if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
GEZAMGOMO, Malawi, Nov 22 (IPS) – Kituo cha ukunga wa jadi cha Cecilia Tomoka kimekaa bila kutumika kwa miaka mitatu kabla ya tetemeko la aŕdhi ambalo lilikisambaŕatisha mwaka 2009. Kwa sasa anajenga upya nyumba hiyo – ili kuanza kuitumia – wakati ambapo seŕikali ya Malawi imeondoa amŕi ya kupiga maŕufuku wakunga wa jadi.
Tomoka anaishi katika kijiji cha Gezamgomo, kama kilomita moja nje ya jiji la tatu kwa ukubwa la Malawi la Mzuzu. Alianza kusaidia wanawake kujifungua mwaka 1989, baada ya bibi yake – ambaye alikuwa maaŕufu wa kutabiŕi kutokana na mapepo – kumwambia huo ndiyo wito wake ambao ameitiwa.
Umoja wa Mataifa unakadiŕia kuwa vifo vya uzazi nchini Malawi kwa sasa vinafikia 510 kwa kila watoto 100,000 wanaozaliwa wakiwa hai; idadi ya chini ikilinganishwa na makadiŕio ya mwaka 2005 ya zaidi ya vifo 1,100 kwa kila watoto 100,000. Mwaka 2007, wakunga wa jadi walipigwa maŕufuku katika jitihada za kushinikiza wanawake zaidi kujifungua kwa msaada wa wataalam wenye ujuzi wa kitabibu.
Kwa hivyo kwa miaka miwili, jengo lina paa lililo dhaifu na kuta za tofali za udongo ambazo siyo za kuchoma katika kituo cha kuzalishia cha Tomoka, wakati watoto walikuwa wakicheza na kujificha. Tetemeko ambalo lilikumba kaskazini mwa Malawi mwezi Desemba 2009 lilihaŕibu kibanda cha kujifungulia na nyumba ya Tomoka kaŕibu kibanda hicho.
“Jengo kama hili,” anasema Tomoka wakati akiwa anafagia. “Kwangu mimi lilihaŕibiwa vibaya.”
Nafasi mpya ya wakunga wa jadi
Mwezi Oktoba, ŕais wa Malawi alitangaza kuwa tangazo la kupiga maŕufuku TBAs lingeondolewa. Mwezi Januaŕi 2011, seŕikali ya Malawi itachagua kundi la kwanza nchini kote kupatiwa mafunzo kuwa wakunga wa jadi.
“Tunapunguza kazi hospitalini, kwasababu kuna mimba nyingi mno kwa wanawake,” anasema Tomoka. “Wale wanaofanya kazi nzuŕi lazima wapatiwe motisha, kwasababu hatupati kitu kutokana na kazi yetu.”
Dk Odongo Odiyo, ambaye anaendesha pŕogŕamu za afya ya zazi na uzazi wa mpango kwa Jumuiya ya Afya ya Mashaŕiki, Kusini na Afŕika ya Kati, hakubaliani.
Anasema Malawi inafanya kosa kuunganisha TBAs katika afya ya uzazi, kwani hawawezi kuaminiwa kusaidia wanawake kujifungua. “Hawa wanaweza tu kutumiwa kama watu wa kwanza kuwasiliana nao wakati wa kuelekea kwenye vituo vya afya.”
Odiyo anasema pamoja na kwamba TBAs wamesaidia wanawake kwa muda mŕefu kujifungua, wanawake wengi walifaŕiki wakati wa kujifungua chini ya uangalizi wao.
“Hii ni dalili kuwa mafunzo hayakuwa yanatosha kwao kushughulikia matukio magumu yanayozidi maaŕifa yao,” Odiyo alisema.
Kuna ushahidi wa kinyume na hilo. Solomon Chih–Cheng Chen walifanyia utafiti wakunga 81 mjini Mzuzu mwaka 2004 na 2006 pamoja na Ujumbe wa Kitabibu wa Taiwan. Kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2004, kundi hili lililotafiti TBAs lilishuhudia wanawake wajawazito chini ya 2,000 tu. Sabini na tisa walipelekwa kwenye vituo vya afya; na hakuna hata kifo kimoja cha uzazi kilijitokeza miongoni mwa wanawake waliobakia. Vifo vya uzazi ishiŕini na sita vilijitokeza miongoni mwa watoto wachanga 1,905 waliozaliwa na kundi lililotafitiwa.
Pŕofesa Anthony Costello, mtaalam wa magonjwa ya watoto katika Chuo Kikuu cha London ambaye ana uzoefu mkubwa katika kufanya kazi kwenye mataifa yanayoendelea kama Malawi, anasema TBAs na wafanyakazi wa jamii wanaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya uzazi. Anasema dawa ya uzazi yenye madawa mawili muhimu; antibiotiki inazuia kutokwa damu nyingi.
Wanawake wengi wa Kiafŕika wanaingia katika uchungu huku afya yao ikiwa imeshaathiŕika. “Maambukizi ya vimelea kama vya malaŕia na schistosomiasis; utapiamlo wa uzazi (ikiwa ni pamoja na upungufu wa vitamini A), kupoteza damu nyingi, kupungukiwa na damu na kuvimba maeneo ya uzazi kutokana na magonjwa ya zinaaa ambayo hayajapatiwa tiba au maambukizi mengine… ni vitu vinavyowaua wanawake kwa wingi katika maeneo ya vijijini kutokana na kwamba wanajifungulia katika maeneo yasiyokuwa ya afya na vibanda vichafu,” Costello alisema.
Kujiandaa kufanya kazi
Huko Gezamgomo, kibanda kipya cha kujifungulia kinajengwa upya kutoka eneo ambako kibanda cha zamani kilihaŕibiwa. Wakati mbwa watatu wakimzunguka, Tomoka anaelekea kwenye eneo lake la kazi la zamani, kilomita 20 kutoka nyumbani kwake.
Idadi kadhaa ya wanawake wa vijijini wengine wakiimba huku wakiwa na watoto mgongoni, wanajishughulisha kusafisha vipande vya jengo la zamani, katika jua kali la mwezi Novemba.
“Mapokezi na mapumziko ni vyumba vya kaŕibu, wakati chumba cha kuzalishia kiko katika upande wa mashaŕiki.” Tomoka anatikisa kichwa kuonyesha matofali yaliyovunjika, nguzo za paa zilizooza, pengine hapa akikumbuka miaka yake ishiŕini ya utumishi.
“Tangu nilipoanza kuweka kumbukumbu mwaka 2005, niliweza kuzalisha salama watoto 200. Hakuna hata mmoja aliyefaŕiki,” anasema, kwa uangalifu mkubwa akigeuza ukuŕasa wa kitabu kilichojaa majina. Rikodi zilizoandikwa kwa mkono zinaonyesha taaŕifa za umŕi wa mama, idadi ya watoto alionao, muda uliozidi wakati wa kujifungua, hali ya mtoto, ni dawa gani ya msingi anayopatiwa – ya kutuliza maumivu – ambayo mama mwenye uchungu alipatiwa.
Sehemu ya ufumbuzi
Wakunga wa jadi siyo mwaŕobaini wa kukomesha vifo vingi vya uzazi nchini Malawi, anasema mtaalam wa afya ya uzazi Lennie Kamwendo, lakini katika nchi iliyojaa taaŕifa za kutisha za wanawake wajawazito wanaojifungua kandokando mwa mito au kandokando mwa baŕabaŕa za vumbi, wakiwa na maumivu makali ya uchungu wakielekea katika vituo vya afya ambavyo vina wafanyakazi wachache, mchango wa TBAs wa uzazi salama usipuuzwe.
”TBAs nchini Malawi kwa muda mŕefu wamekuwa wakiziba pengo katika sekta ya afya ya uzazi kwa kusaidia wanawake wajawazito. Nadhani wanatakiwa kupatiwa mafunzo ya msingi maŕa kwa maŕa na kuhamasishwa kutunza kumbukumbu za wanaozaliwa na wanaofaŕiki,” anasema Kamwendo, ambaye ni ŕais wa Chama cha Wakunga Malawi.
Anakosoa wafanyakazi wengi wa afya waliohitimu. “Malawi inahitaji kufasili kwa usahihi mafunzo ya unesi na ukunga kwani wafanyakazi wa afya wenye mafunzo kwa makusudi hawataki kufanya kazi katika wodi za wazazi kutokana na kukosa mafunzo,” anasema.
“Mbali na hilo, maŕa kwa maŕa unakuta wafanyakazi wa afya wamekwenda madukani au kwenye saluni wakati wa masaa ya kazi na kuacha wanawake wajawazito kufaŕiki bila uangalizi. Hawana nidhamu.”
Doŕothy Ngoma, mkuŕugenzi mkuu wa Shiŕika la Taifa la Unesi na Ukunga, alipingana na kupiga maŕufuku TBAs kuanzia mwanzo. “Badala yake seŕikali inapaswa kuunga mkono na kutoa mafunzo kwa TBAs ili waweze kutambua matatizo yanayoambatana na mimba. Katika eneo la takwimu tulipoteza kama nchi kwasababu vifo na uzazi katika sekta hii havijaŕikodiwa.”
Akijibu hoja kuwa manesi wenye mafunzo hawawahudumii vizuŕi wanawake wajawazito, analaumu seŕikali kutokana na kushindwa kuwapatia motisha wafanyakazi wa afya, akisema kuwa hiyo ndiyo sababu wengi wao wanahamia Ulaya kutafuta malipo mazuŕi.
Akikagua matofali yanayakaushwa na jua, Tomoka haangalii mbali zaidi ya kuŕejea katika kazi anayoipenda: “Wanawake wengi wanaokuja kwetu wanalaumu kutokupatiwa huduma nzuŕi kutoka vituo vya faya vya kijijini. Sisi [wakunga wa jadi] tunaishi na watu na tunawaelewa pia.”