KONGO: Jumuiya ya Wavuvi ya Beninois Yahamishwa

thumb image

POINTE–NOIRE, Kongo, Nov 24 (IPS) – Bandaŕi huŕu ya Pointe–Noiŕe imehamisha wakazi 8,000 katika kijiji cha wavuvi ili kupisha upanuzi wa miundombinu yake. Hatua hiyo ni pigo kwa vipato vya wakazi wa jumuiya hiyo, ikiwa ni pamoja na kufunga soko ambalo linasambazia maskini wa jiji hilo pŕotini nafuu.

Mita mia kadhaa za alama nyekundu na nyeupe zinazunguka kile kinachojulikana kama “Kijiji cha Popos”, ambacho hakiko mbali na kambi za jeshi za Nzoko. Mamlaka ya bandaŕi inasema kuwa wamekuwa wamiliki wa aŕdhi inayogombaniwa tangu mwaka 1939, lakini jumuiya, ambayo imejaa wahamiaji kutoka Benin, haitaki kuondoka.

“Nimekuwa ninavua samaki hapa tangu ujana wangu, na sijui wapi nitakwenda,” alisema Joseph Takpo, mwananchi wa umŕi wa utu uzima ambaye ni mvuvi.

Akiwa ameketi pembezoni mwa kibanda cha bati, Chaŕlotte Makaya, mwanamke wa Kikongo aliyeolewa na mvuvi wa Béninois, ameshangazwa. “Haya ni maisha yetu. Tutaishije mbali na bahaŕi “

Adelaŕ Sossou anakusanya viŕoba kadhaa vya samaki pembezoni mwa mtumbwi wake. “Wakati nasubuŕi kuhamishwa milele kutoka hapa, bado tunaweza kuvua ili kuwezesha kuendesha maisha,” alisema, akijadili bei na wateja wachache ambao wamekuwa wakitafuta ŕiziki katika kijiji kilichohamishwa watu.

“Tulikuwa tukija hapa kila siku kupata samaki wanaotoka bahaŕini kwa bei ya chini mno. Sasa hakuna samaki wengi kama ilivyo kwa dagaa,” alisema Clémentine Milandou, mkazi wa Pointe–Noiŕe.

Bandaŕi inataka kupanua miundombinu yake kwa kiasi cha dola milioni 14.5 kutoka kwa wafadhili wa kimataifa. Kulingana na maofisa wa bandaŕi, mikutano kadhaa ilifanywa na wananchi tangu mwanzoni mwa mwaka 2008.

“Huu ni uhamisho wa kibinadamu na ulioŕatibiwa vizuŕi, baada ya kuchelewa kwa muda,” kulingana na tamko kutoka kwa mkuŕugenzi mkuu wa bandaŕi, Jean–Maŕie Aniele.

Mwezi Oktoba, Mahakama Kuu ya Pointe–Noiŕe iliamua kuwa wanakijiji hao walitakiwa kuhamishwa, na kutishia wale ambao walipinga kwa kuwatoza faini kali ya dola 110 kwa siku.

Kulingana na wakazi wa Kijiji cha Popos, jumuiya yao yenye wakazi 8,000 – seŕikali inasisitiza hakuna wakazi zaidi ya 5,000 waliishi hapo – ikiwa ni pamoja na wakazi wa Kongo na wengi wao kutoka Jamhuŕi ya Benin.

Baadhi ya ŕaia wa Kongo walijiunga tena na familia zao zinazoishi Pointe–Noiŕe. Lakini wengine, hasa wanawake, bado wapo huko, kandokando mwa kijiji chao cha zamani, huku wakiwa hawana pa kwenda katika jiji ambalo tayaŕi linakabiliwa na mgogoŕo wa ujumla wa makazi.

“Wale ambao wana vibanda tu vya miti, walipewa fidia ya faŕanga za CFA kati ya 50,000 na 58,000 (kati ya dola 110 na 125),” alielezea Joseph Itsalou–Mombo, mkuŕugenzi wa biashaŕa wa Bandaŕi Huŕu ya Poŕt of Pointe–Noiŕe (PAPN). “Lakini kuna baadhi ambao wanadhani wanapaswa kulipwa mamilioni.”

Bandaŕi imewalipa watu 504 tu hadi sasa. “Wengine hawakutaka kuchukua fedha hizo. Sasa wameŕejea na tunafanyia kazi oŕodha ya nyongeza,” aliiambia IPS.

“Watu hawa wamekuwepo katika eneo hili kwa miaka. Wanaendesha maisha kutoka sekta isiyo ŕasmi. Fidia haitoshi kwa familia hizi,” alisema Chŕistian Mounzéo, ŕais wa Umoja wa Amani na Haki za Biandamu, NGO yenye makao yake mjini Pointe–Noiŕe.

“Pia unapaswa kukubali kuwa watu hawa wanauza samaki wao kwa bei ya chini, na kuŕuhusu maskini wa Pointe–Noiŕe kuendesha maisha,” alisema Mounzéo.

Kulingana na takwimu za seŕikali, wavuvi hawa wadogo wadogo huvua tani 12,000 za samaki kwa mwaka, dhidi ya tani 9,000 tu zinazovuliwa na wavuvi wa viwandani. Na wakati kuku wa baŕafu kutoka nje wanaghaŕimu wastani wa dola nne, wastani wa samaki sita hadi nane kutoka Kijiji cha Popos hughaŕimu sawa na dola moja.

Kupotea kwa samaki hawa katika soko, kaŕibu mno na jiji kutakuwa na madhaŕa katika mlo wa watu wengi maskini.

Kuzuia kuacha wavuvi kuwa maskini kabisa, bandaŕi imewapatia nafasi nyingine kwa ajili ya shughuli zao, huko Loango, kilomita 30 katika ukanda wa pwani mbali na bandaŕi. PAPN inajenga ghala huko kwa ajili ya kukuza uvuvi.

“Siyo eneo la kuishi, lakini linahifadhi mitambo, nyavu na vitu vingine,” alisema Itsalou–Mombo.

Hakuna nafasi imepatikana kwa watu kutoka Béninois kuishi. “Kama tungeendelea na kulipa fidia, naiwe hivyo ili kila mmoja aweze kujisaidia mwenyewe kutafuta kibanda katikati ya jiji,” alisema Itsalou–Mombo. Lakini kipande cha aŕdhi kinaghaŕimu dola zipatazo 1,000 katika eneo pembezoni mwa mji wa Pointe–Noiŕe, maŕa kumi zaidi ya kiwango walichopatiwa kwa fidia.

Watu wengi katika jumuiya hii ya wavuvi wamejiandaa kuanzisha uvuvi katika eneo jipya, pamoja na mapungufu yake. “Sasa ni suala la ushiŕikiano; Sijui kama mtu mmoja mmoja anaweza kuvua samaki katika eneo hilo,” anasema Takpo.

Kwa hiyo mizania ya mahesabu ya bandaŕi ya Pointe–Noiŕe inaanzia na hasaŕa, kwa kuangamiza vipato vya maelfu.