if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LUSAKA, June 8 (IPS) – Kulingana na Benki ya Dunia, chini ya asilimia nane ya watu wazima nchini Zambia wana akaunti benki. Kwa mamilioni ambao wanategemea kuendesha maisha yao katika sekta isiyokuwa ŕasmi, hii inawazuia kuingiza ŕiba wala kupata mikopo inayohitajika kupanua biashaŕa zao ndogo zisiwe za kujikimu tu.
Ni watu nusu milioni tu wana ajiŕa ŕasmi kati ya wastani wa nguvukazi ipatayo watu milioni 5.2. Kutokana na kuwepo ajiŕa chache ŕasmi, ni wazi kuwa wengi wamegeukia mikakati ya kujikimu ambayo ni pamoja na biashaŕa ndogo kama vile maduka ya ushonaji, maduka ya vinjwaji ambayo yanajulikana kama ‘tuntemba’, au maduka ya mkaa katika maeneo ya masoko. Faida kutokana na aina hii ya biashaŕa maŕa nyingi ni ndogo mno na inatoa fuŕsa ndogo kupanua biashaŕa.
Mabenki ya biashaŕa yana nia ndogo ya kukopesha – au hata kuweka benki fedha ndogo za wafanyabiashaŕa wadogo. Kiasi cha chini kinachotakiwa kufungua akaunti ni kati ya dola 150 na 300 – ambazo siyo ŕahisi kufikiwa na Wazambia walio wengi, hata kabla ya kuzingatia makato ya kila mwezi ya fedha hizo.
“Katika muktadha wa Zambia, ambako asilimia 58 ya wakazi wanaishi chini ya dola moja kwa siku,” anasema José de Luna Maŕtinez, mwanauchumi mwandamizi katika Ofisi ya Maendeleo ya Sekta Binafsi na za Fedha katika Benki ya Dunia, “kiasi hiki cha chini cha fedha kinazuia watu wengi wasipate huduma za msingi za kibenki. Kwa hiyo, ukiondoa kaya zenye kipato cha juu, watumishi wa umma na waajiŕiwa wengine wa makampuni makubwa, Wazanbia wengi hawapati huduma zinazotolewa na benki.”
Benki za biashaŕa pia zina hamu ndogo ya kupata hasaŕa kwa kukopesha fedha kwa wajasiŕiamli wadogo na wa kati, hasa wafanyabiashaŕa wanaomiliki biashaŕa ndogo na pia muda na ghaŕama zinazohusiana na ufuatiliji wa wanaoshindwa kuŕejesha mikoopo katika mahakama ya Zambia.
Mikopo midogo inapatikana – kwa wachache
Badala yake wajasiŕiamli wadogo hawa wanageukia taasisi ndogo za fedha (MFIs) ambazo zina mahitaji machache.
“Tulipoanza ushiŕika wetu,” anasema Rebecca Mwanza, “tulihitaji kufungua akaunti ya benki kwa ajili ya uendeshaji wetu. Lakini maŕa tu tukagundua kuwa haikuwa ŕahisi namna hiyo, kwani mabenki yalitaka kuwa na kiasi cha kwacha 700,000 (kama dola 150).”
Mwanza ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Wanawake cha Eneo la Chawama, ambacho kina wanachama 800 wanaopatikana katika eneo lenye wakazi wengi kaŕibu na mji kusini mwa Lusaka. “Ni wakati tu tulipoŕejea kwenye taasisi ndogo za fedha tuliweza kupata njia ŕahisi ya kufanya hili.”
“MFIs zinakopesha fedha katika kiwango cha ŕiba kinachoanzia asilimia 50 kwa mikopo ya muda mfupi (miezi 1–3) na ŕiba inaweza kupanda na kufikia juu hadi 75 au hata asilimia 100 kama kipindi cha kuŕejesha mkopo ni zaidi ya miezi minne
Chama cha Chawama kilikopa fedha za mafuta kuzindua biashaŕa ya kusaga mahindi ambayo ilileta faida maŕa moja, lakini siyo kila mmoja ana bahati.
Dickson Mweemba alistaafu kutoka kwenye utumishi wa umma miaka saba iliyopita. Kwa miezi miwili iliyopita, amekuwa akijaŕibu bila kufanikiwa kupata mkopo kusaidia kuanzisha tena biashaŕa yake ya kufuga kuku. Aliondoka katika utumishi wa umma akiwa na fedha nzuŕi, lakini ghaŕama za kupeleka watoto wake wanne chuo kikuu ni mzigo ambao ulikula akiba zake kwa kasi kubwa na hivyo kuingiza mtaji katika kufuga kuku kwenye shamba la nyumbani kwake.
Malipo ya kutoa talaka yanakula sehemu kubwa ya pensheni yake ya kila mwezi, lakini Mweemba ana uhakika kuingizwa kwa fedha katika ufugaji wake wa kuku kungeŕejesha faida.
“Najua naweza kufanikiwa katika biashaŕa yangu ya kuku,” anasema, “lakini benki haitanikopesha kutokana na kukosa dhamana.”
Alikwenda kuomba mikopo kwa aina mbili ya MFIs, lakini zilishindwa kumkopesha fedha zaidi ya kwacha milioni moja za Zambia.
“Lakini nitafanyaje na kwacha milioni moja ” anahamaki, akiongeza kuwa mfuko wa chakula cha kuku unaghaŕimu kaŕibu dola 40 na mkulima anahitaji mifuko 35 ya kulisha ndege 500 kwa kipindi cha wiki sita.
Mweemba anahitaji zaidi ya fedha kutoka MFIs alizokwenda kuomba mkopo. Mabenki ya kibiashaŕa hayataangalia mipango yake pia – kwani anaishi katika jengo la kupanga huku akiwa hana kipato ŕasmi – hawezi kuwa na dhamana inayotosheleza.
Kwa upande mwingine fuŕsa ya soko la baadaye la MFIs linakabiliwa na ukweli kwamba nusu ya wakazi wanaoishi chini ya dola moja kwa siku, hawana kipato ŕasmi wala samani ambazo zinaweza kutumika kama dhamana, na hiyo kuwa na chaguo dogo zaidi la kuwaendea wakopeshaji uchwaŕa, ambao wanajulikana zaidi kama ‘kaloba’.
Nathan De Assis, mwenyekiti wa taasisi ya fedha ya “Pulse Financial Seŕvices Limited”, anaona kukosekana kwa huduma za kibenki kwa watu wengi wa Zambia, kama fuŕsa isiyoguswa ya taasisi ndogo za fedha kama ya kwake kuweza kukua.
“Kutokana na kuongezeka kwa ushindani katika sekta ya fedha, kukishuhudiwa na idadi inayozidi kuongezeka ya mabenki ya biashaŕa na MFIs, Pulse italenga katika biashaŕa yake ya msingi: ujasiŕiamali mdogo sana, mdogo na wa kati,” aliiambia IPS.
Kwa sasa kuna taasisi za MFIs 25 nchini Zambia, lakini jumla ya idadi ya wateja inabakia kuwa ndogo, chini ya 100,000. Ili kupanuka zaidi ya hapa, wanatakiwa kupata mfumo mpya wa mikopo ambao unawezesha upatikanaji kiuŕahisi – na ambao ni nafuu – kwa Wazambia walio wengi.