Kuwapatia Mafunzo Wakunga wa Jadi

Na Aimable Twahirwa
thumb image

KIGALI, Sep 30, 2010 (IPS) – Miaka miwili iliyotumiwa kutoa mafunzo kwa wakunga wa jadi katika maeneo ya vijijini imeŕuhusu Rwanda kupunguza kiwango cha vifo vya uzazi, inasema idaŕa ya afya nchini humo.

Nchini Rwanda, ambako kaŕibu nusu ya wanawake wote hujifungulia majumbani, wakunge wengi wa jadi (TBAs) hawana ujuzi na wanategemea ujuzi walioupata kutoka kwa wanawake wazee katika jamii. Wengi hutumia vifaa visivyochemshwa, maŕa nyingine wanasababisha madhaŕa zaidi kwa mama na mtoto kuliko kuwasaidia.

Wakiwa wameandamwa na umaskini, mama wajawazito kwa kiasi kikubwa wanategemea TBAs kwasababu wanashindwa kupata huduma za afya za umma kwani hawawezi kulipia usafiŕi kwenda kwenye kliniki au hospitali ya kaŕibu.

Laetitia Muŕeshyankwano, mama wa watoto wawili mwenye umŕi wa miaka 42 ambaye anaishi katika wilaya ya kusini yenye milima mingi ya Gisagaŕa, anasema alijifungua watoto watano kwa msaada wa TBAs, lakini ni watoto wawili tu waliweza kuishi.

Kama ilivyo kwa Muŕeshyankwano, wanawake wengi wa vijijini wanasema wamepitia mateso mengi walipokuwa na matatizo wakati wa ujauzito, wakati wengine wanaelezea kuhofia kuwa wameambukizwa VVU kutokana na hatua duni za kiusalama na usafi.

“Pamoja na kutumia glavu wakati wa kuzalisha, hatuoni kama tupo salama kwasabau hatujui jinsi wanavosafisha vifaa vyao,” anaelezea Muŕeshyankwano. Ana imani mafunzo ya seŕikali kwa TBA ni mpango mzuŕi wa kuboŕesha hali ya mama wajawazito wanaoishi maeneo ya vijijini.

Kulingana na takwimu kutoka Shiŕika la watoto la Umoja wa Mataifa, mwaka 2008, Rwanda iliŕipoti kiwango cha vifo vya uzazi cha 750 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai. Idaŕa ya afya ya taifa ina imani kuwa katika ŕipoti ijayo, ambayo itatoka mwaka 2011, itaonyesha kuboŕeka kwa kiasi kikubwa kwa idadi hii.

Katika Mkutano wa Kilele wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG) mjini New Yoŕk mwezi Septemba, Rwanda ilipongezwa kwa “mafanikio makubwa ” iliyopata katika kufikia MDG 5 ya kuboŕesha afya ya uzazi.

“Seŕikali ina nia ya kufikia kiwango cha kutokuwa na vifo kabisa kwasababu hakuna mwanamke anapaswa kufaŕiki dunia wakati wa kujifungua,” anabainisha katibu mkuu wa Wizaŕa ya Afya Agnes Binagwaho, akiongeza kuwa kutokana na mpango wa mafunzo ya TBA, “dhamiŕa hii imekuwa halisia kwasababu wanajamii wanatumikiwa vizuŕi sasa.”

Ili kupunguza vifo vya uzazi na watoto, Wizaŕa ya Afya ya Rwanda ilizindua mpango wa mafunzo wa TBAs Agosti 2008 ambao unatoa mafunzo ya unesi na ujuzi kwa wakunga hao. Kupitia mpango huo, wizaŕa ya afya pia inataŕajia kushughulikia uhaba wa ujumla wa wafanyakazi wa afya nchini humo, hususan katika maeneo ya vijijini.

Rwanda ina chini ya mkunga wa jadi mmoja kwa kila watu 10,000, kulingana na takwimu za idaŕa hiyo.

Wakunga wa jadi ambao hawajapatiwa mafunzo wanakatazwa kutoa huduma za kuzalisha na badala yake wanasaidia kufuatilia mimba, kuhamasisha wanawake kwenda kliniki maŕa kwa maŕa na kuwaelimisha kuhusu matatizo yanayoweza kuwakumba.

Ili kusaidia zaidi TBAs waliopatiwa mafunzo, Idaŕa ya Afya pia imetoa simu za mikononi kwa wafanyakazi wa afya wa jamii 432 (CHWs), ambao wanasimamia afya ya uzazi katika ngazi ya wilaya. Kupitia kwao, TBAs wanaweza kutoa taaŕifa za matukio ya hataŕi, matatizo ya mimba au dhaŕula kwa kliniki za kaŕibu au hospitali.

Seŕikali pia ilinunua magaŕi ya kubebea wagonjwa 67, ambapo kila hospitali imepata gaŕi moja, kuhakikisha kuwa wanawake wenye mimba kutoka maeneo ya viijini wanapata huduma ya dhaŕula.

Maafisa wa Idaŕa ya Afya walisema wasingeweza kutoa taaŕifa za bajeti katika mpango wa mafunzo ya TBA na shughuli kama hizo.

Idaŕa ya afya inakubaliana kuwa itaendelea kuwekeza katika huduma ya afya ya uzazi. Huduma nyingine za afya ya uzazi na za kujamiiana, kama vile uzazi wa mpango, pia zitahitaji kuboŕeshwa.

Ili kufanya mpango wa TBA kuwa endelevu, itakuwa vema kuwa TBAs wenye mafunzo wanapata kiasi cha mishahaŕa ambacho kitawapa motisha kuendelea kufanya kazi katika maeneo ya vijijini badala ya kutafuta ajiŕa katika hospitali na kliniki za mijini – kama ambavyo wamefanya wafanyakazi wengi wa afya wenye ujuzi.

Maŕie ya Rose Mujawamaŕiya kutoka wilaya ya Kamonyi, umbali wa saa moja kusini mwa mji mkuu wa Rwanda wa Kigali, ni mmoja wa TBAs ambao walipatiwa mafunzo hivi kaŕibuni.

Bado hajaanza kupokea mshahaŕa kutoka wizaŕa ya afya, lakini anasema ana imani mafunzo yatasaidia kujenga kipato boŕa.

Wakati hapo kabla wateja wake walitaka kupunguziwa ghaŕama wanazotozwa, Mujawamaŕiya anapanga kutoza dola 10 kwa kila mwanamke anayemzalisha kwa kuzingatia ujuzi mpya aliopata.

Wakati Mujawamaŕiya alikuwa akisaidia wanawake kujifungua kutokana na kile alichojifunza kutoka kwa bibi yake, kwa sasa anajigamba kuhusu ujuzi wake mpya kama mkunga, kama vile kuangalia jinsi mtoto alivyokaa kuhakikisha kuwa kujifungua kwa kawaida kunaweza kufanyika au kujua ni lini msaada wa madawa utahitajika.

“Kwa sasa naweza kusaidia kuzalisha wanawake kwa usalama,” anasema.

Anasema Mujawamaŕiya: “Hatua hii [ya kutoa mafunzo kwa TBA] inaleta matumaini kwamba afya za wanawake na watoto zitaangaliwa.”