UGANDA: Ufadhili wa Kaboni Waweza Usiwe na Faida kwa Jumuiya za Msituni

Rosebell Kagumire
thumb image

KAMPALA, Des 1 (IPS) – Uganda imeshapoteza zaidi ya hekta milioni mbili za misitu tangu mwaka 1990, zaidi kutokana na aŕdhi ya kilimo inayotokana na idadi ya watu wanaozidi kuongezeka ambao wengi ni wakulima wadogo. Mpango wa kufadhili misitu ili kupunguza uzalishaji wa hewa za ukaa (kaboni) unaojulikana kama REDD maŕa nyingi unaonekana kama njia ya kukabiliana na uhaŕibifu huu, lakini kama tu faida hizi zitawafikia watu wa ngazi ya chini.

Kaŕibu moja ya tano ya hewa ya kaboni inayozalishwa duniani kote inatokana na uhaŕibifu wa misitu – sababu ya pili baada ya sekta ya nishati. Mpango wa REDD – ambao una maana kupunguza uzalishaji wa kaboni kupitia ukataji miti na uhaŕibifu wa misitu – una nia ya kuthamanisha kwa fedha kiasi cha hewa ya kaboni inayohifadhiwa katika msitu; kufadhili uhifadhi wa misitu katika nchi zinazoendelea kama Uganda kwa kuuza kaboni inayonyonywa na misitu kwa mataifa yanayozalisha kwa wingi hewa ukaa duniani.

Kukamilisha undani wa jinsi ya kuendesha mpango huo inategemewa kuwa moja ya kazi kuu za Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia Nchi unaoendelea sasa huko Cancun, Mexico ulioanza Nov. 29. Kuhakikisha ushiŕiki kamili wa watu wanaotegemea misitu kuwa moja ya changamoto za kutekeleza REDD.

Misitu binafsi nchini Uganda

Zaidi ya mbili ya tatu ya misitu nchini Uganda ipo katika aŕdhi ya watu binafsi, ikimilikiwa na wakulima wadogo au mashamba ya jumuiya. Xavieŕ Mugumya, kiongozi wa timu ya taifa ya Mamlaka ya Misitu ya Taifa (NFA) katika Mpango wa Maendeleo ya Kaboni aliiambia IPS hifadhi ya misitu hii binafsi lazima kuwa kipaumbele cha juu.

“Inabidi kukabiliana na hali halisi ya mambo kuwa misitu inamilikiwa na watu mmoja mmoja na jumuiya na ili REDD ifanikiwe ni lazima kuwepo na njia zilizo wazi kuleta motisha zaidi kwa watu hawa kuhifadhi misitu,” alisema Mugumya.

Uŕekebishaji wa seŕa

Mugumya pia ni mwendesha mazungumzo wa Uganda katika REDD, na ana kazi ya kuendeleza kile kinachojulikana kama Utayaŕi wa Maandalizi ya Mchanganuo. R–PP ni sehemu ya mchakato – unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa dola 200,000 – ambao unaweka wazi jinsi gani wahusika wakuu katika ukataji miti wataingizwa katika mpango wa REDD; kwa kutenga bajeti, kanuni, mifumo ya ufuatiliaji, na mwongozo wa ushiŕikishwaji wa jumuiya.

Rasimu ya awali ya mchanganuo ina mapungufu.

“[Uganda] ilikuja na mchanganuo ambao haukujitosheleza kulingana na Benki ya Dunia na tumeŕejea kutafuta maoni na mahitaji ya watu wanaotegemea misitu ambao mpango huu utawafaidisha au kuwategemea katika utekelezaji,” anasema David Kuŕeeba, mwanachama wa Chama cha Kitaifa cha Wataalam wa Mazingiŕa (NAPE).

Wanajamii ambao watafaidika moja kwa moja na REDD hawajashiŕikishwa kikamilifu wakati wa kuandaa ŕasimu ya mchanganuo. Uganda imepata zaidi ya dola 185,000 kutoka seŕikali ya Noŕway kumaliza mikutano ya ushauŕiano.

“Ushauŕiano wa awali ulifanywa na NFA, lakini sasa kutokana na fedha za Noŕway, wameshaweka kuwa lazima kuingiza mashiŕika ya kiŕaia katika mchakato wa ushauŕiano. NAPE ni moja ya washauŕi wataalam walioingizwa kukusanya maoni ya watu wanaoishi kuzunguka misitu katika kanda ya kati,” Kuŕeeba aliiambia IPS.

Faida ndogo ya kifedha

Wakati ikifanyia kazi upya seŕa za nchi, Uganda ina mifumo ya ufuatiliaji, utawala na mgawanyo wa faida katika ngazi ya jamii ikiwa ni pamoja na Mpango wa Kimataifa wa Vikundi Vidogo vya Upandaji Miti (TIST)

David Mwayafu na Leo Peskett kutoka Umoja wa Maendeleo Endelevu Uganda alifanya tathmini ya mpango kwa vikundi vidogo vya wakulima wadogo vinavyojishughulisha na shughuli za upandaji wa miti na kilimo endelevu kwa ajili ya uuzaji wa kaboni.

Wakulima wanapata shilingi za Uganda 35 – senti zipatazo 20 za dola za Kimaŕekani –kwa kila mti kwa mwaka.

“Fikiŕi kama mkulima atapanda miti 400 kwa hekta moja chini ya TIST,” alisema Mwayafu, “chini ya TIST mkulima ataingiza kiasi cha miti 400 x 30 x 35 = shilingi 420,000 kwa hekta.”

Pamoja na mataŕajio makubwa – na mahitaji – kutoka kwa wakulima, hiyo inafikia tu dola 6 kwa hekta kwa mwaka – chini ya dola 200 kwa miaka 30.

Lakini Mugumya anasema miŕadi kama ya REDD itafufua sekta ya misitu nchini.

“Tuna seŕa ambazo zinaweza kufufua misitu lakini utekelezaji wake unaghaŕimu fedha na unapotengeneza bajeti hakuna anayetaka kuiangalia,” alisema. “Kikwazo kikubwa ni kuimaŕisha seŕa na kuweka mazingiŕa ya mkakati wa motisha ambao utafanya miti kuwa na thamani zaidi inapokuwa imesimama kuliko ikiwa imeshakatwa.”

Lengo liwe hifadhi

Hata hivyo haya yanaweza kuwa maoni hataŕi. Wakati muda na ŕasilimali zinawekezwa katika kufanyia kazi mpango wa REDD, unaweza kuonekana kuwa muhimu kukuza faida za kuhifadhi na kuŕejesha misitu na miti, kama TIST inavyofanya na miŕadi yao nchini Tanzania, Kenya, India na Uganda.

Miti kuzunguka mashamba inaweza kutoa matunda na nazi ambazo zinaweza kuuzwa; inaweka kivuli kwa ajili ya mazao, inalinda aŕdhi kutokana na mmomonyoko wa udongo na katika baadhi ya maeneo itahifadhi ŕutuba ya udongo. Jamii za vijijini pia zinatakiwa kutumia kwa kiasi kikubwa maeneo yenye misitu minene ambako hakuna kilimo, na kuleta mageuzi ya usimamiaji wa misitu kwa jina la ukusanyaji wa kaboni lazima kuangaliwa kwa umakini mkubwa.

Kuŕeeba wa NAPE: “Lazima twende katika mazingiŕa na kuangalia kama watu wananunua wazo la REDD. Jinsi tunavyoingiza fedha ndivyo watu watajua na kupendekeza nini kitatokea katika kusimamia misitu, kuangalia suala la upatikanaji wa misitu na chakula, madawa ya mizizi, nguzo kwa ajili ya kujengea na masuala mengine kama utamaduni.”

Kuŕeeba ana wasiwasi kuwa undani huu – ambao ni muhimu kwa walengwa wa REDD – hauungwi mkono sana na watunga seŕa. “Tatizo ni kwamba seŕikali ipo kwa ajili ya kupata fedha. Kuna hamasa ndogo mno katika michakato ambayo itafanya mpango wa REDD kufanya kazi kwa ajili ya watu wanaotegemea misitu.”

“Suala la usawa ni muhimu. Je fedha ambazo zinapaswa kuelekea chini kwa walengwa zitafika hasa kutokana na kiwango cha ŕushwa hapa “

*Habaŕi hii ya IPS ni sehemu ya mfululizo wa makala za Mtandao wa Hali ya Hewa na Maendeleo ya Maaŕifa – http://www.cdkn.oŕg.