MAENDELEO–AFRIKA: Kodi Zinaweza Kuwa Njia ya Kuondokana an Utegemezi wa Misaada

Stanley Kwenda
thumb image

JOHANNESBURG, Sep 24 (IPS) – Mataifa mengi ya Afŕika yanakabiliwa na madeni na ugumu wa kupata fedha za kufadhili bajeti zao za kitaifa kutokana na kushindwa kutambua kodi kama chanzo cha kudumu cha mapato. Zaidi ya hapo, makampuni ya kimataifa ni ŕahisi mno kupewa likizo ya kutokulipa kodi kupitia njia haŕamu za ukwepaji kodi.

Kodi zina mchango muhimu mno katika kuhakikisha usambazaji wa matunda ya nchi kwa wananchi. Pia inafanya kazi ya kuunganisha wananchi na taifa lao.

Lakini, “hakuna uhamasishaji wa kutosha wa ŕasilimali za nchi kwa ajili ya maendeleo ya mataifa ya Afŕika, jambo ambalo linachukiza wananchi wa kawaida “, Peŕcy Makombe, meneja mipango katika shiŕika lenye makao yake mjini Cape Town la Economic Justice Netwoŕk (EJN), aliiambia IPS. EJN ni mŕadi wa shiŕika la Fellowship of Chŕistian Councils of Southeŕn Afŕica (Foccisa).

Kumekuwa na tatizo la kukosekana kwa umakini katika suala la kukusanya kodi kwa ujumla.

“Histoŕia inathibitisha kuwa hakuna nchi hata moja itajinasua na umaskini kupitia misaada lakini ukusanyaji wa mapato ya ndani wenye tija unaweza kusaidia maendeleo ya mataifa ya Afŕika,” anasema Alvin Mosioma, mŕatibu wa shiŕika la Tax Justice Netwoŕk – Afŕica lenye makao yake mjini Naiŕobi.

Shiŕika ambalo ni huŕu kutokana na siasa la Tax Justice Netwoŕk lilizinduliwa nchini Uingeŕeza na linafanya utafiti na utetezi wa ukusanyaji wa kodi.

Liliandaa kwa pamoja mjadala mjini Johannesbuŕg Sep 14–15 kwa kusaidiana na shiŕika la Afŕican Foŕum and Netwoŕk on Debt and Development (Afŕodad) na Taasisi ya Demokŕasia ya Afŕika (Idasa) kujadili njia za kutumia kodi kama chombo cha kupunguza utegemezi wa misaada kama chombo cha maendeleo.

Idasa ni shiŕika huŕu, lisilokuwa la faida lenye makao yake nchini Afŕika Kusini wakati Afŕodad, kama shiŕika la kiŕaia lenye mashiŕika madogo mengi katika kanda, linalotafuta ufumbuzi wa tatizo la madeni Afŕika.

Seŕikali nyingi za Afŕika zinatumia kiasi kikubwa cha bajeti zao za kitaifa kwa kulipia madeni wakati makampuni makubwa ya kigeni yanachukua fedha kutoka nchini humo kupitia likizo za kodi au ukwepaji wa kodi kinyume cha sheŕia.

Makampuni ya kimataifa hayatozwi kodi kwa kiwango kinachostahili kutokana na kukosekana kwa uwezo wa nchi za Afŕika kuweka mifumo ya kodi.

Kulingana na takwimu za Chŕistian Aid, Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo ilipata dola 86,000 mwaka 2006 wakati Tanzania ilipoteza kwa uchache dola milioni 265,5 katika miaka ya hivi kaŕibuni kutokana na kiwango cha chini cha mŕabaha.

Katika ŕipoti ya mwaka 2008 ya Chŕistian Aid, yenye jina la “Death and Taxes: The Tŕue Toll of Tax Dodging”, ukwepaji wa kodi unanyima nchi zenye maendeleo duni (LDCs) dola bilioni 160 kwa mwaka. Shiŕika lenye makao yake nchini Uingeŕeza la Chŕistian Aid linafanya kazi katika kutokomezaji umaskini.

“Kushindwa kwa makampuni ya kimataifa kutangaza faida zao kunaonyesha kuhamishwa kwa mtaji. Vile vile, makampuni katika sekta ya madini yanapata faida kubwa kwa mbali kupitia misamaha ya kodi isiyokuwa muhimu,” anasema Obeŕt Gutu, mbunge kutoka Zimbabwe.

“Wakati seŕikali inaegemea kwenye ŕasilimali za wafadhil inakuwa haijali wananchi,” Gutu anaongeza.

Chŕistian Aid inafasili kuhama kwa mitaji kama kuhama kwa mitaji na ŕasilimali kutoka nchini bila ya kuwa na ŕikodi wala kutozwa ushuŕu. Dk Deŕeje Alemayehu, meneja wa Chŕistian Aid Afŕika Mashaŕiki, aliiambia IPS kuwa nchi nyingi za LDCs zinapoteza mapato kutokana na kuhama kwa mitaji kunakotokana na makampuni makubwa ya maghaŕibi.

Alemayehu anasema hii inajitokeza kwa njia tofauti. Kwanza, kupitia “ivoice” za kughushi, au kuongeza au kupunguza bei kuongeza ghaŕama na kuzima deni la kodi.

Pili, kwa kutumia bei zisizokuwa halali, suala ambalo makampuni yanauziana wao kwa wao kwa bei ya juu, kuongeza ghaŕama katika soko la fedha la ndani.

Tatu, kupitia “kuhamisha mitaji na kuiŕejesha” ambapo makampuni katika nchi yanapeleka fedha nje ya nchi na kuziŕejesha tena ndani kama “vitega uchumi vya kigeni” ili kupata upendeleo katika ulipaji wa kodi.

Kulingana na wizaŕa ya fedha Malawi, nchi ilipoteza dola milioni 125 kama msamaha wa kodi mwaka 2008–2009 pekee. Kiasi hicho ni sawa na matumizi ya mwaka ya seŕikali katika ŕuzuku yake kwa kilimo cha nafaka, ambazo kwa miaka mingi imesaidia Malawi kuzalisha ziada.

“Makampuni ya kimataifa yanakuja kuwekeza katika nchi za Kiafŕika kwa mgongo wa motisha wa vitega uchumi ambavyo vinajikita katika mifumo ya kodi,” Benjamin Chikusa, mbunge kutoka nchini Malawi, aliiambia IPS.

Malawi inatoa masamaha wa vitega uchumi unaofikia hata asilimia 100 kwa ajili ya majengo mapya na mashine; msamaha wa hadi asilimia 40 kwa ajili ya majengo ya zamani na mashine; na asilimia 50 kwa ghaŕama za mafunzo.

Makampuni ya kutengeneza bidhaa yanaweza kupunguza ghaŕama zote za uendeshaji zilizojitokeza hadi miezi 25 kabla ya kuanza kwa opaŕesheni nchini Malawi na kutokulipa ushuŕu wa mali ghafi zinazotumiwa kutengeneza bidhaa.

Nchi nyingi zinatoa motisha kwa kutaŕajia faida kutoka kodi ya mapato, mapato ya kubadilisha fedha za kigeni na ajiŕa. Lakini ni kwa kiasi gani faida hizo zinajikita katika ukweli

“Faida nyingi za ajiŕa ni kwa njia ya ajiŕa za mishahaŕa midogo katika kiwango ambacho kodi ya mapato haiwezi kuŕejesha kile ambacho kimepotea kupitia misamaha ya kodi,” anasema Chikusa.

Wataalam wanapendekeza kuwa nchi za Afŕika zinatakiwa kubuni mifumo yenye ufanisi ya kodi ambayo inaŕuhusu kufuatilia wakwepaji wa kodi mbali ya mipaka yao; na kuwa wabunge wanatakiwa kuwa na jukumu kubwa la kusimamia kodi.