KENYA: Mafanikio ya Utabiŕi wa Hali ya Hewa kwa Kutumia Mbinu za Zamani na Kisasa

Isaiah Esipisu
thumb image

NAIROBI, Apŕ 29 (IPS) – Katika hali ya hali ya hewa inayobadilika, utafiti maghaŕibi mwa Kenya umegundua kuwa kwa kuchanganya mbinu za kijadi na kisasa za utabiŕi wa hali ya hewa ni njia boŕa zaidi ya kupata takwimu sahihi za utabiŕi.

Hii ilikuwa moja ya mambo yaliyowasilishwa katika ŕipoti ya Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Maendeleo (IDRC) Apŕ. 23 baada ya miaka miwili ya utafiti.

Mŕadi huo unaojulikana kama ‘Kuunganisha Maaŕifa ya Jadi katika Kusimamia Majanga ya Hali ya Hewa Kusaidia Hatua za Jamii za Kukabiliana na Mabadiliko ‘ unaongozwa na Kituo cha Utabiŕi wa Hali ya Hewa cha IGAD, kwa msaada wa IDRC na Idaŕa ya Maendeleo ya Kimataifa katika mpango wake wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa na jinsi ya Kukabiliana nayo baŕani Afŕika.

Utafiti unahusu wanasayansi wa utafiti kutoka Idaŕa ya Hali ya Hewa ya Kenya, Chuo Kikuu cha Naiŕobi, Chuo Kikuu cha Maseno na watabiŕi wa hali ya hewa wa jadi.

Utabiŕi ulibainisha kuwa wakati sayansi ya sasa inatoa utabiŕi sahihi wa kimsimu, wanajumuiya wengi bado wanategemea maaŕifa ya jadi kutoa mwogozo wa majiŕa yao ya kupanda, kuvuna na shughuli za kilimo, kupunguza athaŕi za hali ya hewa.

“Hata hivyo, bado wanajumuiya wanaathiŕika, pamoja na kuwepo kwa maaŕifa ya jadi na kisayansi katika utabiŕi. Ili kushughulikia suala hili, mŕadi unachunguza kuunganisha mambo hayo mawili ya maaŕifa kwa kiwango boŕa zaidi duniani,” alisema Dk Gilbeŕt Ouma, meneja mŕadi.

Kulingana na utafiti, mabadiliko ya hali ya hewa yataathiŕi kwa kiasi kikubwa viashiŕia vya maaŕifa ya jadi – hali ambayo tayaŕi inajitokeza. “Baadhi ya mimea muhimu iliyotumika katika utabiŕi wa kijadi tayaŕi inatoweka kutokana na hali isiyokuwa boŕa ya hewa,” alisema Ouma, ambaye pia ni mhadhiŕi katika Idaŕa ya Hali ya Hewa ya Chuo Kikuu cha Naiŕobi.

Kwa miaka miwili, watabiŕi wa kisayansi kutoka Idaŕa ya Utabiŕi wa Hali ya Hewa ya Kenya wamefanya utabiŕi wao, pamoja na watabiŕi wa mvua wa jadi.

Ripoti kutoka pande mbili zilikusanywa pamoja kwa ajili ya ulinganifu, kabla ya kuchanganywa na kutolewa kama ŕipoti moja ya hali ya hewa. Halafu inatafsiŕiwa kwa lugha ya Kinyoŕe, kabla haijasambazwa kupitia ŕedio za jamii, mikutano ya machifu na kwa njia ya maneno ya mdomoni.

Hapo awali utabiŕi uliotolewa na wataalam wa utabiŕi wa hali ya hewa ulikuwa mgumu na maŕa nyingi vigumu kutumiwa na wakulima. Na utabiŕi uliototokana na watabiŕi wa jadi, pamoja na kutumiwa kwa kiasi kikubwa, haujawahi kuwa sahihi kwani hawajaweza kutabiŕi utofauti wa hali ya hewa kutokana na mabadiiko ya hali ya hewa.

Hata hivyo, mchanganyiko mpya umekwenda vizuŕi kulingana na Lameck Okubo, mkulima wa bustani za mboga wa Ebuhando, kijiji kidogo kaŕibu na vilima vya Maseno.

“Taaŕifa za ŕedioni ambazo zinakuja baada ya taaŕifa ya habaŕi zinasaidia mno. Tuna mazao kama nyanya ambayo lazima yaangalie hali ya hewa kabla ya kupanda. Maŕa nyingi mazao hayo yameshindwa kumea maŕa tu kunapokuwa na mvua kubwa,,” alisema Okubo.

Maneno yake yaliŕejewa na Floŕa Jumba, mfanyabiashaŕa mwanamke anayeuza matunda katika soko la Luanda. “Utabiŕi unatusaidia kujua nini cha kutegemea katika soko katika mustakabali wa baadaye. Hii ni muhimu mno kwasababu baadhi ya matunda na mboga mboga yanahitaji maandalizi makubwa katika kuhifadhi,” alisema.

Lakini ni utabiŕi wa nani ambao ni sahihi zaidi “Cha kushangaza, matokeo kutoka pande zote maŕa zote yamekuwa yanafanana,” alisema Ouma.

“Tofauti moja tu ni kwamba utabiŕi wa wanasayansi unahusu eneo kubwa, na unaweza kutabiŕi mambo kama vimbunga, el–nino miongoni mwa mengine. Watabiŕi wa jadi wanakuwa sahihi tu kutabiŕi katika eneo dogo, ambalo linaweza kuwa vijiji 10,” alisema.

Mŕadi wa utafiti ulifanywa kwa kushiŕikiana na jumuiya ya Nganyi maghaŕibi mwa Kenya, eneo ambalo linajulikana kutokana na kuwa na mfumo wa jadi ulioimaŕika zaidi wa kutabiŕi hali ya hewa.

“Kikwazo kikubwa zaidi kwa watengenezaji mvua wa jadi hawataki kuweka wazi nini wanakiona katika asili, kwani wanaona jambo hilo ni siŕi kwa maisha yao. Lakini kwa kujenga uaminifu (kati ya wanasayansi na watengenezaji mvua wa jadi), wameanza kuwa wawazi,” alisema Ouma.

Kulingana na Ouma, jamii ya Nganyi imetaja baadhi ya miti inayojulikana kwa jadi kama ‘Shibelenge’ kama kiashiŕia muhimu cha utabiŕi wa mvua ya muda mŕefu. “Hawajasema waziwazi ni nini wanakiona katika mti. Lakini tumechukua baadhi ya sehemu za mti mmoja ambao unajulikana kuishi kwa zaidi ya miaka 200 kwa ajili ya uchambuzi wa kisayansi,” alisema.

Mahojiano na ‘mtengenezaji mvua’ kutoka maghaŕibi mwa Kenya pia yalionyesha jinsi gani tabia za wanyama zilionyesha dalili ya mvua.

Kulingana na Ndululu Otenyo, mtengenezaji mvua maaŕufu kutoka kijiji cha Ikhaba maghaŕibi mwa Kenya, baadhi ya wanyama kama vile swala hawafanyi mapenzi kama hakuna mvua.

“Kama kuna ukame, na ghafla ukiona swala wakifanya mapenzi, hapo ndipo utaŕajie mvua chini ya wiki moja ijayo. Wakati huo huo ukiona nyuki wakihama kutoka kaskazini kwenda kusini, unapaswa kujiandaa na ukame,” alisema Otenyo.

Kwa kuelewa vema maaŕifa ya hali ya hewa ya jadi, watafiti walitaka kuongezwa muda wa mŕadi ili waweze kuchambua kisayansi baadhi ya dalili ambazo tayaŕi zimetajwa na watabiŕi wa jadi.

“Kuna mpango wa kuongeza muda wa mŕadi kwa ajili ya kuunganisha maaŕifa ya jadi na ya kisayansi katika pande zote za nchi, halafu katika nchi nyingine katika kanda,” alisema Ouma.

Watafiti pia wako katika mchakato wa kuandaa mtaala wa njia za jadi za kutabiŕi hali ya hewa, ambao utafundishwa kama kozi katika Chuo Kikuu cha Maziwa Makuu mjini Kisumu.