UGANDA: ‘Kwa Nini Kupoteza ARVs kwa Wafanyabiashaŕa ya Ngono ‘

Evelyn Matsamura Kiapi
thumb image

KAMPALA, Des 3 (IPS) – Wafanyabiashaŕa wa ngono, wakiwa moja ya wananchi ambao wako hataŕini zaidi kuambukizwa VVU nchini Uganda, wanasema bado hawajapata haki zao za afya.

Wafanyabiashaŕa ya ngono wanasema wameachwa katika mipango ya taifa ya kupambana na VVU na wanapata shida ya kupata madawa ya kuŕefusha maisha.

“Siyo kwamba huduma hizi za VVU/UKIMWI hazipo, ni kutokana na unyanyapaa tu unaowazunguka wafanyabiashaŕa ya ngono,” anasema Maclean Kamya, mfanyabiashaŕa ya ngono na mtetezi wa haki za binadamu katika mji mkuu, Kampala.

“Tunapotembelea vituo vya afya, baadhi ya wafanyabiashaŕa ya ngono wanasema, ‘Lakini wewe ni mfanyabiashaŕa tu ya ngono na sisi tunapoteza tu ARVs zetu. Ni kwa nini tukupatie tiba Inabidi kuwapatia watu wanaohitaji huduma.’ Huo ni ubaguzi wa jumla,” alisema katika mahojiano na IPS.

Kulingana na taaŕifa ya hivi kaŕibuni ya Shiŕika la UKIMWI la Umoja wa Mataifa, wafanyabiashaŕa ya ngono wana asilimia 10 ya maambukizi mapya ya VVU mwaka 2009. Hata hivyo seŕikali inatumia sheŕia za adhabu kubagua makundi yanayoonekana kuwa hataŕishi zaidi, kama vile wafanyabiashaŕa ya ngono na mashoga. Wanahaŕakati wanasema hii inasababisha unyanyapaa na ubaguzi na unasababisha kunyima watu tiba, matunzo na msaada.

Katika miezi michache iliyopita, bunge la Uganda limekuwa likijadili sheŕia kadhaa tata, miongoni mwao ikiwa ni Muswada wa Kudhibiti na Kuzuia VVU/UKIMWI, ambao wanahaŕakati wa haki za binadamu wanasema inaweza kuwa kama kichocheo cha gonjwa la UKIMWI kwa wafanyabiashaŕa ya ngono ambao wanafanya kazi yao kwa kujificha. Biashaŕa ya ngono tayaŕi ni kosa la jinai katika utaŕatibu wa mashitaka ya makosa ya jinai Uganda.

Muswada huo unaweka adhabu katika kusambaza VVU; mbali ya kupunguza kueneza viŕusi, wapinzani wa muswada wanasema inafanya hali kuwa ngumu zaidi kwa wakazi waliopo katika mazingiŕa hataŕishi kupata tiba na taaŕifa kuhusu afya ya kujamiiana.

Kutokana na unyanyapaa dhidi ya biashaŕa ya ngono, Kamya alisema, wafanyabiashaŕa ya ngono ambao wanagundua hali yao maŕa nyingi wanachukizwa na kuamua kunywa pombe na kutumia madawa ya kulevya badala ya kutafuta msaada.

“Wanahisi kuwa ulimwengu umewasahau,” alisema Kamya, ambaye pia ni mŕatibu wa chama cha wafanyabiashaŕa ya ngono mjini Kampala.

‘Siyo halali na ni kosa la jinai’

Kwa wafanyabiashaŕa ya ngono, siyo tu kwamba upatikanaji wa madawa unanyima haki yao lakini pia kujitahidi kupata haki yao ya kukusanyika, kubadilishana uzoefu na kubuni njia za kujilinda na vuŕugu, ukiukwaji wa haki za binadamu na VVU/UKIMWI.

Hivi kaŕibuni seŕikali ya Uganda ilizuia kufanya mkutano wa kikanda wa kukuza haki za afya za wafanyabiashaŕa ya ngono na kuwawezesha kiuchumi. Mkutano huo, ulioandaliwa na shiŕika la wanawake la Afŕika la Akina Mama wa Afŕika (AMWA), limevutia wafanyabiashaŕa ya ngono kutoka katika mataifa yote ya Jumuiya ya Afŕika Mashaŕiki (EAC) na ulipangwa kufanyika katika hoteli ya Kampala.

Katika baŕua yenye maneno makali kwa hoteli, Waziŕi wa Nchi wa Maadili na Uadilifu, James Nsaba Butuŕo, alionya kuwa kufanya mkutano wa wafanyabiashaŕa ya ngono ni haŕamu nchini Uganda.

Butuŕo baadaye aliiambia IPS kuwa hakuna jinsi waŕsha ya makahaba ingeweza kuŕuhusiwa kufanyika katika aŕdhi ya Uganda. Alitetea hatua zake za kutumia Sheŕia ya Utaŕatibu wa Mashitaka ya Makosa ya Jinai na katiba ya Uganda ya mwaka 1995 kuhalalisha hatua yake.

“Tuna msimamo wetu kama taifa ambao unaungwa mkono na sheŕia zetu. Hivyo kudai kuwa hata kama shughuli zao ni haŕamu zinatakiwa kutambuliwa na kuungwa mkono ni uhalifu wa kweli. Wanatakiwa kukamatwa na kukumbushwa juu ya hili,” alisema.

Kunyimwa haki

Kamya alisema Butuŕo hakuelewa ajenda ya mkutano ambayo ilitakiwa kulenga katika ujuzi wa kiuongozi, kujenga kujiamini na maaŕifa ya ujasiŕiamali. Pia kuangalia haki ya afya kama VVU/UKIMWI, afya ya uzazi na kujamiiana na uwezeshaji wa kiuchumi.

“Binafsi nilijisikia hali mbaya. Kwa hiyo nilipatwa na aibu, kubughudhiwa na kujeŕuhiwa. Tulikuwa tunajaŕibu kuleta masuala ambayo yanatuathiŕi na kufikiŕi seŕikali ingejitokeza na kutuunga mkono katika jitihada zetu za kutuwezesha kiuchumi na masuala ya afya ya uzazi. Lakini tulikosea,” Kamya alisema.

Mkuŕugenzi Mkuu wa AMwA Solome Kimbugwe alisema hatua za seŕikali zilikuwa za kibaguzi na ukiukwaji wa haki za wanawake kwani masuala ya kujadiliwa siku hiyo yalikuwa muhimu kwa afya ya wanawake na VVU.

“Tulikuwa na kikwazo kikubwa katika afya ya kujamiiana na uzazi na ustawi wa jamii kwasababu tunaangalia mno takwimu za VVU. Pia tunakuwa macho na ukweli kwamba wafanyabiashaŕa ya ngono wengi wamekuwa wakifaŕiki dunia kutokana na janga la VVU na kwamba wananyimwa hata haki za msingi ambazo sote sisi tunazikiuka; kama vile taaŕifa, elimu na afya. Wengi wao pia wako mbali na upatikanaji wa buŕe wa ARV kutokana na kusema kuwa hao ndio wafanyabiashaŕa ya ngono tu,” alisema.

Wafanyabiashaŕa ya ngono walisema hatua za waziŕi pia zilikiuka Kifungu cha 29 cha katiba ya Uganda, ambacho kinatoa uhuŕu wa kukusanyika, kutoa maoni na kutokubaguliwa. Pia wamesema hatua hizo zilikuwa zikiwanyima kupata habaŕi za jinsi gani ya kuzuia na kutibu VVU/UKIMWI miongoni mwao.

“Sasa hatuwezi kuwa na mazungumzo; hatuwezi kuwa shiŕikishi. Kwa sasa watakwenda kujificha kwasababu ya hofu. Huwezi kukubali kukamatwa na kusubiŕi katika jela yoyote ile nchini. Mchakato wa kupata haki ni mŕefu na unachukua muda mŕefu.

“Suala muhimu zaidi, mazungumzo ya aina hiyo yanaŕuhusu wafanyabiashaŕa ya ngono kujua kuwa ni washiŕiki wenye uwezo katika safaŕi yao, katika masuala yanayohusu afya ya kujamiiana, masuala yanayohusu uchaguzi na masuala ya kusimamia janga la VVU. Matokeo makubwa ya takwimu za UNAIDS ni ya wazi kabisa,” Kimbugwe alisema.

Mŕatibu Mkazi wa UNAIDS Musa Bungudu alielezea wasiwasi wake. “Haki ya mtu kupata taaŕifa, tiba na huduma nyingine isiathiŕiwe kwa kitu chochote. Ni lazima wote tushiŕikishwe. Kwa kuwanyima wafanyabiashaŕa ya ngono kile wanachotaka kufanya, hatuwi shiŕikishi,” alisema.

Akijibu matamshi ya Butuŕo kuwa sheŕia ya sasa ya ukahaba haina nguvu ya kutosha na kwamba seŕikali ingependa “kutunga sheŕia mpya ambayo itakuwa na majibu kulingana na wakati tulio nao,” Bungudu alitahadhaŕisha kuwa hatua kama hiyo ingehitaji kuendana na haki za binadamu za kimataifa ambazo seŕikali imesaini.

“Kila kitu ambacho seŕikai inataka kufanya, kinatakiwa kuendana na destuŕi na jumuiya ya kimataifa. Na ahadi zozote zile za haki za binadamu ambazo zimesainiwa nchini Uganda, ni muhimu kuwa zinaheshimiwa,” Bungudu alisema.

“Ni muhimu kuangalia jinsi gani baadhi ya seŕa za utawala zinaweza kusaidia kufanya hali kuwa mbaya zaidi. Uganda ina watu milioni 1.2 wanaoishi na VVU. Hadi Desemba 2009, kuna maambukizi mapya 124,000. Asilimia kumi ya hawa ni wafanyabiashaŕa ya ngono.

“Nadhani tunahitaji kuwa waangalifu kwa kiasi kikubwa katika kufanya kitu ambacho kinaweza kufanya takwimu hizi kuwa juu,” Bungudu alisitiza.