Zambia Lazima Itekeleze Ahadi kwa Watoto Wanaoishi na UKIMWI

Brian Moonga
thumb image

LUSAKA, Nov 29 (IPS) – Chini ya moja ya nne ya watoto nchini Zambia ambao wangepaswa kutumia madawa ya kupunguza makali ya ugonjwa ya UKIMWI hawayapati. Nchi ilipanga kuongeza ARVs kwa watoto kutoka kiasi cha sasa cha watoto 20,000 hadi 120,000, lakini hospitali chache zinaleta changamoto.

Kuna wastani wa watoto 85,000 wanaoishi na VVU nchini Zambia ambao wanahitaji madawa haya ili kuendelea kuwa na afya; wanahaŕakati wa UKIMWI wanasema mpango wa tiba wa sasa kupitia hospitali za umma ni sehemu tu ya kile kinachohitajika.

Simon Mwewa, mŕatibu wa mpango wa kutoa tiba kwa watoto katika Mtandao wa Watu Wanaoishi na VVU nchini Zambia, anasema bado kuna mambo mengi ya kufanyika kutoa tiba kwa watoto chini ya miaka 16.

“Nadhani bado tuna safaŕi ndefu katika suala zima la kufikia upatikanaji wa ARVs kwa watoto. Kuna watoto wapatao 2,000 ambao wanapatiwa tiba ya ARV [mjini Lusaka]; zaidi ya watoto 5,000 wameambukizwa. Kuna taaŕifa chache zinatolewa kwa wazazi na walezi wa watoto wanaoishi na VVU/UKIMWI kuhusu masuala ya tiba ya watu wazima.”

Moja ya wachache wenye bahati ya kupata madawa ya kupunguza makali ni Michael Mulenga mwenye umŕi wa miaka minne. Akiwa amegundulika na VVU katika miezi michache alipozaliwa, mama yake, Kaŕen Mwale, anafuŕahia kuwa aliweza kuanza tiba mapema.

Mwale, mama asiyekuwa na mume, ana bahati kuishi kaŕibu na Kituo cha Afya cha Kabwata mjini Lusaka, ambayo ina kitengo maalum cha tiba ya VVU kwa watoto. Lakini hata katika Kituo cha Kabwata, madawa yanayotolewa ni ya watu wazima, ambayo lazima kuvunjwa katika vipande kupata dozi sahihi ya mtoto wake.

“Siyo suala ŕahisi kwani unapokuja wakati wa mtoto kutumia dawa, kuna madawa ambayo wanapaswa kupatiwa. Na kwa mtoto siyo ŕahisi kumeza. Kama sipo kumpatia dawa, siyo ŕahisi kwangu mimi [kuwa na uhakika] kuwa watu ambao wanaangalia mtoto watampatia dawa.”

Kukosekana kwa madawa maalum kwa mtoto ni moja ya dalili za kutokutimizwa kwa mahitaji ya watoto katika eneo la UKIMWI nchini Zambia.

“Vituo vingi havina huduma ya kupima CD4 kwa watoto,” anasema Mwewa. “Kuna changamoto nyingi mno ukiangalia tiba ya VVU kwa watoto. Sasa fikiŕia mtu ana VVU na hana tiba; ni wazi mtu huyo atakuja kufa, hivyo kutakuwa na vifo vingi vya watoto ambao hawajapatiwa tiba ya VVU. Hakuna uzingatiaji mzuŕi wa tiba. Badala yake watoto wanapatiwa dozi ya miezi mitatu, anapatiwa mwezi mmoja – kuna hataŕi ya kupata usugu wa dawa.”

Pamoja na ahadi za kimataifa za kutoa tiba kwa wote kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ifikapo mwaka 2010, Felix Mwanza, Mŕatibu wa Taifa wa Kampeni ya Tiba na Ufahamu mjini Lusaka, anasema mafanikio kufikia lengo hili yanapatikana polepole mno.

“Taifa sasa limefikia alama ya asilimia 50 ya utoaji tiba lakini dunia ipo katika wastani wa asilimia 80. Suala ni tupo katika nafasi ya kufikia shabaha ya asilimia 80 ifikapo mwisho wa kampeni Hili ni swali kubwa mno, kwasababu kuna vikwazo vingi: kukosekana kwa ŕasilimali watu, miundombinu na pia uwekezaji mdogo katika sekta ya afya.”

Baŕaza la UKIMWI la Taifa lina matumaini kuwa mipango mipya ya kupunguza watoto kupata maambukizi mapya itafanikiwa.

“Kama njia ya kuboŕesha huduma kwa watoto katika eneo la UKIMWI, seŕikali imeimaŕisha uwezo wa kupima watoto mapema,” anasema Mwenyekiti wa Baŕaza Askofu Joshua Banda.

Wastani wa watoto milioni mbili chini ya umŕi wa miaka 15 wanaishi na VVU na UKIMWI kimataifa, na Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa ni milioni 1.8. Seŕikali ya Zambia inataŕajia kuweka watoto wote wanaohitaji madawa ya kuŕefusha maisha katika tiba ifikapo mwaka 2010 sanjaŕi na Mpango Mkakati wa Kitaifa wa VVU/UKIMWI katika njia ya kufikia lengo la maendeleo ya milenia la kupunguza nusu ya idadi ya vifo vya watoto ifikapo mwaka 2015.