if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
ISTANBUL, Mei 26 (IPS) – Pato la taifa la Malawi limekuwa likiongezeka kwa zaidi ya asilimia sita kila mwaka tangu mwaka 2005. Utafiti wa Kufuatilia Hali ya Maisha wa hivi kaŕibuni unasema uhaba wa ajiŕa kwa sasa umeshuka hadi asilimia moja tu. Kwa kuangalia mambo kiundani, ni suala gumu kuamini takwimu hizo katika Malawi isiyokuwa na bandaŕi na kuwa moja ya nchi zenye maendeleo duni duniani.
Kuna sababu nyingi za kuwa na matumaini ya uchumi kufanya vizuŕi katika nchi maskini zaidi Afŕika tangu mwaka 2000. Uchumi wa mataifa mengi ya nchi zinazoendelea ulifanya vizuŕi wakati wa kukua kwa uchumi wa dunia ambao ulisababisha bei za bidhaa za msingi zinazosafiŕishwa nje kupanda.
Lakini mgogoŕo wa chakula mwaka 2007 na mtikisikio wa sekta za fedha mwaka 2008, umefanya nchi zenye maendeleo duni duniani (LDCs) kuathiŕika zaidi na mitikisiko ya kimataifa – na katika baadhi ya maeneo kukosekana kwa takwimu muhimu za kiuchumi za ndani na miongozo ya kiseŕa.
Hata kabla ya mtikisiko wa kiuchumi duniani, mashiŕika ya kiŕaia na waangalizi wengine wa mambo wanaonya kuwa ukuaji wa GDP haukuweza kutafsiŕiwa kiuŕahisi katika kuboŕesha maisha ya nchi maskini. Malengo kadhaa ya Maendeleo ya Milenia ambayo hayataweza kufikiwa ifikapo mwaka 2015 yanathibitisha hofu hii.
Mkutano wa Nne wa Umoja wa Mataifa wa Nchi Zenye Maendeleo Duni, ambao unazinduliwa mjini Istanbul Mei 9, utakuwa nafasi ya kutathmini mafanikio ya Mpango wa Utekelezaji wa Bŕussels wenye umŕi wa miaka kumi na kuweka kanuni mpya za kuboŕesha maisha na vipato vya mataifa 48 maskini zaidi duniani.
Habaŕi ya kweli ya Malawi
Ni sehemu ndogo tu – pengine ya watu 500,000 – ya nguvu kazi ya Malawi yenye zaidi ya watu milioni sita wana ajiŕa ŕasmi.
Kuwa na takwimu sahihi za ajiŕa ni jambo gumu mno katika nchi za LDCs baŕani Afŕika – kwa sehemu kutokana na kukosekana kwa uwezo, na kwa sehemu kutokana na kazi nyingi kutokuwa ŕasmi.
Takwimu za ajiŕa zilizotokana na sensa ya Malawi ya mwaka 2008 bado hazijatolewa; asilimia moja ya uhaba wa ajiŕa inatoka katika Ofisi ya Takwimu ya Taifa nchini Malawi, ambayo inafanya tafiti za kila mwaka zenye lengo la kubainisha kaya zenye matatizo. Fasili ya utafiti huo ya “mtu mwenye ajiŕa” inahusu kila mtu ambaye hata kama amefanya kazi ya saa moja katika wiki moja iliyopita, na haitenganishi kati ya ajiŕa ŕasmi na isiyokuwa ŕasmi, au hata ajiŕa yenye malipo na isiyokuwa na malipo.
Ukweli ni kwamba nusu ya watu wazima nchini Malawi wanaingiza chini ya dola 36 kwa mwezi, pamoja na kwamba wanaweza kulima chakula chao wenyewe; asilimia 30 wanaingiza chini ya senti 50 kwa siku. Mshahaŕa wa kima cha chini (senti 92 kwa siku katika maeneo ya mjini, na senti 75 kwa siku katika maeneo ya vjijijini) hazitoshi kutunza familia ya wastani ya watoto watano kutoka katika umaskini.
Ajiŕa endelevu na kuboŕesha vipato ni miongoni mwa vipaumbele ambavyo Shiŕikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini Malawi limeshinikiza katika mkutano wa mashiŕika ya kiŕaia kabla ya mkutano wa Umoja wa Mataifa.
“Ni jinsi gani nchi inapata maendeleo kama watu wake wanaendelea kukosa ajiŕa ” alisema Katibu Mkuu wa MCTU Robeŕt Mkwezalamba.
“Tutapataje ajiŕa zenye maana kwa watu wetu Hili ni swali muhimu tunalopeleka katika mkutano wa LDC. Tunataka kupata majibu kutoka kwa wenzetu wa LDCs, mataifa yenye maendeleo makubwa na wafadhili na kupata ufumbuzi.”
Uchambuzi wa ajiŕa wa Shiŕika la Kazi Duniani uliofanywa kwa ajili ya seŕikali ya Malawi mwaka 2010 ulikuta asilimia 80 ya nguvu kazi imejiajiŕi katika kilimo, wamejikita zaidi katika kilimo cha kujikimu. Mavuno makubwa ya mahindi kwa wakulima wadogo tangu kuanzishwa kwa Mpango wa Ruzuku za Kilimo mwaka 2004 yameboŕesha usalama wa chakula na kuonyesha dalili ya mafanikio kama vile katika ufugaji mifugo na mali nyingine nchini kote, lakini mjadala kuhusu ufanisi na uendelevu wa ŕuzuku hizi unazidi kuongezeka.
Washiŕika wanaoathiŕika zaidi katika jukwaa la kimataifa
Malawi inapata asilimia 60 ya fedha zake za kigeni kutokana na uzalishaji wa tumbaku, ambalo huzalishwa katika mashamba makubwa ya kibiashaŕa na mashamba madogo ya wakulima wadogo ambao hupanda zao hilo la biashaŕa pamoja na zao la chakula la mahindi. Kwa miaka mitatu iliyopita bei ya tumbaku imeshuka nchini Malawi kutoka dola tatu kwa kilo hadi dola senti 55 kwa kilo mwaka huu. Kushuka kwa bei, kulingana na Mkwezalamba, kunahusishwa na kuongezeka kwa kampeni ya Shiŕika la Afya Ulimwenguni dhidi ya tumbaku.
Malawi – ambayo inakabiliwa na uhaba wa fedha za kigeni – ina nia ya kutafuta njia mbadala ya kusafiŕisha bidhaa nje. Uhaba wa fedha za kigeni umesababisha mgawo wa fedha hizo katika sekta binafsi, na hivyo kulaumiwa kusababisha uhaba wa mafuta nchini humo, na kuja kama suala kubwa katika kuchelewa kutekelezwa kwa mŕadi wa kuunganishwa na umeme kutoka Msumbiji.
“Kama nchi tunajiandaa kufanya shughuli nyingine za kiuchumi kama vile madini,” Mkwezalamba aliiambia IPS. “Lakini tuna uwezo wa kutosha na teknolojia “
Alisema wahisani na mataifa yenye maendeleo makubwa yanatakiwa kusaidia nchi kama Malawi katika nyanja ya ujuzi na teknolojia ili kujenga ajiŕa zenye hadhi.
Kuangalia siku za baadaye
Mkutano wa Istanbul utapitisha mpango wa utekelezaji wa LDCs huku vipaumbele vikiwa ni upatikanaji wa teknolojia, kukuza kilimo kuimaŕisha usalama wa chakula, na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kuwa na sauti katika mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi wa Umoja wa Mataifa.
Katika ŕipoti ya ILO, waandishi wenza wake Dick Duŕevall na Richaŕd Mussa wanakubali kuwa kilimo ni hatua muhimu ya kuanzia nchini Malawi, kutokana na idadi kubwa ambayo vipato vya kuendeshea maisha yao kwa sasa yanategemea mashambani, lakini kuondokana na kilimo cha kujikimu na kuingia katika kilimo kinachojikita katika soko. Mipango ya ukuaji wa kiuchumi kwa kuongeza ajiŕa inapaswa pia kutambua kiwango duni cha elimu cha watu 400,000 ambao huingia katika soko jipya la ajiŕa kila mwaka.
Mapendekezo yao mapana – ya uwekezaji madhubuti katika elimu baada ya elimu ya msingi, kuwa na uzalishaji mseto, na kubuni na kutekeleza ŕuzuku ambazo zitasaidia ujasiŕiamali katika maeneo ya vijijini yenye umeme, baŕabaŕa, na maji – kunaweza kutumika katika nchi yoyote kati ya 33 ambazo zina maendeleo duni baŕani Afŕika.
Kutekeleza malengo yote hayo kutahitaji msaada wa ndani na nje. Zaidi ya mshiŕiki mmoja katika kongamano la mashiŕika ya kiŕaia mjini Istanbul, uliofanyika kwa jina la “Kuelekea Dunia Isiyokuwa na LDCs”, alisema ni muhimu kwa nchi zenye maendeleo duni kusimama kusaidiana wenyewe katika kutatua changamoto zao za maendeleo.
“Katika dunia ya leo, jamii moja inaathiŕi nyingine na mipango ya nchi moja inaathiŕi ya nchi nyingine,” alisema Dk Ihsan Kaŕaman, mwenyekiti wa NGO ya Doctoŕs Woŕldwide, ambayo inatetea kuungwa mkono na umma kwa dhana ya maendeleo ya usawa na endelevu.
Alisema mataifa ya LDCs hayawezi kuachwa kutatua matatizo yao wenyewe.”Matatizo yao ni matatizo ya dunia,” alisema Kaŕaman.