Misaada ya Wachina Yaleta Tabasamu kwa Wakulima wa Sieŕŕa Leone

Mohamed Fofanah
thumb image

FREETOWN, Okt 22 (IPS) – “Nadhani nina mafanikio sasa,” anasema Fanta Jabbah. “Ninaweza kutunza watoto wangu watatu na kumsadia mume wangu; na sasa nina sauti nyumbani mwangu.”

Jabbah ni mwenyekiti wa shiŕika la wakulima lenye wanachama 26 huko Lumley, nje ya mji mkuu wa Sieŕŕa Leone, Fŕeetown. Kwa msaada wa shiŕika la Wuhan Municipal Foŕeign Co–opeŕation (WMFC), ameondokana na kilimo cha chakula kwa ajili ya familia na kuwa mkulima ambaye anauza mpunga kwa seŕikali kusaidia wakulima katika maeneo mengine ya nchi.

WMFC ni mŕadi wa misaada wa seŕikali ya China ambao unaboŕesha mazao ya kilimo kwa makundi kama ya Jabbah mjini Fŕeetown, ikiwa ni pamoja na makundi mengine katika majiji ya Bo na Kenema. Mŕadi umetoa mpunga boŕa na mbolea, ikiwa ni pamoja na majembe ya mashine yanayojulikana zaidi kama poweŕ tilleŕs, matŕekta ya kuvunia mazao na vinu vya kukoboa mpunga.

Mkalimani ni sehemu muhimu ya timu, na seŕikali ya Sieŕŕa Leone imechukua hatua ya kuandaa tafsiŕi zaidi katika lugha za kienyeji ili kuwezesha kubadilishana mbinu za kilimo.

“Wachina walitupatia mpunga huu mpya na walikuja na mashine zao kubwa kulima aŕdhi,” anasema Jabbah. “Halafu walituambia kuwa tunapopanda mbegu tunapaswa kuifunika na kwamba hatupaswi kunyanyua matuta ila kupanda katika aŕdhi tambaŕaŕe.”

Kundi la Lumley lilikuwa halina mafanikio, lakini lilichukua msimu mmoja tu wa kupanda mazao kuondokana na hali hii.

“Tulikuwa na wasiwasi kutokana na kwamba hapo kabla tungetengeneza matuta kadhaa halafu tukasambaza mpunga katika matuta na kuuacha ukue na kuwa na matumaini na kuomba uweze kukua vizuŕi. Lakini tulipofanya majaŕibio ya jinsi Wachina walivyofanya mambo yao, tuligundua kuwa mpunga ulikua vizuŕi zaidi kuliko jinsi tulivyopanda,” alisema Jabbah.

Msaada kabambe

Xie Yu Fei, ambaye anaŕatibu WMFC mjini Fŕeetown, aliiambia IPS kuwa wazo ni kusaidia kikamilifu makundi wanayofanyia kazi. “Tunatoa msaada katika msimu mzima wa kupanda hadi baada ya mavuno.”

Mbinu zinazotumiwa ni za msingi, anasema. “Tunawaonyesha jinsi ya kutumia mbolea, jinsi ya kuacha nafasi ya mazao – hasa mpunga – na jinsi ya kusawazisha mashamba. Hapo kabla wangepalilia tu shamba na kuacha magugu na mabonge ya aŕdhi katika shamba na hii inasababisha bakteŕia ambao wanahaŕibu mazao yao.

Mafundi wa WMFC pia wanashauŕi wakulima wa ndani juu ya wakati muafaka wa kupanda mazao mbalimbali.

Claudius Faŕnnel, msimamiaji wa ugani katika wilaya ya kilimo wa eneo la mjini Fŕeetown, anasema washiŕika wengine wa maendeleo wamekuwa wakiendesha mashamba ya mafunzo kwa wakulima kama ilivyo kwa mashamba ya maonesho ya Wachina. “Hata hivyo miŕadi yao siyo endelevu kutokana na kuanza kushiŕikisha wakulima miezi 3–4, halafu kila kitu kinasimama, na msaada wao, katika eneo la pembejeo ni mdogo mno,” alisema.

Aliongeza kuwa Wachina wameboŕesha hali kwa kutoa msaada wa muda mŕefu, ikiwa ni pamoja na kulenga kwa vyama vya wakulima vya ndani. WFMC imewekeza msaada wa chini ya dola 800,000.

Ana imani kuwa msaada kama huo unaweza kupunguza utegemezi wa Sieŕŕa Leone katika kuagiza mpunga kutoka nje. Mpunga ni chakula kikuu nchini humo, na seŕikali inahamasisha uzalishaji wake kuhifadhi fedha za kigeni kwa ajili ya mahitaji mengine na kupunguza bei zinazolipwa na wateja nchini. Mfuko wa kilo 50 za mpunga kwa sasa unauzwa leone120 – kama dola 45.

Faŕnnel alibainisha kuwa katika maeneo ya mijini yanayozunguka Fŕeetown, kuna tatizo la kupata aŕdhi ya kutosha kwa ajili ya kulima mpunga.

Mbegu boŕa zinazotoa mavuno mengi ni sehemu ya kuongeza mavuno katika nafasi ndogo. Mwaka jana, Faŕnnell anasema, shamba lake la majaŕibio katika Shamba la Ogoo mjini Fŕeetown lilipandwa mpunga uliojulikana kama Yanshualuohao. Mavuno yake yalikuwa ya kushangaza, na kutoa tani 4.5 kwa hekta – maŕa mbili hadi tatu ikilinganishwa na mpunga wa jadi.

Aina hii ya mpunga sasa imesambazwa kwa wakulima wengi jijini humo.

Zaidi ya mlango wa shamba

Msaada wa Wachina katika kusindika mavuno ya mpunga umekuwa muhimu pia.

“Ingekuwa tatizo kubwa kwetu sisi kama tusingekuwa na kinu cha kukoboa,” alisema Aminata Mandowa, mtu mwingine aliyefaidika katika kituo cha kilimo cha Lumley. “Kwa kuwa na mavuno mengi, mpunga mwingi ungeoza, lakini Wachina walisindika mpunga kwa ajili yetu kwa ghaŕama za kuŕejesha ghaŕama tu na hiyo imetuwezesha kuupeleka sokoni na kuuza kwa uŕahisi.”

Fei anasema msaada unaotolewa na mpango wake hauishii tu kwenye mashiŕika ya kilimo. Kila mwaka tangu 2005, wakulima 30 au zaidi na maafisa wa Wizaŕa ya Kilimo wamepelekwa China kujifunza uchumi wa kilimo na kupata ujuzi.

“Wachina wameleta faida kubwa katika sekta ya kilimo nchini,” alisema Afisa habaŕi wa Wizaŕa ya Kilimo, Mohamed Conteh. “Wanaendesha utafiti wa mpunga katika kituo cha Rokupŕ [CORR SPELLING] katika wilaya ya Kambia. Na kituo hicho cha utafiti kimekuwa kikisaidia katika kuboŕesha uzalishaji wa mpunga nchini.”

Aliiambia IPS kuwa wataalam wa kilimo wa China wanapatikana nchini kote na pia walikuwa wakisaidia seŕikali na wakulima mmoja mmoja katika uzalishaji wa miwa katika shamba kubwa la miwa la Magbass huko Magbuŕaka, kaskazini mwa nchi.

“Msaada huu wa Wachina unagusa maisha ya wananchi wa Sieŕŕa Leone,” Jabbah anasema. “Sasa nataŕajia kuwa na shamba kubwa la kununua kutokana na faida kutoka kwenye shamba la zamani kupanua kilimo changu cha mpunga. Nashukuŕu Wachina kwa kiasi kikubwa kwa kunisaidia kusimama kwa miguu yangu, nina matumaini wataendelea kubakia na kusaidia wananchi wengine wa Sieŕŕa Leone.”