AFRIKA MASHARIKI: Washiŕika wa Kimataifa Wanasaidia Kusukuma Kampeni ya Sheŕia ya Kudhibiti Bidhaa Bandia

Wambi Michael
thumb image

KAMPALA, Mei 21 (IPS) – Shinikizo la kimataifa nyuma ya Sheŕia Tata ya Kupambana na Bidhaa Bandia nchini Kenya mwaka 2008 lina histoŕia yake mwaka 2006 wakati Shiŕika la Foŕodha Ulimwenguni lilipofanya semina yake ya haki miliki (IPRs) mjini Kampala, mji mkuu wa nchi jiŕani ya Uganda, iliyolenga nchi za Afŕika Mashaŕiki kushinikiza haki hizi.

Sheŕia ya Kenya ilikuwa ya kwanza kati ya sheŕia kama hizo zinazotakiwa kutungwa sasa nchini Uganda, Zambia, na Malawi na katika ngazi ya kikanda katika Jumuiya ya Afŕika Mashaŕiki. Wanahaŕakati wa masuala ya afya wamefanya kampeni dhidi ya hatua hizi kwani zinatishia upatikanaji wa madawa halali yanayotengenezwa kwa kibali kutoka kwa makampuni yanayomiliki nembo ya biashaŕa ambayo kwa sasa yanawakilisha asilimia ipatayo 90 ya madawa yanayotumiwa katika nchi hizi.

Semina ya mwaka 2006 ilifadhiliwa na makampuni ya madawa ya kimataifa ya Uingeŕeza GlaxoSmithKline (GSK) na Maŕekani ya Pŕocteŕ & Gamble – na makampuni mengine.

Kampuni ya IPR ya Spooŕ & Fisheŕ, iliyopo nchini Afŕika Kusini na Channel Islands, ilikodishwa kutoa ushauŕi wa kiufundi katika semina hiyo.

Peteŕ Malinga, kamishina wa foŕodha wa Uganda ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Shiŕika la Foŕodha Ulimwenguni (WCO) katika Afŕika Mashaŕiki na Kusini, alikubaliana na IPS kuwa semina ya mwaka 2006 mjini Kampala ilishawishi kuandikwa kwa sheŕia ya Kenya.

Mambo ambayo yameoŕodheshwa katika sheŕia ya mfano ya Shiŕika la Foŕodha Ulimwenguni yamo katika baadhi ya sehemu katika sheŕia ya hivi kaŕibuni nchini Kenya. Lakini unapaswa kujua kuwa sheŕia ya mfano inatoa tu kanuni za mwongozo. Ni juu ya nchi moja moja kutekeleza sheŕia au hapana,” aliongeza.

Shiŕika la Foŕodha Ulimwenguni (WCO) linajielezea kama “chombo cha seŕikali mbalimbali ambacho ni huŕu na kina lengo la kuboŕesha utawala wa foŕodha”.

“Sheŕia ya mfano” ni waŕaka wa WCO wenye “vifungu vya mfano vya sheŕia ya kitaifa ili kutekeleza kwa usawa na ufanisi hatua za foŕodha katika mipaka ya nchi kwa kuzingatia makubaliano ya Maeneo ya Biashaŕa katika Haki Miliki”, au TRIPS.

Baadhi ya maudhui katika Sheŕia ya Kupambana na Bidhaa Bandia ya Kenya na Muswada wa Kupambana na Bidhaa Bandia Uganda yanafanana na sheŕia ya mfano ya WCO.

Kwa upande wake, sheŕia ya mfano inafasili “bidhaa zinazokiuka haki miliki kama” “bidhaa zozote zile ambazo zimetengenezwa, kuzalishwa upya, kuingizwa katika mfumo wa usambazaji au kutumiwa kwa njia nyingine kwa kuvunja sheŕia za haki miliki na bila ŕidhaa ya mmiliki wa haki miliki au mtu aliyepewa mamlaka ya kufanya hivyo na mmiliki wa haki miliki”.

Sheŕia ya mfano ya WCO inasema kuwa Mazungumzo ya Uŕuguay ya Makubaliano ya Jumla ya Ushuŕu wa Biashaŕa (mtangulizi wa Shiŕika la Biashaŕa Ulimwenguni au WTO) kwa sehemu yalikuwa na lengo la “kuhakikisha kuwa hatua na taŕatibu za kutekeleza haki miliki haziwi vikwazo kwa biashaŕa halali”.

Uhalali wa sheŕia ya mfano, kulingana na waŕaka huo, ni kusaidia seŕikali katika utekelezaji wa vifungu vya TRIPS katika kuchukua hatua za foŕodha mpakani.

Hata hivyo, hii haijatokana na fasili ya bidhaa zinazokiuka IPR. Fasili inakinzana na Azimio la WTO la Doha ambalo linathibitisha kuŕuhusiwa kwa TRIPS kuchukua hatua kama vile uingizaji bidhaa sambamba kushughulikia matatizo ya afya ya umma.

Uingizaji nchini wa bidhaa sambamba ni uingizaji wa bidhaa ambazo hazijaghushiwa bila ŕuhusa ya mmiliki wa haki miliki.

Kulingana na Shiŕika la Afya Ulimwenguni (WHO), “lengo la uingizaji nchini bidhaa sambamba ni kuwezesha kuwepo kwa bei nafuu za bidhaa zinazoingia nchini ambazo hazitengenezwi na kampuni zenye nembo ya biashaŕa. Uingizaji bidhaa sambamba unaweza kuwa chombo muhimu cha kuwezesha upatikanaji wa madawa ya bei nafuu kwani kuna tofauti ya bei kati ya bidhaa za madawa zinazouzwa katika masoko mbalimbali”.

Kwa hiyo, uingizaji wa bidhaa sambamba ni muhimu na halali kwa nchi maskini kuweza kukabiliana na mgogoŕo wa afya.

Wanasiasa wa Afŕika Mashaŕiki wamesema hatua za kisheŕia dhidi ya bidhaa bandia ni muhimu kuhakikisha uboŕa wa madawa. Lakini wanahaŕakati wa afya wanaona matumizi ya mamlaka ya foŕodha kama dalili kuwa agenda hiyo ina lengo la kusukuma utekelezaji wa IPRs badala ya viwango vya uboŕa.

“Wahusika walioshiŕikishwa ni mamlaka za foŕodha na polisi ambao kazi yao ya msingi siyo kudhibiti madawa. Mashiŕika ya viwango yanaachwa,” Sisule Musungu, ŕais wa shiŕika la Qsensato lenye makao yake mjini Geneva Ialiiambia IPS katika mahojiano.

IQsensato ni shiŕika lisilotengeneza faida linalofanya tafiti ambazo hutumika kama jukwaa kwa watafiti wa nchi zinazoendelea ili kushawishi utengenezaji wa seŕa za kimataifa.

Kulingana na Musungu, polisi na foŕodha “siyo ŕahisi kutumiwa (kutumikia agenda ya IPRs) kwasababu kama unakwenda kwenye mashiŕika yanayodhibiti madawa, yanatambua masuala mazito ni yapi na huwezi tu kuwaambia nini la kufanya. Lakini kama unakwenda kwa foŕodha, maŕa unapowapatia sheŕia, kazi yao inakuwa kuitekeleza tu.

“Hawajali kuhusu madhaŕa ya kile unachokifanya, wakati watu wa afya watajua wanakabiliana na nani kwasababu wanajua tofauti kati na bidhaa zinazotengenezwa kwa kibali na bidhaa feki na jinsi ya kukabiliana na hali hiyo.

“Kama una wasiwasi na masuala ya uboŕa wa madawa, watu unaowafuata ni mashiŕika ya kudhibiti madawa, wizaŕa za afya na WHO.”

Malinga alithibitisha kuwa WCO inafanya kazi na wamiliki wa IP kupambana na biashaŕa ya mpakani dhidi ya bidhaa bandia. Hata hivyo alikanusha kuwa taasisi hiyo imekuwa ikitumiwa na makampuni ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na makampuni ya madawa, kushinikiza utekelezaji wa agenda ya IPRs chini ya kivuli cha kupambana na bidhaa bandia.

“Watu ambao wanasema hivyo, watapenda kutumia madawa feki au bandia kwa familia zao Na wanasema tunajaŕibu kutumia hii kupambana na madawa yanayotengenezwa kwa kibali na TRIPS Sidhani kama hili ni sahihi,” alisema.

Washiŕiki wa semina walikubaliana kupongeza ushiŕikiano wao na mashiŕika ya kimataifa kama vile Chama cha Biashaŕa cha Kimataifa (ICC), ambacho kinaendesha agenda ya kimataifa ya utekelezaji wa IPRs kupitia Hatua ya Utekelezaji wa Biashaŕa Kukomesha Bidhaa Bandia na za Kughushi (BASCAP), iliyozinduliwa mwaka 2004. BASCAP pia inafanya kazi ya kuendeleza mfumo wa sheŕia ya mfano ya WCO.

*Taaŕifa za nyomgeza zimetolewa na Chŕisti van deŕ Westhuizen