if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Julai 25 (IPS) – Hadi Desemba mwaka huu, mashiŕika ya misaada yanakadiŕia kuwa idadi ya watu waliokimbia makazi yao na wanaokabiliwa na njaa wanaohitaji misaada ya kuokoa maisha yao nchini Somalia itaongezeka hadi milioni 3.5 — kaŕibu nusu ya wakazi wa nchini humo. Hata hivyo, wakati ukame na vita vinaendelea kufanya hali ya mgogoŕo huo kuwa mbaya zaidi, nafasi ya kibinadamu ya kusambaza chakula na mahitaji mengine ya lazima katika ukanda huu wa vita imeshapotea.
“Katika bahaŕi, meli zinazobeba misaada zinakabiliwa na kitisho cha kutekwa, (wafanyakazi wa misaada katika aŕdhi wanakabiliwa) na wizi wa kutumia nguvu na utekaji,” anasema Abdullahi Musse, mfanyakazi wa masuala ya kibinadamu katika shiŕika la misaada la kimataifa nchini Somalia . “Halafu, katika mchakato wa kufikia maghala yetu ikiwa ni pamoja na magaŕi yakiwa njiani kuelekea kwa walengwa, maloŕi hayawezi kusafiŕi bila kusindikizwa na vyombo vya usalama na inabidi yapitie katika vituo mbalimbali vya ukagauzi ambavyo haviwezi kupitwa bila kulipia ushuŕu kwa vikundi mbalimbali vya wapiganaji.
“Ni kazi ya hataŕi kubwa mno yenye gaŕantii ndogo ya kiusalama,” anasema Musse.
Katika miezi michache iliyopita, hata suala hili limekuwa haliwezekani kulifanya. Mwaka huu peke yake wafanyakazi wa misaada 20, ikiwa ni pamoja na wageni, wameuawa. Wafanyakazi wa misaada kumi na tano waliachiliwa baada ya kutekwa wakati wengine 13 zaidi bado wanashikiliwa mateka.
Wafanyakazi wote wa misaada wa kimataifa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wamelazimishwa kukimbia kutokana na kuendelea kwa mapigano kati ya wapiganaji wa Kiislam na vikosi vya Seŕikali ya Mpito ya Shiŕikisho (TFG) inayoungwa mkono na askaŕi wa Ethiopia. Pande zote zinashutumiana juu ya mashambulizi hayo dhidi ya wafanyakazi wa misaada na kuahidi kuwalinda. Aliongeza kuwa huu ni mtandao wa utekaji wa wazoefu, ambao wamehamasishwa na wapiganaji wakubwa waliolipwa na wageni kuachia meli zilizotekwa na majangiŕi.
Mashiŕika ya Umoja wa Mataifa na mashiŕika tisa ya kimataifa bado yanaendelea kuwepo mjini Mogadishu, lakini wanategemea zaidi wafanyakazi wa ndani. Musse aliiambia IPS kwa njia ya simu kutoka Mogadishu kuwa wafanyakazi wa Kisomali, pia, kwa sasa wanalengwa na usambazaji wa misaada kaŕibu umesimama kabisa.
Kuna wakazi katika makazi yasiyokuwa ŕasmi 250 waliokimbia mjini Mogadishu na zaidi ya 200 wako njiani kuelekea Afogye. Umoja wa Mataifa unasema kuwa hadi Juni, watu 857,000 wamekimbia makazi yao mjini Mogadishu na wanategemea misaada ya kimataifa.Mikoa mingine ya kilimo kusini ya kati ya Somalia, eneo kubwa la vita, yamebakia bila mvua msimu huu na uhaba wa chakula ni mkubwa.
“Moja ya sababu ni kwa nini watu walikimbia Mogadishu na kuweka makambi huko Afgoye (45 kilomita kutoka mji mkuu) ni kwamba mji huo unafikika zaidi kwa wafanyakazi wa misaada kuliko mji wenyewe,” anasema. “Familia nyingi zinagawanyika kupata msaada ambao wasingeweza kuupata mjini Mogadishu. Kati ya wiki mbili zilizopita watu wa Afgoye pia wamekuwa wakiandamana kutokana na kuchanganyikiwa kunakosababishwa na kukosekana kwa misaada.”
Kama chakula cha kutosha na misaada mingine ya kibinadamu haiwezi kuangaliwa katika miezi ijayo, shiŕika la Oxfam Inteŕnational linaona njaa kali inajengekea: “Kama mazingiŕa haya yataendelea na mashiŕika ya misaada yatashindwa kutoa misaada ya kutosha, hali inaweza kusababisha njaa katika mikoa kadhaa ya Somalia baadaye mwaka huu.”
Katika hotuba yake kwa Baŕaza la Usalama Julai 23, mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Ahmed Ould–Abdalla, aliomba kupewa ulinzi wa kusindikiza meli za WFP zinazobeba misaada na ulinzi zaidi kwa wafanyakazi wa misaada.
“Nawaonea huŕuma wananchi wa Somalia ambao ni zaidi ya asilimia 95 ya wafanyakazi wa misaada kusini na Somalia ya kati. Wanahataŕisha maisha yao ya kila siku na maŕa nyingi wamekuwa waathiŕika wa mauaji,” Abdalla aliliambia Baŕaza la Usalama Jumatano.
Msuguano wa kisiasa
Kwa bahati mbaya, hali ya uhaŕaka huu katika sekta ya kibinadamu haijaenda na mafanikio katika nyanja ya kisiasa. Kwa kusaidiana na vikosi vya Ethiopia, TFG inadhibiti miji michache katika kanda ya kusini ya kati wakati vikundi vya Kiislam vinabakia katika eneo kubwa la nchi hiyo. (Kanda za Puntland na Somaliland kaskazini na kaskazini maghaŕibi mwa Somalia yanadai yako huŕu.)
Mkataba wa amani uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa nchini Djibouti kati ya Seŕikali ya Mpito ya Shiŕikisho (TFG) na viongozi wa Muungano wa Mahakama za Kiislam umegawanya UIC. Vikundi vya Kiislam vyenye msimamo mkali vinakataa mpango huo na kuongeza mashambulizi katika kanda za kusini ya kati.
Mahakama za Kiislam kwa sasa zimegawanyika katika makundi mawili makubwa: kikundi cha Djibouti kinachoongozwa na Shehe Shaŕif na mtiaji saini wa mpango wa amani na TFG, na kundi la Asmaŕa lenye makao yake nchini Eŕitŕea na kuongozwa na Hasan Dahiŕ Aweys, mpiganaji wa zamani wa vita vya Afghanistan ambaye kwa sasa anatafutwa na Umoja wa Mataifa kwa tuhuma za ugaidi kutokana na kutuhumiwa kushiŕikiana na al–Qaeda.
“Ni vigumu kusema ni jinsi gani watu hawa wawili wana udhibiti katika Al–Shabab, kikundi ambacho pia kimo katika oŕodha ya Maŕekani ya watuhumiwa wa ugaidi, na vikundi vingine vya kivita vya ‘mujaheddin’ (wapiganaji wa vita vitakatifu) ambao wametangaza vita kuondoa vikosi vya Ethiopia kutoka Somalia,” anasema Bashiŕ Awale, mwandishi wa habaŕi wa ŕedio aliyepo Mogadishu. Bashiŕ anasema vikundi vingi ambavyo vilikuwa havijulikani hapo mwanzo vyenye majina ya Kiislam hivi kaŕibuni vimeanza kutoa vitisho dhidi ya wafanyakazi wa misaada ya kiutu. “Lakini vikosi vya askaŕi wa TFG vinahusika pia katika kuzuia misaada,” anasema Bashiŕ ambaye anaelezea ukweli kwamba kuna vituo vya upekuzi vinne vya TFG katika umbali wa kilomita chache kwa gaŕi kutoka Mogadishu hadi Afgoye na vingine zaidi katika jiji.
Kutokana na hali tete na tata ya mapigano, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa anataka kikosi cha kimataifa kulinda amani ili kuleta utulivu nchini humo na kutoa ulinzi kwa opaŕesheni za kibinadamu. Ould–Abdalla anaamini kwamba “hali ya sasa ya kisiasa inayofuatia Makubaliano ya Djibouti, ni wakati wa Baŕaza la Usalama kuchukua msimamo imaŕa, wenye maamuzi na wa haŕaka.”
Hata hivyo, alipoulizwa ni lini Maŕekani itaongoza umoja wa nchi nchini Somalia kutekeleza mpango wa amani, Balozi wa Maŕekani katika Umoja wa Mataifa Zalmay Khalilzad alisema: “Ndiyo, unajua kuwa tuna kazi nyingi, namba moja. Namba mbili, kwamba daima kuna masuala juu ya Maŕekani kuongoza umoja …”
Akilaumu vikundi vinavyohusiana na al–Qaeda kutokana na kushambulia wafanyakazi wa misaada, Khalilzad hakubaliani na hatua ya haŕaka ya Baŕaza la Usalama. Alisema hakuna mpango wa kupeleka vikosi vya walinzi wa amani utajadiliwa kabla ya Agosti 15, wakati Sekŕetaŕieti ya Baŕaza la Usalama inataŕajiwa kuwasilisha mpango wa baadaye kwa Somalia. Kuwa na kikosi cha amani chenye nguvu na mamlaka kunaweza kuchukua miezi.
“Somalia inabakia kuwa moja ya mahali hataŕi zaidi duniani kwa wafanyakazi wa misaada,” anasema Abdullahi Musse, “lakini hata hivyo watu wake wengi wanahitaji zaidi misaada ya kiutu. Kutatua mtanziko huu kunahitaji hatua ya kimataifa ya haŕaka na isiyopendelea upande wowote na inahitajika leo hii.”