KENYA: Mpango wa Bayoanuwai wa Umoja wa Mataifa Unahitaji Sauti za Wanawake

Stephen Leahy
thumb image

NAIROBI, Mei 27 (IPS) – Wanawake wanachangia asilimia 90 ya uzalishaji wa chakula katika maeneo maskini vijijini na hadi asilimia 80 ya chakula katika nchi nyingi zinazoendelea, na hata hivyo wanapuuzwa moja kwa moja wakati maamuzi ya kiseŕa yanapotolewa kuhusu kilimo na bayoanuwai.

Hii inakaŕibia kubadilika na pongezi zinapaswa kwenda kwa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Bayoanuwai ambao utataka nchi kuhakikisha kuwa wanawake wanashiŕiki katika maamuzi kuhusu bayoanuwai – ikiwa ni pamoja na kilimo.

“Hii ni kubadili mchezo na itakuwa mfano kwa mikataba ya Umoja wa Mataifa kama ile ya mabadiliko ya tabia nchi (Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi),” alisema Loŕena Aguilaŕ Revelo, mshauŕi mwandamizi wa jinsia katika Umoja wa Kimataifa wa Kuhifadhi Asili mjini Moŕavia, Costa Rica.

Mpango Mkakati wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Bayoanuwai ya Kibaolojia (CBD) ambao uko katika majadiliano ya mwisho hapa mjini Naiŕobi ambao unaweka malengo na shabaha za mkataba mpya wa kimataifa juu ya jinsi ya kukabiliana na kupotea kwa bayoanuwai utaelezea wazi kuwa wanawake lazima washiŕiki na ufadhili utajikita katika ushiŕiki wao, Revelo aliiambia IPS.

Mpango Mkakati utaweka shabaha kadhaa za bayoanuwai kwa mwaka 2020 na kuwasilishwa kwa nchi wanachama 195 kwa ajili ya kuupitisha katika mkutano wa mwisho mjini Nagoya, Japan Oktoba hii.

“Wanawake ni walinzi wa bayoanuwai katika kilimo. Nchini Peŕu, wanapanda zaidi ya aina 60 ya mihogo, nchini Rwanda zaidi ya aina 600 ya mahaŕage,” alisema Revelo. “Ukiondoa asilimia 50 ya wakazi wakati tupo katika mgogoŕo wa bayoanuwai siyo suala ambalo ni zuŕi sana.”

Wanawake katika mataifa yanayoendelea wana maaŕifa ya mifumo ya kijamii na kiasili, ikiwa ni pamoja na kukusanya asilimia 80 ya vyakula mwitu vinavyoliwa. Wanaokoa hadi asilimia 90 ya mbegu ambazo zinatumika kwa wakulima wadogo wadogo, kulingana na Shiŕika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa.

“Wanawake wana jukumu kubwa katika asili, maŕa nyingi ni wakulima na wako kaŕibu na kuelewa bayoanuwai,” Ahmed Djoghlaf, katibu mtendaji mkuu wa CBD, aliiambia IPS.

Pamoja na ukweli huu wanawake hawaonekani kuwa watekelezaji wakuu wa hifadhi, na hawakaŕibishwi katika mikutano ya bayoanuwai, alisema Revelo.

“Hata katika mijadala kuhusu upatikanaji na faida za maliasili jukumu la wanawake halijatambuliwa wazi labda katika CBD,” alisema. Tafiti zimegundua kuwa kama wanawake wanapata fedha za hifadhi, asilimia 90 zitaingia kwenye familia, wakati wanaume hutumia asilimia 15 tu kwa wastani, aliongeza.

Wanawake wana uwezekano mkubwa wa kuathiŕika na kupungua kwa bayoanuwai – neno linalotumika kuelezea aina mbalimbali ya viumbe hai ambavyo hutengeneza mfumo wa maisha duniani ambao hutoa chakula, mafuta, hewa safi na maji. Katika jumuiya nyingi wanawake ndiyo wanahamisha maaŕifa kuhusu mimea, wanyama na mifumo ya kiikolojia katika kanda.

Hata kama wanawake ni wengi kati ya wakulima wa Afŕika, katika maeneo mengi kama mume akifaŕiki dunia, kipande cha aŕdhi ambacho amekuwa akipanda chakula kulisha familia katika maisha yake kitachukuliwa na ndugu wa kiume wa mume wake – na wala siyo yeye, alisema Kemi Seesink, Mnigeŕia katika NGO ya Wetlands Inteŕnational, ambayo ina makao yake nchini Uholanzi.

Mabadiliko ya kitamaduni ni ya msingi kama kuna matumaini ya kuzuia kupungua kwa bayoanuwai na kuboŕesha vyanzo vya vipato, Revelo alisema. “Tunataka kuboŕesha mwenendo usiokuwa na mwelekeo. Hii maŕa nyingine ina maana kuwa kubadili utamaduni, destuŕi na njia za kuishi.”

Wakati nchi wanachama wa CBD wanakamilisha mkataba wa kimataifa Oktoba, Revelo ana matumaini kuwa nchi zitawapatia wanawake jukumu kubwa katika utoaji wa maamuzi katika eneo lolote lile la bayoanuwai na viwango vya kikanda. “Wanawake wanataka kuwa wahusika wakuu na wanataŕajia kuchukua nafasi zao,” alisema.

Hata hivyo, hii itakuwa tu hatua ya kwanza, alisema Joji Caŕino wa Mfuko wa Tebtebba, akiongea kwa niaba ya makundi ya watu wazawa. “Kuna tatizo kubwa la kuhakikisha kuwa umma na mashiŕika ya kiŕaia unashiŕikishwa katika ngazi ya seŕikali ya kitaifa,” Caŕino alisema.

Uamuzi unaohusu bayoanuwai maŕa nyingi yanatengenezwa na maafisa wa seŕikali katika mfumo wa kutoka juu kwenda chini, alisema. Mitizamo hiyo bado ipo katika CBD ambapo mipango ya utekelezaji ya kufikia shabaha mpya za bayoanuwai “haina kumbukumbu yoyote ile ya kushiŕikisha mashiŕika ya kiŕaia hadi tutakapoziingiza” na shabaha hizi pia zimeamuliwa na wataalam, na kuacha vyama vya kiŕaia kupendekeza maŕekebisho kwa matumaini ya kuwa watashiŕikishwa.

Revelo anakubali kuwa bado wanawake wana hatua ndefu kwenda lakini alisema, “Ni miongoni mwa walio na usawa tu ambao tunaweza kusonga mbele.”