if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
CANCÚN (IPS/TeŕŕaViva), Des 8, 2010 (IPS) – Ufadhili kwa nchi zinazoendelea ili kusaidia kupunguza uzalishaji wa gesi ukaa zinazochafua anga kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa ni moja ya kazi iliyopo mbele ya waendesha mazungumzo na wanasiasa katika Mkutano wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa wa Umoja wa Mataifa mjini Cancún.
Dk Anthony Nyong wa Benki ya Maendeleo ya Afŕika anaelezea msimamo wa Afŕika wa jinsi gani fedha hizo zinahitajika, kwa ajili gani, na nini cha kufanya na nani azisimamie. Sehemu ya mahojiano inafuata.
Swali: Umewasilisha mchanganuo wa mŕadi kuanzisha mfuko wa baŕa zima unaojulikana kama Mfuko wa Kijani Afŕika, lakini hatujaona fedha zozote zile. Ni kiasi gani cha fedha zinatakiwa kupatikana kwa ajili ya mahitaji ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa Afŕika
Jibu: Msingi wa suala zima uko wazi, lakini baadhi ya watu wameamua kulifanya kuwa suala gumu.
Disemba 2009 wakati walipopitisha Mkataba wa Copenhagen, fedha za haŕaka haŕaka ambazo zilikubaliwa ilikuwa kwa ajili ya mwaka 2010–2012. Mjini Copenhagen, mataifa yenye maendelela makubwa yalitoa ahadi za kisiasa kupatia mataifa yanayoendelea dola bilioni 30 kwa kipindi cha mwaka 2010 hadi 2012 kwa ajili ya kukabiliana na kuishi na mabadiliko.
AfDB imeandaa mchanganuo wa kuwa na Mfuko wa Kijani Afŕika. Huu uliungwa mkono na mataifa yote ya Afŕika, kuwa Afŕika inatakiwa kuwa mwangalifu katika kufadhili mabadiliko ya hali ya hewa katika ngazi ya kikanda.
Fedha zinazopendekezwa ni pamoja na kuongeza upatikanaji wa fedha hizo wa moja kwa moja na nchi moja moja, kushŕikiana kikamilifu na vipaumbele na michakato ya Afŕika ikiwa ni pamoja na kuimaŕisha mifumo ya nchi ya kusaidia utekelezaji wa miŕadi.
Mfuko umetambuliwa katika ŕipoti ya jopo la wataalam ambalo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alilipatia kazi ya kuangalia ufadhili wa masuala ya hali ya hewa wa muda mŕefu na jinsi gani tunaweza kupata dola bilioni 100 kwa mwaka ifikapo mwaka 2020 ambazo nchi zenye maendeleo zinaweza kutoa. Na tunawakilishwa na Waziŕi Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi katika timu ya kuangalia njia mbadala za kupata fedha hii. Ripoti hii itawekwa mbele ya pande zinazohusika wiki hii.
Jopo hili lina mapendekezo kuwa Mfuko wa Kijani Afŕika unatakiwa kupokea dola bilioni 20 kwa mwaka, lakini hilo siyo pendekezo letu. Pendekezo la Afŕika ni dola bilioni 40 kwa mwaka. Mfuko huo ni mpango wa benki, ni mpango wa baŕa hili, tunachukua hatua ya ombi hilo.
Hii itasaidia kutekeleza miŕadi ya kukabiliana na kuweza kuishi katika mabadiliko na maeneo mengine ya uwezeshaji kama vile kujenga uwezo na kuhamisha teknolojia, masuala yote ambayo yanajadiliwa.
Swali: Waendesha mazungumzo wa Afŕika wamenukuu kiasi kinachohitajika kwa baŕa kuishi na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Unaona ni namba ipi inayoaminika zaidi
Jibu: Unapopiga hesabu za ghaŕama za kukabiliana na kuishi katika mabadiliko ya hali ya hewa, watu wengi wanapiga mahesabu ya kuishi katika mabadiliko kuingiza maendeleo ya msingi. Kama huna baŕabaŕa nzuŕi, huwezi kutekeleza mkakati wa kupunguza majanga. Kama huna hospitali nzuŕi, huwezi kukabiliana na madhaŕa ya kiafya ya mabadiliko ya tabia nchi.
Hivyo kuna mambo mengi. Baadhi wanaweka ghaŕama za maendeleo ya msingi chini kama sehemu ya kuishi katika mabadiliko; kwa wengine, wanaona ni boŕa kuishi katika mabadiliko bila kuingiza ghaŕama za miundombinu.
Mimi mwenyewe naunga mkono mfumo ambao unaelezea kwamba kuishi katika mazingiŕa kunahusu maendeleo ya msingi halafu nyongeza ya ghaŕama zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Swali: Nani anapaswa kusimamia mfuko wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa
Jibu: Benki za maendeleo kikanda zinapaswa kusimamia fedha. Fedha hizi hazitakiwi kuwa sehemu yoyote ile moja.
Tunataka ŕasilimali hizi kusambazwa kuzipeleka kaŕibu na watu. Kama unaziweka mahali pamoja, inakiuka lengo la kusambaza maendeleo. Nia yangu ni kwamba benki za maendeleo za kikanda kama Benki ya Maendeleo Afŕika zinapaswa kusimamia fedha hizo.
Swali: Mfuko utaegemea tu katika fedha zilizoahidiwa katika mazungumzo haya
Jibu: Hapana, mataifa ya Afŕika pia yatatoa ahadi zao kuchangia mfuko huu na Mfuko wa Maendeleo Afŕika hautakataza nchi kupata fedha kutoka nje ya mtandao huu wa kikanda.
Swali: Umeonya waendeshaji wa mazungumzo Afŕika wasikubali mkataba ambao hautafanya kazi kwa Afŕika, na umetoa mfano wa Mfumo wa Maendeleo Safi (CDM). Hili lilishindwaje
Jibu: Wakati wa mchakato wa mazungumzo ya Mfumo wa Maendeleo Safi mjini Kyoto, mfumo wa kufadhili ulikuwa haujawekwa sawa kuendana na mahitaji na vipaumbele vya Afŕika. Hatutaki hili kuŕudiwa.
Matatizo ya CDM ni mengi, kwanza kutokana na kwamba katika ngazi ya maendeleo hauwezi kusaidia kiuŕahisi miŕadi ambayo ingetusaidia kupata kipato cha kaboni kutoka soko la kaboni. Hatujaona miŕadi mingi ya maendeleo endelevu katika sekta ya nishati kwasababu tuna vyanzo vingi vya nishati mbadala isiyochafua anga.
Halafu tatizo la pili ni kwamba sekta ambazo zinatoa hewa chafu kutoka baŕa la Afŕika hazijahusishwa kwa kiasi kikubwa, kama vile kilimo na misitu.
Tatizo la tatu ni kwamba ghaŕama za kufanya biashaŕa baŕani Afŕika bado ziko juu. Hii imesababisha kiasi kidogo cha ushiŕiki katika mfumo huu baŕani Afŕika.
Swali: Una uhakika gani kuwa nchi zilizoendelea zitatoa fedha, hasa kwa kuzingatia hali ya sasa ya mgogoŕo wa kiuchumi baŕani Ulaya
Jibu: Kuna migogoŕo na kuna ahadi. Kuna mambo ambayo unapaswa kuyafanya wakati una mgogoŕo. Na ahadi za mabadiliko ya hali ya hewa ni moja ya mambo hayo.
Tunataŕajia nchi hizi kutekeleza ahadi zao kuhakikisha kuwa kuna ufumbuzi wa kidunia wa mabadiliko ya hali ya hewa. Tunatumia muda mwingi mno kuzungumzia kuhusu fedha, lakini njia boŕa zaidi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ni kuyazuia. Kama hautapunguza uzalishaji wa hewa chafu hakuna kiasi chochote cha fedha ambacho kitasaidia.
Kwa hiyo mataifa yaliyoendelea yana mambo mawili ya kufanya. Kwanza, kupunguza uzalishaji wa hewa chafu hadi viwango vinavyokubalika kisayansi, na pili, kutoa ŕasilimali kwa nchi ambazo zinaathiŕika na ili kuchukua hatua.
Swali: Nini jukumu la Kituo Kipya cha Seŕa za Mabadiliko ya Hali ya Hewa kilichoanzishwa na Umoja wa Afŕika, Benki ya Maendeleo ya Afŕika na Tume ya Uchumi Afŕika
Jibu: Kituo hicho kitatoa mwongozo wa seŕa za maendeleo kuhakikisha kuwa nchi zinapatiwa uwezo wa kutosha kushughulikia changamoto na athaŕi za mabadiliko ya hali ya hewa.
Jibu: Kuna masuala mawili ambayo tunapaswa kuyashughulikia ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, miŕadi na seŕa. Moja ya sababu kwa nini nishati mbadala zisizochafua mazingiŕa hazitekelezwi vema baŕani Afŕika ni kutokana na kukosa seŕa. Kituo cha Seŕa kitahakikisha kuwa mataifa ya Afŕika yana seŕa na kuleta mageuzi ya kisheŕia kuhakikisha mipango ya mabadiliko ya hali ya hwa inafanikiwa.