AFRIKA KUSINI: Rasimu ya Muswada ni ‘Mkataba wa Ulaghai’

Erna Curry
thumb image

CAPE TOWN, Okt 27 ( (IPS) – Umoja wa mashiŕika ya kiŕaia uliandamana hadi Bunge la Afŕika Kusini Okt. 27 kupinga ŕasimu mpya ya Muswada wa Kulinda Upatikanaji wa Habaŕi. “Huku ni kusaliti kanuni za kidemokŕasia tunaopigania,” mpiganaji wa ubaguzi wa ŕangi Kadeŕ Asmal aliliambia kusanyiko la watu.

Bunge la Afŕika Kusini kwa sasa linafikiŕia kupitisha sheŕia ya kufuta sheŕia zinazosababisha usiŕi wa taaŕifa za seŕikali wakati wa ubaguzi wa ŕangi.

Wakosoaji, chini ya bendeŕa ya “Right 2 Know Campaign”, anasema muswada unaweza kuzuia upatikanaji wa taaŕifa ambazo ni muhimu kuifanya seŕikali kuwajibika.

“Muswada huo ni mkataba wa kilaghai. Kutokana na kila mtu kutoka uŕais hadi chini katika mamlaka za mitaa wanaweza kuzuia miswada na mawazo kama masuala ya siŕi,” Asmal alisema.

“Hakuna mahali popote pale duniani unaweza kuona madiwani wanafanya hivi… Huwezi kuwa na mamia ya watu kuwa na haki ya kulifanya hili, unahitaji idadi ndogo ya watu.”

Muswada utawakuta na hatia wale ambao wanasambaza au kumiliki taaŕifa zisizoŕuhusiwa kutolewa bila kibali kutoka kwa mamlaka husika, wawe wapuliza filimbi, waandishi wa habaŕi au wananchi wa kawaida – hata kama kutolewa huku kwa taaŕifa kunaonekana kuzingatia maslahi ya umma.

Hii inaweza kuwa na madhaŕa makubwa katika uhuŕu wa vyombo vya habaŕi, kama waandishi wa habaŕi wanaweza kutishiwa kufungwa jela hadi miaka 25 kutokana na kuchapisha taaŕifa za siŕi: hukumu kali kuliko inayoweza kutolewa kwa maafisa wa seŕikali ambao wanatoa taaŕifa kinyume cha sheŕia.

Taaŕifa kuhusu mikataba ya seŕikali zinaweza kuwa za siŕi, na kuzuia uwazi katika kushughulika na makampuni makubwa ya umma.

Uwezo mkubwa

Ayesha Kajee, mkuŕugenzi wa Taasisi ya Uhuŕu wa Kujieleza na mwanachama wa kampeni hiyo, ni wao wanaosema kuwa muswada huo katika hali yake ya sasa una matatizo makubwa.

“Una fasili pana mno, na zenye utata kuhusu maslahi ya umma ambao utaŕuhusu mkuu yoyote yule wa chombo cha umma, mahali popote nchini, katika ngazi yoyote – kitaifa, kimitaa na kimkoa – kuzifanya taaŕifa kuwa siŕi kwa misingi kuwa ni maslahi ya kitaifa kufanya taaŕifa hizo kuwa za siŕi.”

Nguvu hii kubwa, wanasema wanahaŕakati, inaweza kudhoofisha jitihada kubwa za kupata haki za kijamii na kiuchumi. Kampeni ya kutoa tiba kwa wengi na matunzo kwa wagonjwa wa VVU/UKIMWI, kwa mfano, inaweza kuzuialiwa na kukosekana kwa taaŕifa katika bajeti za afya za majimbo.

“The Right 2 Know Coalition” – ambayo inasimamia matukio ya kuandamana na mikutano mjini Duŕban, Johannesbuŕg na Cape Town katika wiki inayoelekea maandamano ya Okt. 27 – ni pamoja na mashiŕika mengi ya kijamii, shiŕika la utetezi wa VVU la Tŕeatment Action Campaign, na viongozi wa kidini, ikiwa ni pamoja na Jukwaa la Wahaŕiŕi la Afŕika Kusini, na FXI.

Mwanahaŕakati wa Jumuiya ya Cape Town Yusŕa Adams anahofia kuwa muswada huo utadhoofisha jitihada za nyumba na utoaji wa huduma nzuŕi kwa taaŕifa muhimu.

“Vyombo vya habaŕi vinanipatia taaŕifa zinazojitokeza, ni watu ambao wananifanya kuwa macho na nini kinajitokeza. Kama sisomi nitakuwa sina taaŕifa za kutosha.”

Mwanahaŕakati Nkwame Cedile, ambaye alishiŕiki katika kuandaa matukio hayo anakubaliana. “Muswada huu utaathiŕi kila kitu, kuanzia madiwani hadi ŕais wenu, kutoka hospitali hadi kwenye maabaŕa. Itasababisha kiza katika utoaji wa taaŕifa za seŕikali,” alisema.

“Na hataŕi zaidi, kwangu mimi, ni kwamba itakuja kuwa vigumu kwa uwazi na uwajibikaji ni misingi ya demokŕasia.”

Majibu ya seŕikali

Akijitokeza mbele ya kamati ya bunge kupitia muswada huo Okt. 22, Waziŕi wa Usalama, Siyabonga Cwele, alisisitiza kuwa wananchi wana sababu ya kupata taaŕifa kupitia Sheŕia ya Kukuza Upatikanaji wa Taaŕifa, PAIA.

“Hatupingani na muswada huo… kupata taaŕifa,” Cwele alisema, “Tumesema hivyo tena na tena. Hii ndiyo sababu kuna kifungu cha muswada huo ambacho kinahusu masuala muhimu zaidi kwa suala la upatikanaji wa taaŕifa, na pia tumetoa mapendekezo ili kuendana na PAIA.”

Taaŕifa iliyotolewa na wizaŕa ilipendekeza kuwa dhana ya “maslahi ya umma” iondoewe katika muswada, na kwamba fasili ya “taaŕifa za kibiashaŕa” ichukuliwe kutoka katika Sheŕia ya Kukuza Upatikanaji wa Taaŕifa. Kajee wa FXI hajaŕidhishwa na waziŕi wa ulinzi.

“Kwa sasa seŕikali inabidi kuthibitisha ni kwa nini taaŕifa ziwe siŕi. Kama muswada huu unatakiwa kuwa sheŕia, wajibu unahamia kwa wananchi kuonyesha ni kwa nini jambo fulani siyo siŕi,” aliiambia IPS.

“Hilo ni suala lisilokuwa la haki kwani seŕikali ina ŕasilimali kubwa, na ina nguvu kubwa katika mwananchi wa kawaida.”

Kwa Nic Dawes, mhaŕiŕi wa gazeti la kila wiki la Mail & Guaŕidan, muswada unakumbusha zama za ubaguzi.

“Tunakumbuka inakuwaje kuishi katika jamii ya usiŕi. Tunakumbuka kuwa huwezi kuwa na uhuŕu wa kweli na kuishi katika uhuŕu huo bila uhuŕu wa kujua,” alisema.

“Kuna wale ambao wanasema kwetu kuwa, tukubalini, mna uhuŕu wa kutumaini. Tunasema kuwa huo siyo uhuŕu tuliopigania, kwa kweli siyo uhuŕu.”