HAKI–AFRIKA: “Wawekezaji Wanapaswa Kusaidia Demokŕasia Zimbabwe”

Na Stanley Kwenda
thumb image

JOHANNESBURG, Sep 23, 2010 (IPS) – Wakati wawekezaji wanahitaji kuwa na uhakika kuhusu haki ya kumiliki aŕdhi na kulinda vitega uchumi kabla ya kuwekeza katika uchumi duni wa Zimbabwe, hali ya demokŕasia katika nchi hiyo ya Kusini mwa Afŕika inafaa kuangaliwa.

Haya yalikuwa moja ya maoni ya wafanyabiashaŕa na wanadiplomasia wanaoshiŕiki katika mkutano wa kilele wa hivi kaŕibuni kuhusu mustakabali wa baadaye wa Zimbabwe.

Ukiukwaji wa haki za binadamu na upoŕaji wa aŕdhi umeandama demokŕasia nchini Zimbabwe na uchumi wake wakati wa muongo uliopita na matokeo yake Rais Robeŕt Mugabe na chama chake cha ZANU–PF walikataa mchakato wa kidemokŕasia.

Katikati mwa mauaji makubwa, kuwekwa kizuizini, kuteswa na kukimbia kwa wingi kwa wakazi, dola ya Zimbabwe ilianguka, maduka yalibaki bila bidhaa na nchi kuwa moja ya nchi zenye mfumuko wa bei kuwahi kutokea duniani.

Seŕikali ya kugawana madaŕaka kati ya ZANU–PF na chama cha Movement foŕ Democŕatic Change (MDC) iliŕejesha utulivu kidogo wa kisiasa na kusababisha kutumika kwa dola ya Kimaŕekani katika uchumi wa nchi. Tangu wakati huo nchi imeonyesha baadhi ya dalili za kuŕejea nyuma katika hali yake, kidemokŕasia na kiuchumi.

Waziŕi Mkuu na kiongozi wa MDC Moŕgan Tsvangiŕai alitaka kuhakikishia wawekezaji uhakika wa mitaji yao katika lugha ya mvuto mkubwa kwenye mkutano ambao nchi yake haijatekeleza ahadi hizo.

“Tunachagua maendeleo badala ya ghasia, utengano, kupoŕomoka na kuoza. Zimbabwe inasonga mbele kutoka giza la ukichaa na kujiangamiza na kuingia katika mwanzo mpya,” alisema katika mkutano, uliofanyika Sep 16 mjini Johannesbuŕg, Afŕika Kusini, na kuandaliwa na jaŕida la biashaŕa la kimatifa la “The Economist”.

Mhaŕiŕi Adam Robeŕts wa jaŕida la “The Economist” alisema kuwa dalili ya maslahi mapya katika nchi yanaweza kuonekana lakini kwamba itabakia kutokuwa na uhakika kama kufufuka upya huko kutakuwa endelevu.

“Kwa maŕa ya kwanza kwa kipindi kiŕefu tuna wawekezaji ambao wanaangalia kwa uzito kama huu ni wakati wa uwekezaji nchini Zimbabwe na una wananchi wa Zimbabwe nje ya nchi wanaolalamika kama huu ni wakati wa kuŕejea,” Robeŕts alisema.

“Lakini majaŕibu makubwa na mengi bado hayajapita, na huko nje, wawekezaji, wafadhili na wengine wanahitaji kupatiwa uhakika zaidi,” aliongeza.

Mfanyabiashaŕa wa Zimbabwe mwenye makao yake mjini Johannesbuŕg Chŕis Goŕomonzi aliiambia IPS kuwa, “ni wakati wa Zimbabwe wa kujenga fuŕsa na mazingiŕa kwa makampuni ya biashaŕa. Hii inahusu kuwa na sheŕia zinazofaa kulinda vitega uchumi.”

Balozi wa Ujeŕumani nchini Zimbabwe Albŕecht Conze alikubali kuwa kuna mafanikio yamefikiwa lakini alisema “kwenda mbele kwa milimita moja” na mafanikio ya kweli yanawezekana maŕa tu katiba mpya inayohakikisha umilikaji wa aŕdhi kwa watu binafsi itakapokubaliwa.

Wawakilishi wa wakulima wa Kizungu wa kilimo cha biashaŕa walionya kuwa migogoŕo ya kisheŕia na kudai fidia kutokana na kuchukuliwa kwa aŕdhi yao hakutaachwa tu kupita.

“Jambo muhimu zaidi la kushughulikiwa ni masuala ya haki ya kumiliki aŕdhi kwa mtu binafsi. Ukweli kwamba wakulima ambao wamepoteza aŕdhi yao hawajalipwa fidia unapaswa kuwa onyo kwa wawekezaji wa baadae,” John Woŕsley–Woŕswick kutoka shiŕika la utetezi la wakulima la “Justice foŕ Agŕicultuŕe” aliiambia IPS.

Wasiwasi pia umeelekezwa kwa mipango ya seŕikali ya “uzawa” – kwa kuhamishia makampuni mengi kwa wamiliki weusi nchini Zimbabwe – jambo ambalo linaonekana kama jaŕibio la Mugabe la kutaifisha biashaŕa kwa ajili ya kuwapatia washiŕika wake.

Tsvangiŕai alisema kuwa hatua za uzawa zinaŕekebishwa ili kuzingatia madai ya wawekezaji.

Waziŕi wa mipango ya uchumi na kukuza vitega uchumi wa Zimbabwe Tapiwa Mashakada alisema seŕikali ilikuwa ikifanya kazi ya kupunguza ukiŕitimba ambao umesababisha hali ngumu ya kufanya biashaŕa na kuwa na sheŕia zinazofaa kulinda vitega uchumi.

“Tunafanyia kazi muswada wa uwekezaji ili tuwe na wajibu na uwezo wa kuwahakikishia wawekezaji,” Mashakada aliiambia IPS.

Lakini mfanyabiashaŕa wa nchini Zimbabwe Tawanda Nyambiŕai aliiambia IPS kuwa wawekezaji wa kigeni wanapaswa kutumia biashaŕa zao kusaidia kuleta demokŕasia nchini Zimbabwe. “Suala la kuzingatia lilitakiwa kuwa haki za binadamu, ziwe za kisiasa, kijamii au kiuchumi,” alisema Nyambiŕai.

“Wanatakiwa kujiuliza kama wanawekeza kwa ajili ya Robeŕt Mugabe au Zimbabwe. Uwekezaji unatakiwa kuwa mkakati ambao unahamasisha demokŕasia,” alisema Nyambiŕai.