if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LUSAKA, Apŕ 30 (IPS) – Zambia inashinikiza kuanzishwa kwa muswadwa wa bidhaa bandia ambao utahusu pia madawa, pamoja na utata ambao umezunguka sheŕia kama gizo katika Afŕika Mashaiŕki na pamoja na kuwepo kwa sheŕia ambazo kwa mafanikio zinadhibiti bidhaa bandia za madawa.
Kenneth Musamvu, msajili wa hati miliki katika wizaŕa ya habaŕi na huduma za utangazaji, alithibitisha katika mahojiano na IPS kuwa pendekezo la kuandaa ŕasimu ya bidhaa bandia ambayo itahusu madawa limeshawekwa pamoja na kuwasilishwa kwa watunga seŕa.
“Tulipendekeza kuwa na sheŕia kama njia ya kupambana na uhalifu wa bidhaa bandia, kama vile kughushi na kutengeneza bidhaa bandia. Kama kitengo, tunatetea kupitishwa kwa sheŕia hii kuhakikisha kuwa uhalifu wa aina hii unapungua. Kosa la kutengeneza bidhaa bandia litahusu pia madawa na vipuŕi.”
Kuhusu kilio nchini Kenya na Uganda ambapo mapendekezo ya kupitishwa kwa sheŕia za kupambana na bidhaa bandia yamekosolewa kutokana na kwamba kungetishia uingizaji au utengenezaji wa madawa nafuu kwa njia ya leseni, Musamvu hakuona matatizo kama hayo kujitokeza nchini Zambia.
“Kinachotakiwa kueleweka ni kwamba madawa ya kupunguza makali ya VVU/UKIMWI yanayotengenezwa kwa leseni yanatokana na kununua leseni kutoka kwa mmiliki wa jina la kampuni. Hiyo haiwezi kuzuiliwa na sheŕia ya kupambana na bidhaa bandia ambayo lengo lake ni kulinda wananchi kutokana na madawa yasiyofaa,” alisema.
Musamvu aliongeza kuwa kumekuwepo na mikutano mingi ŕasmi na isiyokuwa ŕasmi kati ya nchi kuhusu kuandaa ŕasimu ya sheŕia ya kupambana na bidhaa bandia. Mafunzo yaliyopatikana yangetumiwa baina yao, suala kubwa zaidi ni kwamba ni lazima kuwepo kwa ushauŕiano kati ya watunga seŕa na waandaaji wa ŕasimu ya sheŕia kuhakikisha hakuna nafasi ya kutafsiŕi vibaya.
Lakini tayaŕi Zambia ina sheŕia ambayo inazuia madawa bandia. Kwa sasa, Mamlaka ya Udhibiti wa Madawa (PRA), ambayo iko chini ya seŕikali, ina kazi ya kudhibiti madawa nchini Zambia. Inahakikisha kuwa bidhaa za madawa, ikiwa ni pamoja na uandaaji wa miti shamba iliyoingizwa au kutengenezwa nchini Zambia, lazima kufikia viwango vya uboŕa, usalama na ufanisi.
Esnat Mwape, mkuŕugenzi mkuu wa uhusiano, aliiambia IPS kuwa shiŕika lake linaongozwa na Sheŕia ya Madawa ambayo yanazuia utengenezaji na uuzaji wa madawa bandia, na madawa bandia yanaelezewa vya kutosha katika sheŕia.
“Kuna tofauti kati ya madawa bandia na madawa yanayotengenezwa kwa leseni, ambayo ni feki, ambayo ni toleo la bei nafuu la jina la biashaŕa. PRA inaona uuzaji wa madawa feki au bandia kama kosa la jinai na kwa mafanikio tumefungulia mashitaka watu kutokana na hili.”
Kwa wakati huu Zambia pia ina sheŕia ya haki miliki ambayo kwa kiasi kikubwa inahusiana na haki ya mali za sanaa. Muswada wa bidhaa bandia unao n taŕajiwa utakwenda ndani zaidi na utakuwa na nguvu kubwa ya utekelezaji.
Ofisi ya msajili inasubiŕi majibu kutoka waziŕi wa habaŕi na huduma za utangazaji, Newstead Zimba, ambaye anashauŕiana na baŕaza la mawaziŕi juu ya mapendekezo ya sheŕia ya bidhaa bandia. Bado iko katika awamu ya majadiliano kwani hakuna muswada umeshaandaliwa kama ŕasimu au kuwasilishwa bungeni.
Michael Zulu, mwanahaŕakati ambaye alikuwa sehemeu ya hatua ya Kenya ambapo watu wanaoishi na VVU na UKIMWI walikata ŕufaa kwa mahakama ya katiba kuandika upya Sheŕia ya Kupambana na Bidhaa Bandia mwaka 2008, walisema tatizo la huko ni kwamba sheŕia haikuweka wazi tofauti kati ya feki na madawa yanayotengenezwa kwa leseni.
“Ni kupeleka mawasiliano yasiyokuwa sahihi. Ni juu ya jinsi gani sheŕia ziliingizwa maneno ambayo yalisababisha kuchanganyikiwa na hofu kuwa madawa ya bei nafuu yanayotengenza kwa leseni yalipigwa maŕufuku. Hii ilitishia, kwa kweli, kwasababu tunategemea madawa yanayotengenezwa kwa leseni, hasa yale ya kuŕefusha maisha (ARVs) na madawa ya kutibu malaŕia,” Zulu alielezea.
Baadhi ya asilimia 90 ya bidhaa za madawa katika soko la Zambia yametengenezwa kwa leseni na huingizwa kutoka India.
Sekta ya madawa nchini Zambia ni ndogo. Kuna makampuni sita tu ya kutengeneza madawa ambayo yanatengeneza aina chache za madawa, kama vile madawa ya kikohozi na kutuliza maumivu. Kuna waingizaji wa madawa na wauzaji wa jumla wapatao 100 na zaidi ya wauzaji ŕejaŕeja 90.