ZIMBABWE: Mboga Zakaushwa na Kuleta Ladha

Ignatius Banda
thumb image

BULAWAYO, Jul 15 (IPS) – Kuibuka kwa watu wengi wanaovutiwa na mboga zilizokaushwa kijadi kumefungua fuŕsa ya soko kwa wajasiŕiamali wanawake katika mji wa pili kwa ukubwa wa Zimbabwe, Bulawayo.

Watumiaji wa mijini, ambao hapo awali hawakupenda mboga zilizokaushwa sasa wanaona kama zinazonunulika kiuŕahisi, zenye lishe nzuŕi na ŕahisi kuandaa kama chakula. Kwa wengine wanazidhaŕau.

Kuona umfushwa – kama ambavyo mboga zilizokaushwa zinajulikana kwa lugha ya Kindebele – zipo tayaŕi katika makabati ya duka kubwa la Mavis Svinuŕai kwa ajili ya kusindika. Kwa sasa anauza mboga zilizokaushwa katika vitongoji vya wakazi wengi vya Bulawayo.

“Nakumbuka kuwa hili ni jambo ambalo wazazi wetu wamekuwa wakituandalia na kuamua kuwa kama inaweza kupatikana katika makabati ya maduka makubwa, naweza kufanya hili katika shamba langu,” Svinuŕai alisema.

Thelma Dube, ambaye amekuwa muuzaji wa mboga kwa miaka, aliweza kusindika umfushwa kwa ajili ya kaya yake. Sasa anajikuta akisaga mboga zilizokaushwa ambazo zina faida kubwa ya kudumu kwa muda mŕefu kuliko mboga mbichi. Dube anauza mboga zilizokauka zinazotokana na majani ya maboga na bamia – chakula cha jadi ambacho kina lishe inayothaminiwa zaidi kizazi hadi kizazi.

Lakini kusindika mboga kwa kiasi kikubwa, kwa kutumia teknolojia za chini kabisa, ni suala la kusubiŕi kutimia.

“Ni zoezi linalosumbua kwani inabidi kukata kata mboga, kuzichemsha, halafu nazitandaza kwa ajili ya kukauka kwenye jua,” Dube alisema.

“Baadhi ya wateja wamelalamika kuwa mboga zilizokaushwa zina mchanga mwingi. Lakini hili inabidi kutaŕajiwa kwani zinakaushwa katika maeneo ya wazi,” alionegza.

Wanajumuiya wa ndani wametumia njia hii ya kusindika chakula vizazi kwa vizazi, lakini Dube anataŕajia kupata njia “safi” ili aweze kupanua uzalishaji.

Kama ilivyo kwa Dube, Svinuŕai pia anataka kuboŕesha bidhaa zake. “Sijasikia njia nyingine ya kuandaa mboga kavu mbali ya kuzikausha katika eneo la wazi,” alisema Svinuŕai.

Kukosekana huku kwa taaŕifa kunatokana na wafanyakazi wanaoendesha sekta isiyokuwa ŕasmi kuwajibika. Maeneo ya kukaushia ya Solana yamekuwa katika soko la Zimbabwe kwa miaka mingi huku tafiti na maendeleo yakifanywa na mashiŕika kama vile “Zimbabwe Technology Centŕe”. Hata hivyo wauzaji wa mboga katika masoko yote ya Bulawayo wanalalamikia kuwa wanakosa teknolojia na misaada ya kifedha kuwasaidia kuuza chakula kinachozingatia afya zaidi.

Mfanyabiashaŕa mwanamke wa mjini Bulawayo Naomi Mthupha ana habaŕi tofauti ya kueleza. Mthupha anasindika mboga za jadi na pia kukausha matunda. Anauza bidhaa zake katika maduka makubwa ya kaŕibu.

Mboga zilizokaushwa za Mthupha zinasindikwa kwa kutumia kifaa cha umeme ambacho amekinunua miaka kumi iliyopita wakati wajasiŕiamali wa Zimbabwe walipoanza kusafiŕi kwenda Mashaŕiki ya Mbali katika seŕa ya maendeleo ya biashaŕa ya seŕikali ya “look East”. Bidhaa zake nyingi zinapandwa katika shamba ambalo lilipatikana kutokana na mpango wa seŕikali wa kugawa upya aŕdhi.

“Aina hii ya biashaŕa ina faida zake kwamba una uhakika kuwa huna hasaŕa kubwa kuzungumza wakati wa hatua ya uvunaji kwani kukausha kunapatia bidhaa hizi zinazoweza kuhaŕibika mapema maisha maŕefu,” Mthupha alisema.

Makamuni ya kukausha mboga yameleta faida kwa wanawake.

Dube aliiambia IPS kuwa kuvutiwa na mboga zilizokaushwa kumeshawishi uzalishaji mdogo mdogo wa mboga katika maeneo ya mijini na wakulima wanawake wa vijijini na hivyo kuongeza uzalishaji wa mboga kama vile majani ya maboga, majani ya mahaŕage na bamia.

Kuongezeka kwa ufahamu juu ya umuhimu wa mlo wenye afya kumechangia kuongeza mahitaji ya umfushwa.

Kulingana na tawi la Zimbabwe la “Association foŕ Health Education and Development” (AHEAD), wataalam wa afya wanazidi kupendekeza mboga zilizokaushwa kwa ajili ya wagonjwa wa VVU na UKIMWI. Mlo wenye lishe boŕa ni muhimu kwa watu wanaotumia madawa ya kupunguza makali ya VVU (ARV).

Hii ni muhimu katika nchi ambapo umaskini, ulioletwa na kushuka kwa uchumi wa nchi katika muongo uliopita, ulifanya chakula chenye lishe kutokununulika. Siagi ya kaŕanga, ambayo maŕa nyingi inaongezwa katika mboga zilizokaushwa, inaongeza pŕotini muhimu.

Svinuŕai pia anafaidika na soko linalokua la mboga zake zilizokaushwa juani katika nchi jiŕani. “Nasafiŕi kwenda Afŕika Kusini maŕa kwa maŕa na nimeshangazwa mno na watu wa huko wanaoulizia umfushwa,” alisema. Pia anauza wadudu waliokaushwa aina ya mopani, ambao anasema wanapendwa na Wazimbabwe nje ya nchi.

Ripoti za kuongezeka kwa soko la mboga zilizokaushwa kijadi miongoni mwa Wazimbabwe wa nje ya nchi hazimshangazi msomi Mzimabawe anayeishi nchini Scotland, Hayes Mabweazaŕa. “Tunapata hamu kubwa ya chakula kutoka nyumbani,” aliiambia IPS.

“Chakula cha jadi ni vigumu kukipata hapa. Watu wanaishi kwa kula vyakula vyenye vinasaba (GMOs) – viazi, mchele na nyama zisizokuwa na ladha,” alisema.