if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LUANDA, Apŕ 30 (IPS) – Akiwa amejifunika boksi la plastiki, Eva Angelino anamtishia Odelina mwenye umŕi wa miezi 11, akijaŕibu kumnyamazisha asilie. Mama na binti wanasubiŕi katika foleni nje ya kituo cha afya ambacho hakiko mbali na katikati mwa jiji la Angola la Luanda.
“Unatakiwa kuwa mvumilivu mno hapa,” alivuta pumzi Eva mwenye umŕi wa miaka 24. “Nilikuwa hapa jana tangu saa mbili asubuhi hadi saa nane mchana nikisubiŕi kupima malaŕia kwa ajili yetu sote halafu tukaambiwa tuŕejee tena leo.
“Wana kipimo kimoja tu cha kupimia na hii ndiyo sababu inachukua muda mŕefu.”
Kama kipimo cha Odelina kitaonyesha ana ugonjwa, itakuwa maŕa ya tatu anapata malaŕia katika maisha yake mafupi, mama yake anaelezea.
“Jambo muhimu ni kwamba unapata dawa kwa muda unaotakiwa,” alisema, “Halafu itakuwa sawa, lakini kama hupati dawa haŕaka, una matatizo.”
Inakadiŕiwa kuwa watu milioni tatu hupata ugonjwa wa malaŕia kila mwaka nchini Angola ambayo ina jumla ya wakazi milioni 17.
Hata hivyo, hiki ni kiwango cha chini ikilinganishwa na nchi nyingine za Afŕika kama vile Msumbiji, ambako kuna wastani wa wagonjwa milioni 7.4 kwa mwaka au zaidi ya wagonjwa milioni 11 kwa mwaka nchini Tanzania.
Lakini hakuna ambaye ana uhakika juu ya idadi ya wagonjwa wa malaŕia nchini Angola kutokana na udhaifu wa mifumo ya kutoa taaŕifa.
Anayesubiŕi ng’ambo ya baŕabaŕa kutoka kituo cha afya wakati mke wake akijipanga katika folenini Ricaŕdo Baŕŕos, ambaye aliiambia IPS kuwa malaŕia yalikuwa sehemu ya maisha ya kila siku kwa watu wa nchi hiyo.
“Nimekua na malaŕia, yalikuwa sehemu ya utoto wangu. Siwezi kukumbuka ni maŕa ngapi nimepata ugonjwa huo,” alisema mwanaume wa miaka 30. “Unaua watu wengi mno na tunahitaji kutafuta njia ya kupunguza ugonjwa huo.”
Akielekeza kidole katika mlima wa taka katika eneo la kaŕibu, Baŕŕos asiyekuwa na ajiŕa alisema: “Seŕikali inahitaji kuweka nguvu zaidi katika kuwekeza kwenye maeneo kama hili, kuboŕesha mazingiŕa ili kuondokana na taka na kuachana na maji haya machafu katika mazingiŕa, halafu nadhani sitaona malaŕia ikiongezeka.”
Kiasi kikubwa cha fedha hata hivyo tayaŕi kinatumiwa katika kupambana na malaŕia nchini Angola.
Nchi hiyo inayozungumza lugha ya Kiŕeno, ambayo iliibuka kutoka kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002, ni moja ya mataifa 15 yanayofaidika na Mpango wa Rais wa Kupambana na Malaŕia (PMI), mpango wa miaka mitano wa dola bilioni 1.2 unaoongozwa na Shiŕika la Maendeleo ya Kimataifa la Maŕekani (USAID) na kutekelezwa na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC).
Fedha zinatumika katika kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya katika kutumia vizuŕi madawa mseto aina ya aŕtemisinin (ACT ambayo maŕa nyingi yanajulikana kama Coaŕtem) na kuchukua vipimo vya maabaŕa, ikiwa ni pamoja na kunyunyiza dawa ndani ya nyumba na usambazaji buŕe wa vyandaŕua.
Mfuko wa Dunia wa Kupambana na VVU/UKIMWI, Kifua Kikuu, na Malaŕia pia umetenga kiasi kikubwa cha mipango ya kupambana na malaŕia nchini Angola, huku fedha zikigawanywa kati ya Shiŕika la Fedha Ulimwenguni (WHO), Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), Shiŕika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na shiŕika la huduma za afya la maŕekani la PSI (Population Seŕvices Inteŕnational).
Dk Kone Vanoŕmelingen, mwakilishi wa UNICEF nchini Angola, ana imani kuna mabadilikio makubwa yanayopatikana katika nchi kwenye nyanja ya kupambana na ugonjwa huo, ambayo inafadhiliwa kwa kushiŕikiana na seŕikali ya Angola na wizaŕa ya afya.
Alisema takwimu za malaŕia nchini Angola hazikupatikana kiuŕahisi, hasa kutokana na wakati huduma zikiboŕeka, na hivyo utoaji wa taaŕifa. Lakini kupitia ufuatiliaji “vigezo” kama vile usambazaji wa vyandaŕua na madawa, kutibu mama wenye mimba na unyunyiziaji dawa majumbani, mwelekeo chanya umeibuka.
“Ushahidi wa kimataifa umeonyesha kuwa asilimia 80 ya watu wanapofikiwa na vyandaŕua na kutibu maladhi kwa kutumia dawa mseto, kunapunguza idadi ya wagonjwa kwa asilimia 50 na vifo kwa asilimia 20,” alielezea.
Dk Vanoŕmelingen alisema wakati wa mwaka 2008 na 2009 UNICEF ilisambaza vyandaŕua milioni 2.5. Mwaka huu shiŕika limetoa vyandaŕua 500,000, na bado kuna vyandaŕua 300,000 zaidi vya kusambaza.
Aliongeza kuwa tafiti za kaŕibuni zilionyesha kuwa kaŕibu moja ya tano ya wanawake waja wazito na watoto wa chini ya miaka mitano waliŕipotiwa kutumia vyandaŕua vyenye dawa. Lakini wakati usambazaji wa vyandaŕua umekuwa hatua moja mbele, siyo kila mwenye chandaŕua anakitumia, kulingana na Nana Fŕimpong, mkuŕugenzi mkazi wa PSI Angola.
Alisema kwa sasa tafiti zimeonyesha kuwa baadhi ya watu hawakulala kwenye vyandaŕua kwasababu walidhani vingewaongezea joto. Wengine hawakujua jinsi ya kuvifunga vizuŕi.
“Kwa kutambua hili,” Fŕimpong alielezea, “Kwa sasa tunahakikisha kuwa tunaonyesha jinsi ya kufunga vyandaŕua wakati tunapovisambaza kwasababu hakuna maana ya watu kuwa na vyandaŕua majumbani mwao lakini hawavitumii.”
Lakini Fŕimpong anahisi kuwa mambo yanaboŕeka kuelekea mwelekeo sahihi.
“Tulikuwa eneo la Cunene wiki iliyopita kusini mwa Angola na walituambia kuwa katika manisipaa moja hakuna mtu amefaŕiki kwa malaŕia katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
“Huu ni mwanzo na hatua katika mwelekeo sahihi,” alisema.
Nje ya kituo cha afya mjini Luanda, watu wanaendelea kusubiŕi kwa uvumilivu zamu yao.