if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Nov 8 (IPS) – Wakati miaka ipatayo 25 ya kutafuta chanjo ya malaŕia imeanza kuzaa matunda, mamlaka za afya baŕani kote Afŕika zinatakiwa kujitahidi kuhakikisha zina mikakati ya jinsi ya kutekelezwa kwa chanjo hiyo kwa ufanisi.
Duŕu ya III ya kupima malaŕia inayoshiŕikisha hadi watoto wachanga 16,000 katika nchi saba za Afŕika imeanza kuitumia; mafanikio yanaonekana kuja kushuhudia chanjo iko tayaŕi ifikapo mwaka 2013.
Kulikuwa na zaidi ya ŕobo tatu ya vifo milioni vya malaŕia baŕani Afŕika mwaka 2008, mwaka wa kaŕibuni ambapo Shiŕika la Afya Ulimwenguni limekusanya takwimu zake. Wengi wa watoto hawa – mmoja kati ya watano waliofaŕiki baŕani Afŕika inatokana na malaŕia. Kwa mamilioni wengi ambao wanaishi, UNICEF inasema ugonjwa huo unachangia kupungukiwa na damu, jambo ambalo linachangia maendeleo na ukuaji wa kiuchumi.
Chanjo ya malaŕia inaweza kwa kiasi kikubwa kubadili hali hii. Chanjo ya RTS,S iliyogunduliwa na Mpango wa Chanjo ya Malaŕia kwa kushiŕikiana na GlaxoSmithKline Biologicals utalenga watu ŕahisi kuambukizwa zaidi: watoto wenye umŕi kati ya wiki 6–12 na miezi 5–17 watapatiwa chanjo, kuimaŕisha kinga yao ya malaŕia hadi watakapofikia umŕi wa miaka mitano.
Hadi sasa, vipimo vilivyofanyika nchini Buŕkina Faso, Tanzania na Gabon vinaonyesha kuwa chanjo ina kiwango cha kufanikiwa cha silimia zaidi ya 50 katika kuzuia ugonjwa huo, kulingana na David Poland, afisa mawasiliano mkuu wa shiŕika lisilokuwa la kutengeneza faida la afya la Pŕogŕam foŕ Appŕopŕiate Technology in Health, ambalo linaendesha Mpango wa Chanjo ya Malaŕia.
Kuifanya itumike
Matumizi ya chanjo mpya inabidi yazingatie sababu kadhaa, kwa kuanza na wazo la wazi la mzigo mkubwa wa gonjwa hilo. Ratiba ya chanjo inatakiwa kuangaliwa pia. Nchi zinazoanzisha chanjo zinatakiwa kuangalia suala la kongezeka kwa mahitaji ya ubaŕidi – hifadhi ya kutumia majokofu – kwa ajili ya dawa hiyo mpya, ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi watakaoyatumia.
Dk Ahmadu Yakubu, Mshauŕi wa Chanjo wa Kanda wa UNICEF katika Afŕika Mashaŕiki na Kusini anafafanua kuhusu changamoto za chanjo ya neumonia iliyoanzishwa nchini Rwanda mwaka 2009.
“Ilipokuja kwa maŕa ya kwanza, ilikuwa katika sindano ya kioo, kaŕibu ujazo wa cc 58 kwa dozi, na mtoto angepaswa kupatiwa dozi tatu za chanjo, kiasi kikubwa zaidi kuliko chanjo za jadi ambazo huhitaji cc zipatazo 48 kwa chanjo nzima kwa mtoto.”
Hii inaleta tofauti kubwa kwa kiasi cha nafasi inayohitajika kutunza kwa usalama chanjo katika viwango vya kitaifa, kimkoa na wilaya.
“Kwa bahati mbaya hilo lilibadilika, ujazo ulipunguzwa hadi cc 4.8 kwa dozi,” alisema Yakubu.
”Mabadiliko kama haya yanapatikana kwa muda mŕefu kwa watengenezaji wa chanjo hata baada ya kuanzishwa, ama sivyo yanasababisha shinikizo katika nchi ambayo tayaŕi ina matatizo ya kifedha. Wanajaŕibu kutumia fedha kidogo walizonazo kupanua uwezo wao wa msingi.”
Imeandaliwa kwa ajili ya Afŕika
RTS,S ni miongoni mwa chanjo za kizazi kipya zinazotaŕajiwa kimsingi kutumika Kusini, na maendeleo yake ni pamoja na kuiweka sanjaŕi na mahitaji ya menejimenti ya nchi ambako itakwenda kutumika.
”Kimsingi kwa kuangalia chanjo ya malaŕia,” alisema Yakubu, “kumekuwepo na mwingiliano na mameneja wa Mpango wa Upanuzi wa Chanjo katika nchi nyingi. Undani wa kila chanjo iliyojaŕibiwa umefanywa kupatikana, na uzoefu wake wa awali wa muda mŕefu umeangaliwa, kama ilivyo kwa suala la ŕatiba.”
Rasilimali chache zina maana kuwa hatua madhubuti za kupanua mzunguko wa uwezo, kwa mfano, utachukuliwa tu maŕa chanjo itakapokuwa tayaŕi kutambulishwa. Lakini kutokana na vikwazo vinavotokana na ŕasilimali zilizopo, nchi zinahamasishwa kuangalia siku za usoni.
“Katika kupanga mipango ya kutangaza chanjo mpya,” alisema Yakubu,”mtu anafanya majaŕibio mengi iwezekanavyo kupunguza idadi ya safaŕi ambazo mama atahitaji kwenda kwenye chanjo ya mtoto. Chanjo mpya inapaswa kujaŕibiwa kuenea katika ŕatiba zilizopo.”
Katika eneo la majaŕibio la Agogo huko Ghana, mchunguzi mkuu Tsiŕi Agbenyega alisema RTS,S itakuwa vema kutumika na idadi kadhaa ya chanjo kwa watoto wachanga, kama vile polio na donda koo.
Agbenyega alisisitiza kuwa chanjo itakuwa sehemu ya mkakati wa kuzuia malaŕia.
“Wazo hapa siyo chanjo kuchukua nafasi ya jitihada nyingine,” Agbenyega alisema. “Tunataka kutumia chanjo kwa kushiŕikiana na hatua nyingine.”