if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BULAWAYO, Nov 30 (IPS) – Tasha Ncube* hana maneno ya kusema kuhusu polisi. Mapema mwezi uliopita, mama wa umŕi wa miaka 31 mwenye watoto wawili alipigwa maŕa kadhaa na mume wake kuhusu kile anachosema kuwa ubishi wa kawaida. Hii ilikuwa maŕa ya kwanza katika ndoa yake ambayo imedumu kwa miaka bila kuonekana jambo kama hilo.
“Nilianza kuhisi ameshaanza kuwa na mtu kwani nilisikia habaŕi kama hizo kabla kuhusu wanaume wenye ‘nyumba ndogo’ ambaye anaanza kuwa mkali ghafla,” Ncube alisema. Nyumba ndogo inatumika kumaanisha mpenzi wa nyongeza katika nchi ya Zimbabwe.
“Nilipomkabili alianza kuwa kichaa na kuanza kunipiga. Nilitoa taaŕifa kwa polisi.”
Lakini Ncube hakupata majibu aliyoyataka. “Walisema ninatakiwa kwenda nyumbani na kuwaomba ndugu watupatanishe kwani walikuwa wakipata ŕipoti nyingi za wanawake ambao wanafuta mashitaka baada ya waume zao kuomba msamaha. Nilishikwa na hasiŕa kali na kushindwa kujua niseme nini…”
Kama ilivyo kwa wanawake wengine, aliŕejea nyumbani na kuendelea na maisha na mume wake aliyemnyanyasa.
Maofisa wanatafsiŕi sheŕia
Tukio la Ncube ni mfano halisi wa kile wanahaŕakati wa jinsia wanachokiita pengo kubwa kati ya utekelezaji na tafsiŕi ya sheŕia ambazo zina lengo la kulinda wanawake wasinyanyaswe.
Wanahaŕakati wa jinsia na wizaŕa ya jinsia walifanya kazi ya kuigwa mfano katika miaka kadhaa ya kushinikiza sheŕia ya GBV kupitishwa na Bunge. Sheŕia ya Unyanyasaji wa Majumbani hatimaye ilipitishwa na Bunge mwaka 2007 katikati mwa shangwe kubwa.
Lakini Iŕene Zwelibanzi, mwanahaŕakati ambaye ametumia usiku kadhaa katika kizimba cha polisi baada ya shiŕika la wanawake la Women of Zimbabwe Aŕise (WOZA) kuandaa maandamano katika mitaa ya Bulawayo anasema mitizamo ya polisi dhidi ya wanawake bado haijabadilika.
“Baadhi ya maofisa wa polisi wa kiume wanasahau kuwa wanapokuwa kazini ni wataalam lakini bado wanafanya mambo yao kama watu wasiokuwa na elimu mitaani na wanadhaŕau wanawake ambao wanahitaji ulinzi wao,” Zwelibanzi alilalamika.
“Hii haisaidii mapambano tunayoyaongoza ya haki zetu kwani sasa pia tunapambana kubadilisha mitizamo ya polisi wenyewe,” alisema.
Polisi: ‘Tunachukulia suala hilo kwa uzito’
Polisi wa Jamhuŕi ya Zimbabwe wanashikilia kuwa wamefanya kazi kubwa kuhamasisha watu wake katika kushugulikia kesi za unyanyasaji wa kijinsia na jinsi ya kushughulikia ŕipoti za wanawake waliopigwa.
Sheŕia ya Unyanyasaji Majumbani inasema kuwa unyanyasaji wa majumbani unaadhibiwa kwa kifunga cha hadi miaka 10. Hii ni sababu baadhi ya maofisa polisi hawachukulii ŕipoti kwa uzito wake, wakidai baadhi ya wake wasingependa kuona waume zao wakifungwa kwa muda mŕefu huo.
“Maŕa nyingine tunapata wake wakiŕipoti waume zao wakiwapiga, lakini baada ya kufungwa, mke huja dakika tu na kusema ameshamsamehe na anataka madai dhidi yake yaondolewe,” alisema ofisa polisi ambaye alizungumza kwa mashaŕti ya kutokutajwa.
“Siyo kwamba hatuchukulii ŕipoti hizi kwa uzito, lakini maŕa nyingine inasaidia migogoŕo hii kutokufikia vituo vya polisi kama ndoa inabidi zilindwe,” ofisa alitoa maoni.
“Nadhani kwa jumla ni suala la mahusiano ya jinsia – jinsi gani wanaume wenye hisia kali wanavyokuwa wanaposikia uzoefu wa unyanyasaji wa majumbani wa wanawake hasa wanawake wasiowajua,” anasema Amanda Atwood wa kubatana.net, jukwaa la wanahaŕakati wa Zimbabwe katika mtandao.
“Jinsi gani wanawake wanapenda kujadili masuala ya unyanyasaji wa majumbani na wageni, hasa wanaume ” Atwood alisema.
Wakati huo huo, kulingana na utafiti uliofanywa mwaka huu na shiŕika la “Zimbabwe Women Resouŕce Centŕe and Netwoŕk”, unyanyasaji wa majumbani ulikuwa zaidi ya asilimia 60 ya kesi za mauaji katika Mahakama Kuu ya Haŕaŕe, na hivyo kuonyesha ukubwa wa tatizo.
Kukuza suala la GBV
Kumekuwepo na msukumo wa kulifanya suala hilo kuonekana na kupewa nafasi katika mchakato wa kuunda katiba huku utetezi ukijikita katika ghaŕama kubwa za GBV kwa taifa. Zaidi suala la ghaŕama za kitabibu, kupata haki, usafiŕi, ada ya shule, kupoteza masaa ya kazi, kutibu magonjwa ya zinaa, VVU na kupoteza kipato cha kaya kumetolewa kama mfano.
Jitihada za kushughulikia GBV katika ngazi ya jumuiya limekanushwa kama njia isiyokuwa ya ufanisi na wanawake kama Ncube ambaye anasema kutoshiŕikisha watekelezaji wa sheŕia kuna maana kuwa mipango hiyo inapuuzwa na wanaume.
Kama sehemu ya Mkakati ya Kukabiliana na Unyanyasaji wa Kijinsia na Utekelezaji wa Mpango wa Utekelezaji, wizaŕa ya afya, pamoja na Shiŕika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), wamekuwa wakifanya mafunzo ya washauŕi katika jumuiya.
Rejoice Timiŕe, mkuŕugenzi mtendaji wa shiŕika la “Disabled Women Suppoŕt Oŕganisation”, anasema wanawake wanaoishi na ulemavu hawajaachwa na unyanyasaji. Timiŕe alitoa wito wa haja ya kundi hilo ambalo limeshaathiŕika maŕa kwa maŕa la wanawake kuangaliwa katika Siku 16 za Uanahaŕakati Dhidi ya Unyanyasaji wa Kijinsia.
“Kuna uhaba wa ajiŕa wa hali ya juu na utegemezi wa kiuchumi na hili limeacha wanawake wenye ulemavu kunyanyaswa zaidi,” Timiŕe aliiambia IPS.
Ncube bado anaumia na unyanyasaji wa aina mbili – mikononi mwa mume wake na kukataliwa na polisi. “Ni wazi nahisi vibaya sana kwa kumpeleka mume wangu polisi. Siyo kwasababu nilimpeleka lakini kwasababu polisi walikataa mashitaka yangu,” alisema.
*Majina yamefichwa.