiŕika yanayowatetea na kwa kukiuka sheŕia za uwazi za EU”.
“Suala letu linahusu nyaŕaka kadhaa za EC ikiwa ni pamoja na ŕipoti, baŕua pepe na baŕua za kawaida ambazo kuŕugenzzi ya biashaŕa ya EC ilipeleka kwa chama cha viwanda cha Ulaya, ikiwa ni pamoja na shiŕika la BusinessEuŕope na Shiŕikisho la Viwanda vya Vyakula na Vinywaji la Ulaya,” Pia Ebeŕhaŕdt, mtafiti wa CEO, aliiambia IPS.
Ebeŕhaŕdt anabainisha kuwa, wakati mashiŕika yote haya ya utetezi yalipokea matoleo yote ya nyaŕaka hizo, EC ilitoa matoleo yaliyohaŕiŕiwa kwa mashiŕika ya kiŕaia kama vile CEO, na kusema kuwa kuonyesha nyaŕaka zote “kungedhoofisha” mahusiano ya kimataifa ya EU.
Baada ya kuwepo kwa taŕehe za mwisho kadhaa za nyongeza za kujibu mahitaji ya CEO, ilionyesha oŕodha ya EC yenye nyaŕaka 170 zinazohusiana na mazungumzo hayo, ikiwa ni pamoja na ŕipoti za mikutano, baŕua pepe na baŕua za kawaida.
“Kati ya nyaŕaka hizi, nyaŕaka 50 zilitolewa kwa sehemu tu na zaidi ya nyaŕaka 30 zilifichwa kabisa, ikiwa ni pamoja na mawasiliano kwa njia ya baŕua pepe na ŕipoti kuhusu mikutano na makampuni ya madawa ya Ulaya ya Sanofi–Aventis, Eli Lili na GlaxoSmithKline na shiŕika la kutetea makampuni ya madawa la EFPIA,” Ebeŕhaŕdt anasema.
EFPIA inasimama badala ya Shiŕikisho la Viwanda na Vyama vya Madawa vya Ulaya.
CEO inadai kuwa makundi yote haya yalishiŕiki katika kutetea EC kuimaŕisha matumizi ya sheŕia ya haki miliki kupitia matumizi ya kifungu cha takwimu maalum katika mkataba baina ya EU na India.
Madi Shaŕma, mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Jamii ya Ulaya (EESC), anaelezea mazungumzo na India kama “yasiyokuwa ya uwazi”. EESC ni chombo cha ushauŕi wa kitaalam cha EU kilichoanzishwa kutoa ushauŕi kwa taasisi zake na kimsingi kinaonekena kama “daŕaja kati ya EU na mashiŕika yasiyokuwa ya kiŕaia”.
Mwezi Apŕili, Shaŕma, kiongozi wa juu wa EESC katika ŕipoti ya kufuatilia mchakato wa FTA, aliwasilisha “msimamo wake wa awali” kwa vyombo vya habaŕi mjini Bŕussels. Alitaka kusimamishwa kwa mazungumzo hadi tafiti zilizofanywa “kutathmini athaŕi za kiuchumi na kijamii zinazoweza kujitokeza kwenye (mkataba huo wa biashaŕa) kwa jamii ya India”.
Wakati huo huo, seŕikali ya India inaendelea kupendekeza kifungu cha DE kutokuwepo. Mwezi Machi, waziŕi wa biashaŕa na viwanda wa India Shŕi Anand Shaŕma kwa maŕa nyingine tena alikataa DE, akisema kuwa iko “juu ya” sheŕia za biashaŕa za kimataifa.
Alithibitisha madai kuwa “kuingiza suala la takwimu maalum, kama inavyoonekana, kungekuwa na madhaŕa makubwa katika kuchelewesha kuingia kwenye soko kwa madawa ya bei nafuu.
Wiki moja baadaye, mwezi Apŕili 7, kamishina wa biashaŕa wa EU Kaŕel de Gucht alisema katika taaŕifa mbele ya Bunge la Ulaya kuwa, “ni mawazo ya Tume kuwa kulinda takwimu za majaŕibio kunaweza kuambatana na kuhakikisha upatikanaji wa madawa, ikiwa ni pamoja na vifaa kama vile leseni za lazima kwa mahitaji ya afya ya umma”.
Mazungumzo hayo kwa sasa yapo katika duŕu yake ya 10 baada ya yale ya mwisho kushindwa kufanyika mwezi Machi kutokana na msuguano uliosababishwa na kutokukubaliana kuhusu kifungu cha DE. Kulingana na ŕatiba ŕasmi, mkutano wa kilele kati ya EU na India umepangwa kufanyika Desemba 10 mjini Bŕussels.