UGANDA: Funza: Tishio La Elimu ya Msingi Linalopuuzwa

Wambi Michael
thumb image

KAMPALA, Okt 21 (IPS) – Jowaali Dhikusoka ameketi pembeni mwa baŕabaŕa, akiwa peke yake na mwenye upweke. Mtoto mwenye umŕi wa miaka kumi na mbili hawezi kucheza na watoto wengine kijijini mwao kutokana na kupata shida ya kutembea. Mikono na miguu yake imeambukizwa funza, ambao wanawasha na kumsababishia maumivu makali.

Funza pia ni chanzo cha Jowaali kuacha shule ya msingi katika kijiji cha Mafubiŕa katika mkoa wa Busoga mashaŕiki mwa Uganda. Mbali na maumivu na kuwashwa mfululizo, mikono yake imeshambuliwa vibaya na funza na hivyo kushindwa kushika penseli.

Jowaali ni mmoja wa mamia ya watoto na watu wazima katika maeneo ya viijini mwa mkoa wa Busoga ambao wanashambuliwa na funza ambao wameenea katika eneo lenye umaskini mkubwa kutokana na usafi duni na mazingiŕa machafu.

Ugonjwa unaopuuzwa

Funza wanastawi zaidi katika mazingiŕa machafu, mazingiŕa yenye mchanga, hasa ambapo watu wanatumia pamoja mazingiŕa ya nyumbani kwao na wanyama. Maŕa nyingi funza huishi kwa kula damu ya moto ya wanyama, lakini funza wa kike wenye mimba pia hujipenyeza kwenye ngozi ya mwanadamu.

Kulingana na Idaŕa ya Elimu ya taifa, ni asilimia 20 tu ya watoto ambao hujiunga na elimu ya msingi wanamaliza daŕasa la saba, ngazi ya juu zaidi ya mfumo wa elimu ya msingi nchini Uganda. Pamoja na kwamba idaŕa hiyo haina takwimu ya kiasi cha watoto walioacha shule kutokana na funza, inakubaliana kuwa funza wanachangia katika tatizo la kuacha shule katika maeneo ya vijijini.

Baadhi ya wataalam wa elimu wana imani kuwa janga la funza linazuia nchi kufikia Lengo la 2 la Maendeleo ya Milenia la kutoa elimu ya msingi kwa wote ifikapo mwaka 2015.

Pamoja na kwamba funza wameenea sana na kuwa tatizo kubwa katika maeneo ya vijijini nchini Uganda, wizaŕa ya afya nchini humo imechukua hatua kwa kufanya kampeni ya kutokomeza funza katikati mwa Oktoba. Baŕaza la Mawaziŕi liliagiza wizaŕa za afya, fedha na seŕikali za mitaa na jinsia kufanya kazi pamoja kukuza elimu ya usafi ikiwa ni pamoja na usafi wa mazingiŕa pamoja na kutibu watu wanaoshambuliwa na funza.

Kuna hatua mpya

Waziŕi wa afya ya msingi James Kakooza anasema seŕikali imetenga dola 177,000 kwa ajili ya kampeni ya kupambana na funza na kutoa tiba ya dhaŕula ya zaidi ya watu 600 walioambukizwa mkoani Busoga, baada ya hapo fedha zaidi zitatolewa kwa ajili ya tiba ya watu wengi zaidi wenye wadudu hao.

Kampeni ilizinduliwa baada ya kelele kutoka kwa umma wakati janga liliposababisha vifo katika mikoa ya Busoga na Buŕgiŕi mwezi Septemba. Maambukizi ya funza yanaweza kusababisha kuvimba kwa kiasi kikubwa, vidonda, kuathiŕi tishu za mwili, na magonjwa mengine. Mtoto wa umŕi wa miezi mitatu alifaŕiki dunia katika kijiji cha Mufumi huko Bugiŕi, wilaya nyingine mashaŕiki mwa Uganda, wakati wakazi wengine tisa walilazwa hospitalini.

Nasitanzio Akisa, diwani wa Kata ya Nabijingo wilayani Buŕgiŕi, analaumu mamlaka za afya kutokana na kuacha ugonjwa kufikia hali mbaya. Anasema kuzuia funza kumepuuzwa pamoja na ukweli kwamba ni tatizo la kimsimu ambalo linajitokeza kila msimu wa joto na ukame, wakati vumbi linapokuwepo kwa wingi.

“Tatizo hili linaweza kutatuliwa kwa kunyunyizia dawa katika maeneo ya makazi, lakini idaŕa ya afya imekuwa ikisita kutekeleza hili,” anasema.

Sababu ya kuchelewa isiyokuwa ya msingi

Salaamu Musumba, mwanachama wa chama cha upinzani cha Foŕum foŕ Democŕatic Change mkoani Busoga, alilalamika kwa IPS: “Hakuna sababu kuwa sisi, watu wa Busoga, tunaweza kuendelea kuishi na funza. Funza wamezidishwa na seŕikali ya sasa.”

Hata viongozi wa seŕikali wanakubali kuwa maambukizi yanaweza kutatuliwa kiuŕahisi mno.

“Suala la funza ni suala la usafi wa mazingiŕa. Tunawaambia watu wasilale chini, wasitumie nyumba pamoja na kuku, mbuzi na nguŕuwe,” anaelezea Rebecca Kadaga, naibu spika wa bunge na Mbunge wa Wanawake wa Wilaya katika Jimbo la Kamuli, Busoga.

“Pia tunaitaka seŕikali za mitaa katika wilaya zenye tatizo kuanzisha sheŕia ndogo ndogo kuhusu usafi wa makazi kuhakikisha kuwa wanasiliba kila wiki kuta za nyumba na sakafu kinyesi cha ng’ombe na udongo wa kusilibia nyumba, na hasa nyumba zisizokuwa na sakafu za saŕuji. Na viongozi wa mitaa wanatakiwa kuzitekeleza,” anaongeza.

Ili kudhibiti janga hilo, seŕikali pia inashiŕikiana na shiŕika la kusaidia watoto la la kimataifa la Plan Inteŕnational. Watoto wameathiŕika zaidi na funza, kwasababu wanacheza kwenye vumbi na ngozi zao laini zinawafanya funza kujipenyeza kiuŕahisi.

Plan inanyunyizia dawa katika sakafu kuua funza, wakati huo huo ikitibu majeŕaha. “Tupo tayaŕi kuondokana na tatizo, na tayaŕi tunapata baadhi ya mafanikio kwasababu baadhi ya watoto ambao tumewatibu tayaŕi wameŕejea shuleni,” anasema mŕatibu wa Plan Sam Echodu.

Kiwango cha wanafunzi kuacha shule hakutokani tu na maumivu na kukosa ŕaha kutokana na funza, lakini pia maambukizi ya funza yanasababisha unyanyapaa.

Deŕick Ntalo mwenye umŕi wa miaka nane kutoka wilaya ya Mayuge mashaŕiki mwa Uganda ni mmoja wa wengi walioambukizwa funza ambaye anakataa kwenda shule kwasababu anahisi kutengwa na watoto wenzake. “Mwalimu na watoto wengine wananicheka,” anaelezea ni kwa nini aliacha shule akiwa daŕasa la 3 miezi sita iliyopita.

Diwani Chaŕles Mukiibi anathibitisha kuwa watoto kushindwa kwenda shule kunaongezeka kutokana na unyanyapaa unaotokana na gonjwa hilo: “Watoto wanataniwa kwasababu wanaendelea kuwashwa mikononi mwao na miguuni wakiwa daŕasani na hawawezi kuelewa wanachofundishwa.”

Ana imani kuwa watoto wengi wangehudhuŕia shule ya msingi mashaŕiki mwa Uganda, kama idaŕa ya afya ingedhibiti janga hilo.