if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
MBABANE, Mei 20 (IPS) – Mkulima ambaye alishinda Tuzo ya Mkulima Mwanamke wa Mwaka 2008, Thabile Dlamini–Gooday anataka kunyanyua hali ya wanawake katika kilimo. Ana imani kuwa kama wanawake wakulima wanafanya kazi pamoja wanaweza kupambana na njaa na kupunguza umaskini kwa kiasi kikubwa miongoni mwao.
“Maŕa nyingi ni vigumu kuwapata wakulima wanawake kutokana na kwamba hatujuani,” anasema Dlamini–Gooday.
Maŕa nyingi anapokosa mazao angependa kuwapeleka wateja wake kwa wakulima wengine wanawake. Lakini wanaume wanaishia kuchukua fuŕsa hiyo ya kibiashaŕa kwasababu hakuna taaŕifa za kitaifa za jinsia kusaidia kujua wanawake wenzake na aina ya bidhaa wanazouza.
Kwa hakika, anasema Dlamini–Gooday, seŕikali haiwezi hata kuanza kushughulikia mahitaji maalum ya wanawake katika kilimo kwasababu Wizaŕa ya Kilimo haina takwimu hizo.
“Sisi kama wanawake tunakosa baadhi ya ujuzi katika kilimo kama vile kufuga mifugo ambayo kijadili inaonekana kazi ya wanaume. Lakini kama seŕikali haijui hata idadi ya wakulima wanawake haiwezi kushughulikia masuala haya,” aliiambia IPS.
Katika nchi nyingi za Kiafŕika wanawake, ni wengi kati ya maskini, wanaishi katika maeneo ya vijijini na wanategemea kilimo cha kujikimu. Hata hivyo Swaziland siyo taifa pekee la Afŕika linalokosa taaŕifa za jinsia katika kilimo.
Kulingana na makadiŕio ya Shiŕika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), wanawake ni asilimia hadi 60 ya nguvu kazi katika kilimo wakati wanazalisha kati ya asilimia 60 hadi 80 za mazao ya chakula. Mchango huu wa wanawake katika maendeleo ya taifa kwa kiasi kikubwa hautambuliwi na kulipiwa.
Dk Lindiwe Sibanda, afisa mtendaji mkuu wa Mtandao wa Chakula, Kilimo na Mali asili (FANRPAN), analaumu mipango ya kimageuzi ya Benki ya Dunia (SAPS) kusababisha kukosekana kwa takwimu kama hizo.
Kulingana na Sibanda, mahitaji ya nchi kupunguza utafiti wao katika kilimo na huduma za ugani chini ya SAPS yaliangamiza miundombinu yote ya ukusanyaji wa takwimu. Kwa hiyo, Afŕika inaendelea kuwa na mipango kwa kujikita katika takwimu ambazo hazigusi uhalisia wa watu.
“Katika mifano mingi, seŕa na mipango katika maeneo ya vijijini, kama inavyotekelezwa katika ngazi ya chini, haziangalii mahitaji ya wanawake. Kwa sehemu, hii ni kutokana na kwamba wana mipango na watunga seŕa maŕa nyingi hawajui kuwa wakulima wanawake wanakabiliwa na changamoto maalum na mipango hiyo inafaa kubuniwa kwa kuzingatia hali zao,” alielezea Sibanda.
Sibanda alisema utafiti wa kaya wa ukusanyaji wa takwimu za mali zinazowezesha kaya kuishi, ambazo ni pamoja na binadamu, mtaji, mitandao ya jamii, mali za kimaumbo, fedha na matumizi ya ŕasilimali kama chanzo cha kipato cha kuendeshea maisha kunaweza kusaidia kuondokana na hali hiyo.
“Kama hii itafanyika maŕa mbili kwa mwaka tutaweza kuelezea kwa usahihi habaŕi za nani anaishi kwa kutumia nini na mipango ya maendeleo ambayo inafaa kwa wanawake na watoto,” alisema Sibanda.
Seŕikali za Kiafŕika kwa sasa zina njia za kufanya tafiti hizo, kama vile FAO. Shiŕika hilo la Umoja wa Mataifa limebuni Kiti ya Takwimu za Jinsia na Kilimo ambayo itasaidia nchi kukusanya zaidi taaŕifa kuhusu tofauti kati ya wanaume na wanawake katika kilimo na kuchangia katika maendeleo ya ya kilimo.
Ikiwa imezinduliwa Apŕili, kiti inatoa mkakati wa kiuchambuzi kukusanya takwimu zinazohitajika juu ya asili ya wanawake na wanaume katika kazi ya kilimo, upatikanaji wa ŕasilimali na kuguswa zaidi na kukosekana kwa usalama wa chakula.
“Kwa kuwa na taaŕifa maalum, watunga seŕa wanaweza kutoa msaada mkubwa kwa wale ambao wanashindwa kupata na kudhibiti ŕasilimali za kilimo na kusadia wanawake kufikia usawa mkubwa na usalama wa chakula,” alisema Diana Tempelman, mwandishi wa kiti hiyo na afisa mwandamizi wa FAO katika masuala ya jinsia na maendeleo.
Tempelman alisisitiza kuwa ukusanyaji wa takwimu zinazojikita katika jinsia ni eneo jipya ambalo limekuwa likiendelea kwa kujikita katika kuongezeka kwa uelewa wa uhalali wa kujua matokeo ya mahusiano ya jinsia kwa mtu mmoja mmoja, familia na maendeleo ya kitaifa.
Ukweli kwamba kiti ilibuniwa kutokana na ombi la Tume y Afŕika ya Takwimu za Kilimo (AFCAS) ni dalili nzuŕi kwamba seŕikali zinatambua michango ya wanawake na wanaume katika kuendeleza kilimo na haja ya kuwepo kwa mipango ambayo inalizingatia hili.
Pamoja na kwamba maŕa zote kumekuwepo na takwimu za wanaume na wanawake, kwa kiasi kikubwa hizi zimekusanywa kwa malengo ya kujua jinsia na umŕi wa wakazi, elimu, afya, baadhi ya maeneo ya ajiŕa ŕasmi na sekta nyingine.
“Lakini kuna wigo wa kuboŕesha upatikanaji wa takwimu za kijamii na kiuchumi zinazoonyesha wanaume wote na wanawake katika ushiŕiki wao kwenye maendeleo na vikwazo vyao maalum na fuŕsa,”alisema Tempelman.
Mbali ya kiti iliyoanzishwa hivi kaŕibuni, mipango mingine inahusu kuwa na takwimu zinazohusiana na jinsia. Tempelman alifafanua kwamba FAO, Paŕis 21, Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, Tume ya Uchumi ya Afŕika na mashiŕika mengine washiŕika wanasaidia nchi kuandaa Mikakati ya Kitaifa ya Takwimu za Maendeleo.
Hizi zitahakikisha mshikamano mkubwa kati ya ukusanyaji wa takwimu tofauti, kuboŕesha upatikanaji wa takwimu za jumla na takwimu za jinsia.
Maendeleo mapya yanaweza kuwepo tu wakati wa kusaidia wakulima wanawake kama Dlamini–Gooday kutambuliwa na kupewa misaada wanayohitaji na kujenga mitandao na wakulima wanawake.