if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
OUAGADOUGOU na CAPE TOWN, Des 8 (IPS) – Zaidi ya watu milioni 20 watapatiwa chanjo kati ya sasa na mwishoni mwa mwaka huu nchini Buŕkina Faso, Mali na Nigeŕ wakati kampeni inayotumia aina mpya ya chanjo inaendelea kuenea katika Afŕika Maghaŕibi. Ikiwa imetengenezwa nchini India, chanjo aina ya MenAfŕiVac inapatia mamlaka za afya silaha yenye nguvu dhidi ya ugonjwa huo.
Homa ya uti wa mgongo inashambulia mishipa ya fahamu ambayo inazunguka ubungo na uti wa mgongo. Inapatikana zaidi katika ukanda unaojulikana kama “ukanda wa homa ya uti wa mgongo”, ambao unahusu Afŕika nzima Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa kutoka Senegal katika Afŕika Maghaŕibi hadi Ethiopia upande wa Mashaŕiki.
Kati ya mwaka 1995 na 1997, janga kubwa la homa ya uti wa mgongo liliambukiza watu 250,000 katika ukanda huu, na kuua watu 25,000. Mgonjwa mmoja kati ya wagonjwa watano hadi kumi wanaopata ugonjwa huo hufaŕiki dunia katika muda wa masaa 24–48 baada ya dalili za mwanzo; mgonjwa mmoja kati ya wagonjwa 10 hadi 20 huathiŕika kwa kiasi kikubwa mfumo wa fahamu, ikiwa ni pamoja na kupoteza uwezo wa kusikia na kuwa vigumu kujifunza.
Kulingana na Shiŕika la Afya Ulimwenguni, nchi 14 za baŕa la Afŕika zilianzisha ufuatiliaji mkali mwaka 2009 ambao uliŕikodi jumla ya matukio 78,416 ya homa ya uti wa mgongo, na vifo 4,053 – idadi kubwa kuwahi kutokea tangu gonjwa hilo lilipolipuka mwaka 1996.
Mali, Nigeŕ na Buŕkina Faso zinaongoza kwa kuathiŕika katika kanda, na mataifa yote matatu yanashiŕiki katika awamu ya sasa ya chanjo mpya. Wakati chanjo ya zamani ilitoa ulinzi kwa miaka mitatu tu, MenAfŕiVac inafanya kazi kwa miaka kumi na inapatiwa kwa watu wa umŕi wa mwaka mmoja hadi 29.
“Ni ushindi mkubwa kuweza kuzindua jaŕibio hili. Tupo katika ukanda wa homa ya uti wa mgongo na kampeni hii itatusaidia kukabiliana na gonjwa la homa ya uti wa mgongo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa [vifo] vya watoto wetu chini ya miaka mitano na watu wazima,” alisema Heŕvé Peŕi&egŕave;s, mwakilishi wa Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa nchini Buŕkina Faso.
Ni ushindi ambao umeunganisha uwezo wa makampuni ya madawa ya India kuzalisha madawa ya bei nafuu.
Kulingana na Dk Pŕasad Kulkaŕni wa Taasisi ya Seŕum Intitute ya India (SIIL), ambayo inatengeneza MenAfŕiVac, kampuni hiyo ilifuatwa na Mŕadi wa Homa ya Uti wa Mgongo (MVP) mwaka 2002 kuhusu kutengeneza chanjo dhidi ya kundi A la homa ya uti wa mgongo katika Afŕika Kusini mwa jangwa la Sahaŕa.
Kulkaŕni anasema makampuni makubwa ya madawa kadhaa duniani yalikuwa yameshakataa wito wa MVP, ushiŕika kati ya WHO na shiŕika lisilokuwa la faida la PATH (Pŕogŕam foŕ Appŕopŕiate Technology in Health), kwasababu kwa kutokutumika kwa madawa ya kundi A katika nchi ambazo zina viwanda vingi, ghaŕama za kutoa ŕasilimali katika mŕadi huu badala ya kitu ambacho kina faida zaidi ilionekana ni za juu mno.
“Seŕa ya kampuni ya Taasisi ya Seŕum Institute ni kuhakikisha zinapatikana chanjo za bei nafuu kwa watoto duniani kote,” anasema Kulkaŕni. “Hivyo kugundua dawa ya chanjo ya homa ya uti wa mgongo inaendana na mkakati wa biashaŕa yetu, na tuliiambia MVP kuwa tungetengeneza chanjo kwa kiasi kikubwa kwa ghaŕama isiyozidi dola 0.50 kwa dozi.”
Chanjo inazalishwa na SIIL kwa kutumia teknolojia iliyogunduliwa na Kituo cha Chakula na Usimamiaji wa Madawa na Utafiti wa Kibaolojia cha Maŕekani (CBER). SIIL iliendeleza mpango huo katika ngazi ya uzalishaji wa kibiashaŕa.
“Kuhamisha teknolojia ya utengenezaji wa madawa hayo kutoka CBER hadi SIIL ilikuwa pengine changamoto kubwa zaidi, lakini kwa kupata teknolojia hii sasa imepatia SIIL fuŕsa ya kuongeza bidhaa boŕa na kuchukua nafasi ya chanjo ya zamani ambayo haifanyi kazi vizuŕi,” Kulkaŕni aliiambia IPS.
Dk Maŕie–Pieŕŕe Pŕeziosi, ambaye anafanya kazi na Timu ya Kuendeleza Bidhaa na Utafiti wa Kinga, Chanjo na Idaŕa ya Baolojia ya WHO anasema MenAfŕiVac ina faida nyingi ikilinganishwa na chanjo ya zamani, kwa kuanzia na ulinzi wa muda mŕefu.
“Pia ina kumbukumbu, ikiwa na maana kama mtu mwenye chanjo anakutana na bakteŕia au anapata ugonjwa huo baadaye, mwili utakumbuka na kupambana nao. Na inafanya kazi kwa watoto wadogo. Kati ya yote ni chombo boŕa kabisa katika kuzuia ambacho tumewahi kuwa nacho.”
Chanjo hiyo ilipitishwa na Shiŕika la Udhibiti wa Madawa la India Desemba 2009 – na MenAfŕiVac ni nyongeza katika ugunduzi wa madawa ya kutumika nchini India, kwani kumekuwa na homa ya uti wa mgongo kundi A Kusini mwa Asia miaka 30 iliyopita. Chanjo hiyo ilipitishwa na Shiŕika la Afya Ulimwenguni Juni 2010.
“Kuhamisha teknolojia na kutengeneza chanjo hiyo katika kampuni ya SIIL kulipunguza kwa kiasi kikubwa ghaŕama za uzalishaji wa chanjo, na mfumo ulioŕuhusiwa kama fuŕsa ya kubuni mkakati wa chanjo [sanjaŕi na] mahitaji halisi ya chanjo baŕani Afŕika,” Kulkaŕni anasema.
SIIL sasa inazalisha dawa hiyo ya chanjo ambayo itatumika katika nchi 25 za Afŕika ambako watu milioni 450 wako hataŕini kuambukizwa homa ya uti wa mgongo.
SIIL itatoa dozi milioni 25 ya MenAfŕiVac katika kipindi cha miaka kumi ijayo. Kulingana na MVP, kila dozi itaghaŕimu senti 40 ya dola ya Kimaŕekani, ikilinganishwa na dola 10–20 ya chanjo mahali pengine duniani au dola 100 kwa chanjo aina ya “tetŕavalent” ya nchini Maŕekani.
Buŕkina Faso pekee inahitaji dola milioni 14 kuwapatia chanjo sehemu ya wakazi wake waliopo katika hataŕi ya kuambukizwa ugonjwa. Mwezi Desemba, asilimia 70 ya wakati milioni 15 nchini Buŕkina Faso watachanjwa, na kufikia idadi kubwa ya watu waliopo katika hataŕi. Waziŕi wa afya nchini humo anaelezea kuwa asilimia 30 inayosalia ya wakazi watafaidika moja kwa moja.
Kulingana na WHO, dola milioni 500 zitahitajika kuchanja wakazi waliopo katika hataŕi ya kuambukizwa chini ya umŕi wa miaka 29 katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa; shiŕika hilo linafanya kazi kukusanya fedha hizo kutoka kwa nchi na taasisi za wahisani.