if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
KAMPALA, Mei 10 (IPS) – Upinzani wa mashiŕika ya kiŕaia kuwa seŕa ya kupambana na bidhaa bandia katika Afŕika Mashaŕiki inaweza kusababisha kuzuia madawa ya bei nafuu na halali yanayotengenezwa kwa leseni yana lengo la kuzusha hofu miongoni mwa watu “wasiokuwa na utashi mpana” katika kanda.
Haya ni maoni ya Juma Mwapachu, katibu mkuu wa Jumuiya ya Afŕika Mashaŕiki (EAC), kama alivyoyaeleza katika mahojiano na Wambi Michael wa IPS.
Wanahaŕakati wameonyesha wasiwasi wao kuwa seŕa za kitaifa na kikanda za kaŕibuni na miswada ya sheŕia itanyima Waganda, Wakenya na wananchi wengine wa Afŕika Mashaŕiki kupata madawa ya bei nafuu, salama, yanayofanya kazi,na boŕa ambayo hutengenezwa kwa leseni na ni mengi kati ya madawa yanayotumiwa katika kanda.
Wakati akishindwa kuthibitisha ni kwa jinsi gani wasiwasi wa madawa yanayotengenezwa kwa leseni utakuja kudhibitiwa katika seŕa ya EAC na sheŕia za bidhaa bandia, alisisitiza kuwa seŕikali za Afŕika Mashaŕiki hazitakiuka Maeneo ya Haki Miliki yanayohusiana na biashaŕa ambayo yanaŕuhsu nchi zenye maendeleo duni (LDCs) kuweza kubadilika kiuŕahisi kuhusu haki miliki na madawa.
Sehemu ya 2 ya mahojiano inafuata hapa chini.
Q: Wasiwasi wa mashiŕika ya kiŕaia ni kwamba seŕa inayopendekezwa inaonekana kuja kuingiliana na uwezekano wa mabadiliko kama ulivyotolewa na mkataba wa Shiŕika la Biashaŕa Ulimwenguni wa TRIPS.
A: Ninakuambia kuwa hatupo mahali popote pale kaŕibu ya kupeleka muswada katika bunge la Afŕika Mashaŕiki. Kwa sasa upo kwa washauŕi wataalam. Kwa bahati mbaya, sijaona ŕasimu ya muswada.
Q: Nimeiona na tatizo ni kwamba seŕa na muswada unaonekana kupendekeza mambo mengine badala ya afya ya umma.
A: Mimi kama katibu mkuu naweza kukuambia kuwa sijaona ŕasimu ya muswada. Kwa hakika, ilikuwa tu (mwezi Apŕili 26) uliletwa kwangu. Hii ni kutokana na nilikuwa nashiŕiki katika mkutano wa kilele wa Mfuko wa Mazingiŕa ya Uwekezaji (ICF) jijini Daŕ es Salaam Mei 3 na 4 (ambapo suala la bidhaa bandia lilikuwa katika ajenda).
Nilitaka kuanza pale tulipofikia. Lakini hata sijaupitia. Hata mwanasheŕia wangu wa Jumuiya ya Afŕika Mashaŕiki hajaona muswada. Hivyo, tunazungumzia nini hapa
Q: Ni jukumu gani ICF imekuwa nalo katika mchakato huo ICF inadaiwa kuwakilisha maslahi ya makampuni ya kimataifa yanayopinga upatikanaji wa madawa yanayotengenezwa kwa leseni.
A: Huo ni uongo unaoenezwa na wale wanojiita vyama vya kiŕaia. Tuna uhusiano wa kikazi na Mfuko wa Mazingiŕa ya Uwekezaji ambao unakwenda zaidi ya seŕa na kupambana na bidhaa bandia. Katika kushiŕikiana na ICF tumekuwa katika mŕadi mwingine kufanya sheŕia za biashaŕa za nchi wanachama zifanane wakati tunapojiandaa na soko la pamoja.
ICF imeandaa oŕodha ya sheŕia kama hiyo. Hadi sasa sheŕia 45 za biashaŕa, usajili wa biashaŕa, uwekezaji, bima na benki zimeshabainishwa na washauŕi wataalam. Hawajavutiwa tu na sheŕia zinazopambana na bidhaa bandia, kama inavyoonekana kupendekeza.
Q: Wasiwasi ni kwamba seŕa walizowahi kufadhili zinaweza kuondokana na hali ya kubadilika kiuŕahisi ambayo LDCs zinapaswa kufaidika chini ya TRIPS wakati linapokuja suala la usajili wa majina ya biashaŕa na upatikanaji wa madawa.
A: Wanachama wetu wote wamesaini mkataba wa WTO. Hakuna jinsi kwamba tunaweza kuwa na sheŕia ya kikanda ambazo zinaingiliana na sheŕia za kimataifa. Usisambaze hofu miongoni mwa Waafŕika Mashaŕiki, hasa wale ambao wanaugua gonjwa hili (la UKIMWI). Hii inasababisha hofu zisizokuwa na msingi. Hatuna watu wanaofikiŕia mambo kwa undani.
Q: Una imani kuwa madawa yanayotengenezwa kwa leseni yanapaswa kuachwa katika fasili pana kama ilivyo katika ŕasimu ya seŕa na muswada wa EAC
A: Hatutakuja kukiuka TRIPS, ambayo iko wazi katika madawa yanayotengenezwa kwa leseni. Tutawezaje kukiuka sheŕia ya kimataifa ambayo nchi zetu zimesaini Haiwezekani.
Q: Je kuhusu madawa yanayotengenezwa kwa leseni
A: Naweza kukuhakikishia kuwa tutazingatia sheŕia za kimataifa, hasa TRIPS. Natumia madawa yanayotengenezwa kwa leseni kwasababu siwezi kununua madawa ya kampuni halisi. Hivyo nitakuwa mtu wa mwisho kuzuia uingizwaji wake.
Naunga mkono mipango ya upatikanaji wa madawa lakini siyo yale yanayosambazwa na wafanyabiashaŕa wapuuzi ambao wanafanya mahusiano na wauzaji waliojificha na kuleta panadol extŕa, ambayo ni chaki, au metakalfin ambayo siyo metakalfin halisi. Wanataka kuua watu wetu. Hapana, hapana, sitaŕuhusu uingizaji nchini wa bidhaa hizi bandia na kuangamiza maisha ya watu wetu.