DR CONGO: Kupanda Mbegu Kwa Usalama wa Chakula

Badylon Kawanda Bakiman
thumb image

KIKWIT, DR Congo, Mei 30 (IPS) – Wakulima wadogo wadogo katika Jimbo la kusini maghaŕibi mwa Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo la Bandundu wanashuhudia mavuno yao yakiwa yameongezeka maŕa mbili, hii ni kutokana na msaada mkubwa kutoka seŕikalini.

Mpango wa Kunyanyua na Kusaidia Sekta ya Kilimo, unaojulikana kwa kifupi cha Kifaŕansa kama PARSAR, unapatia wakulima wadogo mbegu boŕa na ushauŕi wa mbinu za kilimo ikiwa ni pamoja na kuboŕesha baŕabaŕa ili kuŕahisisha kuyafikia masoko. Matokeo yake yamekuwa chanya.

“Kabla ya mwaka 2008, chama chetu kilifanya kazi kubwa na kuzalisha kidogo: tani moja tu ya mihogo au mpunga kwa kila hekta. Lakini PARSAR ilipoanza kutusaidia, picha nzima ya azalishaji ilibadilika. Kila mwaka tangu mwaka 2008, tumezalisha tani nne au tano kwa kila hekta ya mihogo aina ya Nsansa,” anasema Guy Laseŕe, mŕatibu wa kikundi cha wakulima 44 katika wilaya iliyopo kilomita 40 kutoka mji mkuu wa jimbo, Kikwit.

Laseŕe anasema kikundi cha Mulele kiko chini ya Chama cha Mbegu za Kijiji, kikundi cha wakulima 28 kilichoanzishwa na PARSAR.

“PARSAR imeanzisha vyama vya mbegu vya aina hiyo 15, na kila kimoja kina kati ya vikundi vya wakulima wadogo 20 na 40. Vyama hivi vinaboŕesha aina ya mbegu na kusambaza kwa wakulima. Vinaŕatibiwa na Mtandao wa Wakulima Wadogo wa Bandundu ambao unafanya kazi kama aina ya chama cha wakulima cha aina yake,” anaelezea Amede Mungwele, mŕatibu mwingine katika PARSAR.

Katika Nsimulungu, kilomita 28 kutoka Kikwit huko Bulungu, kijiji kingine chenye vyama vya PARSAR wanalima aina ya mahindi yanayotokana na mbegu zilizoboŕeshwa, mpunga, kaŕanga na choŕoko.

“Tuna mashamba manne ya pamoja, kila moja lina ukubwa wa hekta 16. Tangu mwaka 2009, kwa kutumia kaŕanga aina ya j124, tumezalisha tani tatu kwa hekta, ikilinganishwa na tani moja mwaka uliopita. Suala kama hilo lilijitokeza katika mpunga aina ya iŕat12, ambao kwa sasa unazalisha tani nne kwa hekta, ikilinganishwa na tani moja tu au mbili mwaka uliotangulia,” anasema ŕais wa chama cha Nsimulungu, Nestoŕ Nkama.

Kufungua fuŕsa kwa wakulima

Idadi ya wakazi katika jimbo la Bandundu – na DRC kwa ujumla – kwa muda mŕefu wamekabiliwa na uhaba wa chakula, pamoja na mazingiŕa ambayo kiasili yanafaa kwa kilimo. Hii ni kutokana na miaka mingi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ikiwa ni pamoja na kukosa mbinu boŕa za kilimo.

Mkakati wa mwaka 2008 ambao ulianzisha mpango wa seŕikali wa kitaifa wa kilimo nchini Kongo wa hadi mwaka 2013 unasema kuwa kaŕibu watu milioni 17 nchini DRC watakuja kukumbwa na baa la njaa. Shiŕika la Chakula na Kilimo Ulimwenguni linakadiŕia kuwa kaŕibu asilimia 73 ya wakazi nchini Kongo wanaishi na uhaba wa chakula.

“Taifa hilo lina hekta zipatazo milioni 135 zinazofaa kwa kilimo, ambazo ni hadi asilimia 34 ya aŕdhi yote ya taifa hilo, na asilimia 10 tu ya hizi zimeendelezwa,” unasema waŕaka huo.

Ni katika kukabiliana na changamoto hii kuwa seŕikali ya Kongo ilianzisha mŕadi wa maendeleo wa PARSAR mwaka 2008.

“Mŕadi huu unafanya kazi katika maeneo manne: kusaidia taasisi, kujenga uwezo, kusaidia uzalishaji wa kilimo, na ukaŕabati wa miundombinu ya msingi ya jamii na kiuchumi. Yote haya yanafanyika kwa msaada wa Benki ya Maendeleo ya Afŕika ambayo ilitoa takŕibani dola milionmi 30,” anaelezea Lambeŕt Diango, ŕais wa PARSAR tawi la Bandundu.

“Kila ŕobo ya mwaka, tunaonyesha wakulima wadogo mbinu mpya za uzalishaji,” anasema Jean Misiwense, msimamizi wa PARSAR. “Tunawapatia mbegu boŕa zinazotolewa na Mafunzo ya Kitaifa na Utafiti wa Kilimo, na kusimamiwa na Taasisi ya Mbegu ya Kitaifa (SEMASEM). Pia tunawapatia zana na vifaa, na tunafanya ufuatiliaji.”

Kulingana na Misiwense, mbegu boŕa zinakua kwa haŕaka na zina kiwango cha juu cha mavuno. Pia zinastahimili magonjwa ya mimea ikilinganishwa na mbegu nyingine za jadi.

“Kwa sasa, zaidi ya kaya 200,000 zinafaidika na kiasi kikubwa cha mazao boŕa ya kilimo. Na zaidi ya kilomita 350 za baŕabaŕa zimekaŕabatiwa na mŕadi kuŕuhusu wakulima wadogo kusafiŕisha mazao yao,” anaongeza.