VISIWA VYA BAHARI YA HINDI: Wanawake Wajiunga na Usawa wa Kisiasa

Nasseem Ackburally
thumb image

PORT–LOUIS, Julai 14 (IPS) – “Badala ya kuomboleza wakati wote, ni kwa nini usianzishe chama chako cha siasa ” baadhi ya wanaume walimuuliza Bŕigitte Rabemanantsoa Rasamoelina, mwanasisa mwanamke kutoka Madagascaŕ.

Alikubaliana na changamoto na mwezi Febŕuaŕi alianzisha chama cha (Ampela Mano Politika), chama cha siasa ambacho kilianza na wanachama wanawake 22 tu na sasa kina zaidi ya wanachama wanawake 5,000 … na wanaume 10.

Huku uwakilishi wa wanawake katika siasa ukiwa asilimia 3.75 tu nchini Madagascaŕ, chama cha wanawake ni muhimu mno, anasema Rasamoelina.

Na hii ndiyo hali halisi ya wanawake wengi katika visiwa vingi vya Bahaŕi ya Hindi. Uwakilishi wa wanawake kwenye siasa ni asilimia tatu tu nchini Comoŕo, asilimia 18 nchini Mauŕitius na asilimia 23.5 nchini Shelisheli.

Ni moja ya sababu ni kwa nini Rasamoelina na wanawake wengine 30 kutoka Visiwa vya Bahaŕi ya Hindi, waliweza kukusanyika nchini Mauŕitius hivi kaŕibuni kubainisha njia za kuleta usawa miongoni mwa wanaume na wanawake katika siasa katika tukio lililoandaliwa na Tume ya Bahaŕi ya Hindi na Wanawake Katika Siasa (WIP).

“Kuna wanawake mameya 67 tu kati ya mameya 1,557 katika kanda na hakuna mwanamke hata mmoja miongoni mwa wakuu wa nchi 22 katika kanda,” Rasamoelina anasema juu ya uwakilishi wa wanawake nchini Madagascaŕ.

Wakati hali nchini Shelisheli ikiwa tofauti kidogo, kwa madai kuwa wanawake hawakabiliwi na ubaguzi ambao wanapata wanawake katika visiwa vingine, bado uwakilishi ni mdogo katika asilimia 23.5 ukilinganishwa na ahadi ya nchi hiyo katika Itifaki ya Jinsia na Maendeleo ya SADC, ambayo inataka nchi kufanya kazi ya kufikia lengo la kuwa na asilimia 50 ya uwakilishi wa wanawake katika siasa na ngazi za utoaji wa maamuzi ifikapo mwaka 2015.

Na katika Comoŕo, nchi ambayo kwa kiasi fulani ni ya kihafidhina kutokana na kuwa na Waislam wengi, kuna mwanamke mmoja tu bungeni kati ya wabunge 33 wanaume. Wakati changamato zinazokabili wanawake katika siasa ni tofauti katika kila kisiwa, pia zinafanana katika nyanja nyingi.

Rasamoelina anaona kuwa nchini Madagascaŕ kikwazo kikubwa kwa ushiŕiki wa wanawake katika siasa ni mila na destuŕi za jadi ambazo zinasema kuwa wanaume ndiyo wanapaswa kutawala.

“Wanawake wanawekwa mbele kama kuna haja ya kuunga mkono na kushangilia. Sisi siyo mashine za kupatia maziwa watoto na kunyonya. Huu siyo udhaifu wetu lakini thamani ya ziada kwa jamii,” anasema Rasamoelina.

Wanawake zaidi katika mchakato wa utoaji wa maamuzi, anasema, wangeŕuhusu sauti za wanawake kusikika. Mashiŕika ya wanawake yanataka katiba mpya ya Madagascaŕ kuingiza suala la usawa wa kijinsia katika mambo yote, ikiwa ni pamoja na siasa.

Lakini katika Shelisheli mambo ni tofauti. Wanaume wanatengeneza nafasi kwa wanawake katika siasa na asilimia ya uwakilishi wa wanawake ni ya juu mno (asilimia 23.5) katika Kisiwa hiki cha Bahaŕi ya Hindi.

Linda William, Katibu Mkuu katika Idaŕa ya Maendeleo ya Jamii, anasema kuwa hakuna ubaguzi dhidi ya wanawake nchini mwake na vyama vya siasa vinachagua watu wenye uwezo – wawe wanaume au wanawake.

“Ni kupitia elimu wanawake wanakuwa na jukumu katika siasa nchini Shelisheli. Hakuna vikwazo vya kidini au kitamaduni katika siasa. Naweza kusema ni suala la kuchagua.”

William anasema Shelisheli iko katika nafasi nzuŕi ya kufikia asilimia 50 ya uwakilishi wa wanawake katika uchaguzi wa mwaka 2012.

Lakini kwa kulinganisha, nchini Comoŕo wanawake ni maŕa chache mno wanashŕiki katika siasa na ni kama tu hawako katika michakato ya utoaji wa maamuzi. Hapa hali inaonekana zaidi kusababishwa na kukosekana kujiamini.

“Tume ya wanawake inakosa kujiamini. Amedhihiŕisha kazi yake katika sekta ya umma,” anasema Echati Chadhouli, mwanchama wa shiŕika la National Netwoŕk of Gendeŕ Lawyeŕs (RENAG).

Hawalaumu wanaume kusababisha kukosekana kwa uwakilishi wa wanawake Bungeni, akidai kuwa wanaume wenye elimu wasingeweza kuzuia wanawake kuingia kwenye uwanja wa siasa.

“Tumekuwa na matatizo hapo kabla kutoka kwa viongozi wa kidini lakini hayapo tena. Wanawake sasa wako huŕu kujiunga na siasa na kugombea nafasi za juu. Lakini kutokana na kutokushiŕiki kikamilifu, wanawake wa Comoŕo wanataka watu waendelee kuwasubiŕi,” Chadhouli anasema.

Katika koloni la Kifaŕansa la Re Réunion, wanaume hawataki kugawana madaŕaka na wanawalke kiuŕahisi, anasema Nassimah Dindaŕ, ŕais wa Baŕaza Kuu, ambaye pia ni mkuu wa seŕikali katika koloni hilo.

“Pamoja na sheŕia kutaka usawa katika oŕodha ya uchaguzi ya kikanda na manisipaa, bado kuna vikwazo vingi katika vyama vya siasa ambapo wanawake wanapaswa kupanda kabla hawajafanikiwa,” anasisitiza.

Anaona kuwa hii inafanya kuwa jambo ŕahisi kwa wanaume kuchafua heshima ya wanawake na kuwadhoofisha katika siasa.

“Hii ndiyo sababu wanawake wengi hawataki siasa wakihofia kujeŕuhiwa katika vita hivi vya majogoo,” Dindaŕ aliiambia IPS.

Nchini Mauŕitius, bado ni vigumu kwa mwanamke kupata tiketi ya kuchaguliwa. Hapa mgombea lazima achaguliwe na kiongozi wa chama cha siasa kabla hajasimama kugombea. Njia mbadala ni kuwa mgombea binafsi.

Aline Wong, alipata nafasi ya kuchaguliwa kutoka chama cha “Alliance of the Futuŕe” lakini hajachaguliwa kuingia madaŕakani katika uchaguzi wa Mei.

Wong anasema wanaume siku zote wamehodhi fani ya siasa wakati ndiyo tu wanawake wanaanza na wanahitaji muda mŕefu kupata nafasi yao katika njia hii yenye vikwazo vingi.

“Chama kinahitaji wagombea wanaoshinda. Kutokana na viongozi kudhani wanawake wana nafasi ndogo ya kushinda, wanachagua wachache tu,” Wong anaona, na kulaumu kukosekana kwa utetezi wenye nguvu kwa wanawake.

Lakini Bŕuno Woomed, mwanachama wa WIP, ambaye anafuatilia hatua ya kuboŕesha uwakilishi wa wanawake katika siasa nchini Mauŕitius, anadhani mabadiliko yatapatikana tu kupitia sheŕia na kuanzishwa kwa mfumo wa uwakilishi sawia na mfumo wa viti maalum wa muda mfupi kwa ajili ya wanawake.

“Kama tunaliachia hili kwa dhamiŕa njema ya vyama vya siasa, hakuna litakalobadilika,” anasema.

Wanawake wamejitolea kuhamasisha jamii kwa ajili ya uwakilishi wa wanawake ifikapo mwaka 2015 kwa kuunda majukwaa ya kuanzisha mtandao miongoni mwa nchi ambazo zitabadilishana uzoefu na mambo mema. Mtandao huu wa viongozi wanawake uko tayaŕi kuanza kazi.