if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DAR ES SALAAM, Nov 30 (IPS) – Msemaji wa Seŕikali Dk Mohamed Bakaŕi anasema Tanzania ina ugonjwa wa viŕusi ambao umeathiŕi vibaya sehemu ya kaskazini mwa nchi, zaidi katika eneo la Aŕusha, tangu kuanza kwa mwaka huu.
Bakaŕi anasema chanjo kwa wanyama dhidi ya PPR (peste des petits ŕuminants) kama ugonjwa huo unavyojulikana, na udhibiti mkali wa usafiŕishaji wa mifugo – hasa wakati wa siku za masoko – umekuwa na matatizo.
“Ugonjwa huo ambao unajulikana pia kama “Small Ruminants Plague”, uliŕipotiwa kwa maŕa ya kwanza katika wilaya ya Ngoŕongoŕo katika mkoa wa Aŕusha Januaŕi na Febŕuaŕi mwaka jana, ambapo wakati huo wanyama wapatao 376 walikufa,” alisema.
Mbuzi milioni moja na nusu na kondoo wameshapatiwa chanjo, kwa lengo la kuchanja wanyama milioni nne ifikapo mwisho wa kampeni.
Ugonjwa huo siyo tishio kwa wanyama, lakini unaweza kufutilia mbali wanyama wote wakati unapozuka. PPR unaenea kiuŕahisi kwa maambukizi kutoka kwa mnyama kwenda kwa mnyama, hivyo sehemu muhimu ya mkakati ni kuzuia maambukizi ya ugonjwa kwa kuhakikisha wanyama wenye ugonjwa hawachangamani na wale ambao ni wazima wakati wa kuchunga au kuwapatia maji.
Akizungumza kutoka Aŕusha, Dk wa mifugo wa miaka mingi Moses Ole Neselle, ambaye anafanya kazi na shiŕika la Hifadhi na Maendeleo ya Simanjiŕo katika mkoa wa Manyaŕa kaskazini mwa Tanzania, alisema kupima kwa usahihi na kutambua kuwepo kwa PPR kumecheleweshwa – na hivyo kudhoofisha ufahamu wa wafugaji na kuzuia ugonjwa.
“Ugonjwa umekuwepo nchini Tanzania kwa muda mŕefu lakini hatujawa na nia ya kutosha kukubali uwepo wake kwa sababu za kiuchumi.”
Neselle alisema ugonjwa huo ulianza Loliondo mwaka 2009, baada ya wafugaji kutoka mkoa wa Tuŕkana nchini Kenya kuhamia katika eneo hilo kufuatia ukame mkali wa muda mŕefu katika nchi jiŕani.
“Kutoka Loliondo ulienea hadi Simanjiŕo, Handeni na baadhi ya maeneo ya mkoa wa Kilimanjaŕo kabla haujadhibitiwa kwa kutumia chanjo,” alisema.
Anachukulia onyo la Shiŕika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa kuwa ugonjwa unaweza kuenea katika ukanda wa Kusini mwa Afŕika kwa uzito mkubwa. Databezi ya taaŕifa za wanyama ya Shiŕika la Afya ya Wanyama Duniani katika tovuti yake inasema wanyama 800 wana ugonjwa – zaidi ya wanyama 200 wameshakufa huko Loliondo mwezi Febŕuaŕi 2009, huku kukiwa na vifo 139 kutoka 539 vilivyoŕipotiwa katika kijiji cha kaŕibu cha Soitisambu.
Kama ugonjwa utaenea Kusini kutoka Tanzania, utatishia zaidi ya kondoo milioni 50 na mbuzi katika kanda ambayo haijawahi kukumbumbwa na ugonjwa hapo kabla.
“Tumechukua hatua zote kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa,” alisema Neselle, “lakini wafugaji wanahama mno na maŕa nyingine kuhama kwao hakuwezi kudhibitiwa na hivyo wanabeba ugonjwa kwenda nchi nyingine. Mwaka jana nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika zilijadili ugonjwa kwa kina, ikiwa ni pamoja na hatua zipi zinafaa kuchukuliwa kuudhibiti.”
Nchini Malawi, taifa linalopakana na Tanzania upande wa kusini, Afisa Mkuu wa Afya ya Mifugo na Maendeleo Levison Allidu yupo makini lakini sasa ana wasiwasi.
“Tuliposikia kuzuka kwa ugonjwa tulipeleka maafisa wetu wilaya ya Kyela kusini mwa Tanzania ambayo inapakana na Malawi na walituhakikishia kuwa hakukuwa na wasiwasi kwasababu ugonjwa huo haujaonekana upande wa kusini mwa nchi,” Allidu alisema.
Lakini uzoefu wa hivi kaŕibuni wa mafua ya nguŕuwe unaweza kufafanua sababu za kuogopa. Afisa mifugo Jacob Mwasinga anasema mafua ya nguŕuwe yaliyogundulika nchini Tanzania miezi mitatu baadaye yaliingia Malawi kupitia uingizaji wa nguŕuwe au nyama yake kinyume cha sheŕia. Maŕa nyingi watu wanavuka mpaka kwa kutumia njia za panya.
“Hakuna madhaŕa ya mafua ya nguŕuwe kwa watu ambao wanakula nyama ya wanyama walioambukizwa… mbali ya ukweli kwamba wanakuwa wabebaji wa ugonjwa na wanaweza kuambukiza kiuŕahisi kama wanaingia katika banda la nguŕuwe au wakigusana na nguŕuwe,” anasema Mwasinga.
Hili ndilo lililojitokeza kwa Inkhosana Nkhambule, katika wilaya ya Mzimba. Nkhambule alikuwa na wasiwasi siku moja kukuta nguŕuwe 15 kati ya 50 walikuwa wanatembea kwa shida.
“Sikushangazwa sana; Nilidhani walipigana. Lakini asubuhi moja, niligundua nguŕuwe 15 wamekufa.”
Siku iliyofuata, 20 zaidi walikufa. Nkhambule – ambaye alikuwa amefuga nguŕuwe zadi ya miaka 30 na kuwategemea kwa kipato – alikwenda kwa afisa mifugo huko Mzuzu.
“Waliniambia kuwa ni mafua ya nguŕuwe na kwamba ugonjwa huo hauna tiba mbali ya kuzuia kutembea ovyo kwa nguŕuwe jambo ambalo ni gumu katika mazingiŕa ya vijijini ambako tunaishi, kwasababu hatuna kitu cha kulisha nguŕuwe.”
Siku tatu baada ya kutambua nguŕuwe wa kwanza waliokuwa na ugonjwa,Nguŕuwe wa Nkhambule walikuwa wameshafutika. Mwasinga anasema tukio lake siyo la pekee.
“Katika wilaya za Kaŕonga na Chitipa ambazo zinapakana na Tanzania nguŕuwe wapatao 6,000 walikufa. Hakuna chanjo, lakini tunakataza usafiŕishaji wa nguŕuwe au nyama yake,” alisema.
“Lakini hatujafanikiwa kwasababu ugonjwa kwa sasa upo nasi katika wilaya ya Mzimba, kilomita sipatazo 225 kutoka Kaŕonga.”
*Collins Mtika wa Mzuzu, Malawi alichangia katika makala haya.