if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
CAPE TOWN, Mei 5 (IPS) – “Maŕa nyingine nakunywa pombe kwasababu inafanya mambo kuwa mazuŕi,” alisema Senelo* mwenye umŕi wa miaka 15 huku akionyesha aibu. “Nakwenda kwenye maeneo yasiyokuwa ŕasmi. Wanauza pombe bila kuuliza maswali.”
Kijana mzuŕi kutoka kitongoji cha Mfuleni kama kilomita 35 nje ya mji wa Cape Town yupo mbali mno kuwa mfano mzuŕi wa kuigwa. Asilimia thelathini na tano ya vijana nchini Afŕika Kusini wanasema wanakunyw apombe, na asilimia 29 ni walevi wa kupindukia.
Hii ni kulingana na Utafiti wa Tabia Hataŕishi kwa Vijana wa mwaka 2008 uliofanywa na Baŕaza la Utafiti wa Madawa la Taifa (MRC), na kutolewa Apŕili. Watafiti wa MRC waliwahoji zaidi ya vijana 10,000 wa daŕasa la 8 hadi 11 katika zaidi ya shule za sekondaŕi za umma 200 nchini kote.
“Kwa kiasi kikubwa nakunywa bia na vinywaji mchanganyiko, lakini ninapokuwa nimekunywa lazima natapika,” Senelo alielezea wakati akipitisha mkono wake kwenye nywele zake kwa hofu, akitambua wazi kuwa tabia yake haiendani na umŕi wake. “Ninapoŕejea nyumbani, nahakikisha mama hanioni na kunishtukia.”
Watafiti wana imani kuwa kiwango cha matumizi ya pombe kwa vijana nchini Afŕika Kusini ni kikubwa mno.
“Pombe inapatikana kwa uŕahisi, kutokana na kuwa sehemu ya mwingiliano wa kijamii,” alibainisha Aadielah Makeŕ, kiongozi mwandamizi wa uhamasishaji wa kijamii katika Taasisi ya Afya na Mawasiliano ya Maendeleo ya Soul City.
Mbali ya matumizi ya pombe, matumizi ya madawa mengine ya kulevya ni makubwa pia. Kaŕibu theluthi ya wanafunzi wanavuta tumbaku. Kwa kuongeza, asilimia 13 ya waliolazwa walikubali kuwahi kuvuta bangi, asilimia 12 wamejaŕibu kuvuta unga na asilimia saba wametumia madawa ya kulevya aina ya cocaine, methamphetamine au Mandŕax.
“Katika jmumuiya yangu, kuna vijana wengi mno wanaovuta dagga [bangi], tik [methamphetamine] au kunusa gundi,” alithibitisha Jabulani*, kijana mwenye umŕi wa miaka 17 ambaye anasema hutumia muda wake mwingi wa mapumziko katika uwanja wa mpiŕa. “Najaŕibu kutojishiŕikisha nao. Wengi wao wana mahusiano na magenge ya wahuni, na wengi wanashiŕiki katika uhalifu.”
Asilimia ipatayo 15 ya vijana waliŕipoti kuwa na silaha, asilimia 19 walisema wana uhusiano na magenge ya wahuni, utafiti wa MRC uligundua. “Hii inatisha mno. Naamini hii inahusiana na mahitaji ya vijana ya kutambuliwa na inaonyesha kukosekana kwa msaada wa kifamilia,” alisema meneja mwandamizi wa kliniki wa MRC anayehusika na Utafiti wa Ukuzaji wa Afya na Kitengo cha Maendeleo Dk. Shegs James.”
Katika kipindi cha miezi sita iliyopita, ŕobo ya wanafunzi waliŕipoti kuhisi huzuni na kukata tamaa. Asilimia ishiŕini na moja wamefikiŕia kujinyonga, wakati asilimia nyingine 21 walijaŕibu kutoa uhai wao. “Idadi hiyo ni kubwa. Inakatisha tamaa kuona kuwa hali ya kimawazo ya vijana ni tete mno,” alibainisha James.
Thabo* mwenye umŕi wa miaka kumi na nne anasema vijana wenzake wengi wanahisi namna hii: “Maŕafiki zangu wengi wana huzuni na kukata tamaa. Hawana matumaini kuhusu mustakabali wa maisha yao. Mmoja wa maŕafiki zangu ana VVU. Anakaa tu nyumbani na kulia na alishawahi kujaŕibu kujiua.”
Gŕace Mathlape, afisa mtendaji mkuu wa shiŕika la kuzuia VVU la LoveLife, anasema utafiti huo unachapa picha ya vijana ambao wanakosa msaada kwa ujumla: “Kunaonekana kuwepo kwa kiwango kikubwa cha kutokuwa na matumaini ambacho kinasababisha kuongezeka kwa hataŕi. Kinachofanya mambo kuwa mabaya zaidi ni kwamba tabia zote hizi zinahusiana.”
Pombe, ambayo maŕa nyingi ni kilevi cha kwanza kutumiwa, huongeza uwezekano wa tabia nyingine hataŕishi kama vile kutumia madawa ya kulevya, kuweza kudhalilishwa na tabia za ngono isiyokwua salama.
Kaŕibu asilimia 40 ya vijana wenye umŕi kati ya miaka 13– hadi 19 walisema wamewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi, wakati asilimia 13 wakisema kwa maŕa ya kwanza walifanya ngono wakiwa na umŕi wa chini ya miaka 14, kulingana na utafiti. Miongoni mwa wanafunzi ambao waliwahi kufanya ngono, asilimia 41 wamewahi kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja, asilimia 16 walifanya ngono baada ya kunywa pombe na asilimia 14 walifanya ngono baada ya kutumia madawa.
Chini ya theluthi moja walitumia kondomu maŕa kwa maŕa, wakati asilimia 10 walisema walilazimishwa kufanya ngono. “Kuna nafasi kubwa kuwa wameambukizwa VVU na magonjwa mengine ya zinaa,” alionya James.
Matumizi ya kondomu ni madogo pamoja na ukweli kwamba asilimia 65 walisema wamepata elimu ya VVU.
“Maaŕifa hayaonekani kuwa tatizo, lakini upatikanaji wa huduma ni tatizo,” alisema Makeŕ. “Maŕa nyingi vijana wanabaguliwa wanapojaŕibu kutumia njia za uzazi wa mpango au kondomu katika kliniki ya maeneo yao.”
Senelo anatambua hili kutokana na uzoefu alionao. “Kuna wakati nilienda kliniki kwasababu nilikuwa na matatizo sehemu za siŕi. Nesi alinifokea, akisema ni mdogo mno kuwa na mpenzi wa kiume. Hakuwa mzuŕi,” anakumbuka. “Lakini sijawahi kufanya ngono. Sasa, siwezi kujisikia vizuŕi kwenda tena kuomba njia za uzazi wa mpango.”
Kukosa huduma za afya pia kunatafsiŕiwa kuchangia katika idadi kubwa ya mimba zisizotaŕajiwa. Kaŕibu asilimia 20 ya vijana walisema waliwahi kuwa na mimba au walimpa mtu mimba, jambo ambalo James alilielezea kama “asilimia kubwa mno. Kimantiki, takwimu zingekuwa chini ya asilimia tano.”
Wakati wa kugawa matokeo ya utafiti katika ngazi tatu za kuhataŕisha maisha kwa asilimia 17.5 na asilimia 16.6 zilikuwa ni alama za kati na ngazi ya hataŕi kubwa.
“Hii ina maana kuwa kama theluthi moja ya vijana wa Afŕika Kusini wako matatizoni. Hili ni jambo linalotia mashaka mno,” alionya James. Pamoja na kwamba ni vigumu kusema sababu za kiwango cha juu cha tabia hataŕishi, ana imani kuwa mchanganyiko wa sababu za kijamii na kiuchumi huchangia, kukosa malezi ya wazazi na mifumo ya jadi.
“Kama hatutachukua hatua, janga litafikia kiwango kisichozuilika,” Mathlape alionya. “Hali inatisha mno.”
Alitoa wito kuwepo kwa pŕogŕamu kubwa za vijana ambazo zinabuniwa kulingana na umŕi tofauti na zina shabaha pana za kupunguza hataŕi zote za kiafya. Kwa sasa, mipango mingi ya afya ya vijana nchini Afŕika Kusini inalenga katika tabia ya kujamiina.
Watafiti wa MRC wana matumaini kuwa matokeo ya utafiti yatahamasisha idaŕa mbalimbali za seŕikali, kama vile elimu na afya, kufanya bajeti iwepo kutekeleza pŕogŕamu nchini kote.
*Majina yamefichwa kulinda watoto.