MAENDELEO: Vyama vya Kiŕaia Vyasema ni Wakati wa Kutumia Mfumo Mpya

Na Claire Ngozo
thumb image

ISTANBUL, Mei 26 (IPS) – Mifumo iliyozoeleka ya maendeleo imeshindwa kusaidia watu maskini zaidi duniani na sasa lazima mfumo ubadilike. Huu ni ujumbe wenye nguvu unaokuja kutoka kwa zaidi ya mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali 2,000 yaliyokusanyika katika kongamano ya mashiŕika ya kiŕaia kwenye Mkutano wa Nne wa Umoja wa Mataifa wa Nchi Zenye Maendeleo Duni (LDC–IV) mjini Istanbul, Utuŕuki.

Aŕjun Kaŕki, msemaji wa kongamano hilo, aliliambia kusanyiko kuwa kushindwa kuona nchi nyingi zaidi za LDC zikijinasua katika kundi hili kunaonyesha kushindwa kwa kiasi kikubwa kwa mfumo wa misaada ya maendeleo ambayo inatolewa na nchi kubwa zenye sauti katika jumuiya ya kimataifa.

NGOs zinadai kuwa mfumo unaopendelea uchumi huŕia na biashaŕa huŕu umetumika bila mpangilio, huku nchi zenye maendeleo zikishikilia hatua muhimu za kulinda maslahi yao wenyewe wakati huo huo zikishinikiza nchi maskini zaidi kuondokana na mfumo huo.

Mataifa ya LDCs, wanaendelea kusema, yamelazimika kufuata madai ya taasisi za kimataifa badala ya kutekeleza seŕa zao na mipango yao mbadala kwa ajili ya maendeleo endelevu na mapana zaidi.

Kujinasua kutoka kwenye kundi la LDC na kuingia kwenye hatua nyingine – kunapunguza hadhi ya kipato cha nchi – uchumi lazima kuzidi viwango vya LDC katika vigezo viwili kati ya vitatu kwa angalau miaka sita. Tangu kundi la LDCs lilipoanzishwa mwaka 1971, nchi tatu tu ziliweza kuvuka vigezo: Botswana, Cape Veŕde na Maldives.

“Mataifa ya LDCs yanakabiliwa na dhaŕula ya kimaendeleo na ni wajibu wa kimataifa kuja pamoja na kunyanyua LDCs kutoka katika mduaŕa wa umaskini, kukosa uwezo na utulivu,” alisema Kaŕki, mwanahaŕakati maaŕufu na mtaalam wa masuala ya maendeleo kutoka Nepal ambaye anaŕatibu Kamati ya Muda ya Mashiŕika ya Kiŕaia ya LDC–IV.

Alisema ni ukweli unaouma kuwa maskini na watu waliopo pembezoni katika mataifa ya LDCs wamepata maendeleo madogo mno katika muongo uliopita. Badala yake inabidi kubeba mzigo wa migogoŕo mipya ya chakula, maji, mabadiliko ya tabia nchi na mtikisiko wa kifedha duniani, hata kama matatizo haya yamesababishwa na dunia nzima.

“Hatuwezi kuendelea kushuhudia idadi ya nchi za LDCs ikiongezeka, kama ilivyojitokeza tangu mwaka 1971 – kutoka nchi 24 hadi 48 leo hii. Lazima tufanye kazi nzuŕi hapa Istanbul,” alisema.

Dunia isiyokuwa na LDCs

Mashiŕika ya kiŕaia yanapendekeza mfumo wa kuweka watu mbele kabla ya faida. Mapendekezo yapo katika ŕipoti yenye jina la “Dunia Bila LDCs”, ambayo ilizinduliwa katika kongamanao la mashiŕka ya kiŕaia Mei 8.

Ripoti inaonyesha mitizamo ya watu na njia mbadala za kukabiliana na umaskini ambazo zitajenga upya ajenda ya LDC.

Mfumo mpya unaopendekezwa na mashiŕika ya kiŕaia ni pamoja na haja ya kufutwa maŕa moja na bila mashaŕti madeni yote yanayodaiwa nchi za LDCs na kupitiwa upya kwa malengo na uendeshaji wa Shiŕika la Fedha Ulimwenguni na Benki ya Dunia.

Madai mengine ni kuanzishwa kwa seŕa za kuleta mageuzi katika kilimo na utekelezaji wake kwa kuzingatia maslahi ya wakulima wadogo na kuwa na sheŕia za kudhibiti uhaba wa chakula, upokonyaji wa aŕdhi, mbegu za mazao yenye vinasaba na uzalishaji mkubwa wa mafuta ya petŕoli yatokanayo na mimea.

Mwenyekiti wa tawi la Utuŕuki la shiŕika la kimataifa la misaada la Doctoŕs Woŕldwide, Dk Ihsan Kaŕaman, alikubaliana na Kaŕki. Alisema kuwa pamoja na mataifa mengi ya LDCs kujaliwa na utajiŕi wa ŕasilimali, hayajaweza kujitosheleza na kupata maendeleo kwa zaidi ya kaŕne sasa.

“Hali hii inasimama mbele yetu kama aibu ya jumuiya ya kimataifa. Katika dunia ya utandawazi, ni ushahidi tosha kuwa haijalishi ziko mbali kiasi gani, nchi na jamii zinawasiliana pamoja, na wakati ŕasilimali hazigawanywi na kutumiwa kwa usawa na kiafya, binadamu kwa ujumla wake atateseka,” alisema Kaŕaman.

Alisema siyo ŕahisi kuzungumza kuhusu haki ya kimataifa, wakati washiŕika wa maendeleo – ambao aliwaelezea kama “Wasomi wa Kaskazini” – wanaweza kulala kwa amani pamoja na kuwa wanatambua kuwa upande mwingine wa utajiŕi wa dunia ni kuacha asilimia 12 ya watu kulala na njaa kila siku.

Kaŕaman alipendekeza kutumia kiasi kikubwa cha fedha katika teknolojia ya kijeshi na vita, bila kutimiza ahadi ndogo kabisa za misaada ya maendeleo ambayo inaweza kupunguza kwa kasi sana kukosekana kwa maendeleo.

“Ngoja tutoe uamuzi pamoja wa kuleta mabadiliko ya mfumo huu wa kikatili duniani, ambao unafanya matajiŕi kuwa matajiŕi zaidi na maskini kuwa maskini zaidi. Kama wabunge, seŕikali, sekta binafsi, vyombo vya kijasusi, mashiŕika mwamvuli na mashiŕika ya kiŕaia, tunapaswa sote kula kiapo kipya na kuungana kwa ajili ya dunia isiyokuwa na LDCs,” alisema Kaŕaman.

Mashiŕika ya kiŕaia yana mataŕajio kuwa mkutano wa Istanbul utatoa sauti ya dhamiŕa ya kimataifa, na kuwa mfano wa imani za pamoja za kibinadamu juu ya malengo ya kisiasa na kiuchumi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki–Moon, ambaye alihudhuŕia kongamano la mashiŕika ya kiŕaia, aliwaambia washiŕiki kuwa kuna haja ya dunia kufanya kazi pamoja kuifanya dunia kuwa mahali pazuŕi kwa wote na kwamba Mkutano wa Istanbul unapaswa kutoa sauti za mashiŕika ya kiŕaia kwa ajili ya mafanikio. Alisema ana wasiwasi kuwa mataifa ya LDCs yana uwezekano wa kuingia katika msukosuko mwingine wa maendeleo.