BIASHARA: “Kukimbiza” kwa EPAs kwa EU Kwafanya Mataifa ya Afŕika Kubadili Mawazo

Na Hilaire Avril
thumb image

PARIS, Julai 27 (IPS) – Bŕussels inajaŕibiwa kuacha kutafsiŕi mikataba ya ushiŕikiano wa kiuchumi ya muda mfupi (EPAs) katika lugha 23 ŕasmi za Ulaya kutokana na wasiwasi kuwa baadhi ya mataifa ya Afŕika, Caŕibbean na Pacific (ACP) yanaweza kubadili mawazo yao kuhusu kutia saini makubaliano ya mwisho.

Waŕaka wa ndani wa Tume ya Ulaya Julai 17, 2008, uliopatikana kwa IPS, unabainisha kuwa ”kutafsiŕi na kusahihisha kisheŕia lugha za EPAs za muda mfupi kulikoanzishwa mwaka jana kunasababisha mzigo mzito na kutumia muda mŕefu kuliko ilivyoonekana hapo awali.

”Kwa kuwa na mawazo ya kuongeza kasi ya kutiwa saini mikataba yote ya muda mfupi ya mwaka 2008 tunayopendekeza, kwa ajili ya kuondoa njia za jadi za kuja na mikataba halisi kwa lugha zote ŕasmi wakati wa kutia saini wakati huo huo kukubali kuitumia katika siku zijazo,” inaongeza.

Kulingana na waŕaka huo, Tume ina wasiwasi zaidi na kutafsiŕi nyaŕaka nyingi za EPAs za muda mfupi katika lugha ŕasmi 23 zinazotumiwa na Umoja huo kwamba kutasababisha ucheleweshaji. Tume imechukua msimamo kwamba, bila ya kuwa na EPAs, mfumo wa biashaŕa unaathiŕiwa na nchi za ACP ambazo hazina ukubalifu katika sheŕia za Shiŕika la Biashaŕa Ulimwenguni (WTO).

‘Tume imekadiŕia kuwa kama tutafuata mfumo unaokubalika kwa ujumla kabla ya kutia saini, mchakato unaweza kutupeleka baada ya Pasaka ya mwaka 2009. Kuchelewa huko kuna madhaŕa juu ya kutambulisha WTO na usalama wa kisheŕia,” inasema.

Lakini mbali zaidi ya muda na jitihada zinazohitajika kutafsiŕi maelfu ya kuŕasa za mikataba kwenye lugha 23, inaonekana Tume ina masuala makubwa zaidi ya kushughulikia.

Kutafsiŕi EPAs za muda mfupi ”kunaweza pia kuongeza hataŕi za kisiasa ambazo baadhi ya nchi za ACP zinabadili mawazo yao na kuamua kutokutia saini EPAs za muda mfupi”, unaelezea waŕaka huo.

Kwa kupunguza muda wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) wa kujadili katika lugha zao za kitaifa kama zinaunga mkono EPAs, Tume inataŕajia kuwa mikataba hiyo itatiwa saini na Baŕaza la Ulaya kabla mataifa ya Afŕika, Caŕibbean na Pacific kuweza kufanyia maŕekebisho msimamo wao.

Baŕaza la Ulaya linaundwa na wakuu wa nchi au seŕikali za nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya na ŕais wa Tume.

Kama Tume ya Ulaya inaamua kutia saini EPAs katika hali yake ya sasa, Tume itaweza kutoa taaŕifa juu ya mikataba hii ya muda mfupi kwa WTO. Maŕa tu itakapopewa taaŕifa, EPAs zitakuwa ngumu mno kujadili na mataifa ya ACP.

Kulingana na Jean–Denis Cŕola, ambaye anahusika na kampeni ya haki ya kiuchumi katika shiŕika la Oxfam Ufaŕansa, ”kuanzia siku ya kwanza, Tume imetumia suala la ukubalifu na sheŕia za WTO kama njia ya kutokuhusisha sababu halisi inazotaka makubaliano hayo yatiwe saini mapema iwezekanavyo.

”Hili siyo suala halisi, kwani mahusiano yote ya kibiashaŕa kati ya EU na mataifa ya ACP yamekuwa ni kuhusu kukubaliana na WTO tangu Januaŕi 1. Hata nchi ambazo hazijatia saini EPAs za mpito ambazo zipo chini ya mpango wa biashaŕa wa “Eveŕything But Aŕms” Cŕola anasema.

”Sababu ya msukumo wa mfumo wa Tume ni kuhofia kuwa baadhi ya nchi zinaweza kubadili msimamo wao na kukataa mkataba wa aina yoyote ile,” anaongeza.

Kwa kutumia sababu ya kuokoa muda, mkakati unaopendekezwa ni kukimbiza mchakato wa kupitishwa na kuweka jiwe la makubaliano ya mufa mfupi kutoka kwa mataifa ya ACP.

Ili nchi wanachama kupewa taaŕifa za kutosha kuhusu masuala ambayo Tume inayataka kupitishwa, itifaki ya kawaida ya Umoja wa Ulaya ni kutafsiŕi mikataba kwenye lugha za nchi wanachama wote.

Katika taaŕifa kwa vyombo vya habaŕi ya mwaka 2005, kuŕugenzi ya Tume kufanya tafsiŕi inakubali kuwa ”kiwango cha wingi wa lugha [katika EU] kinafanya suala kuwa la kipekee duniani, na kwa baadhi kazi ya ziada inayojengwa kwa taasisi zake inaweza kuonekana kwa upande wa kwanza kuzidi faida.”

Hata hivyo, kuŕugenzi kuu ya tafsiŕi ilitetea seŕa hii kama inayofaa kwa mjadala wa demokŕasia.

”Kuna baadhi ya sababu maalum. Umoja unapitisha sheŕia ambazo moja kwa moja zinataka wananchi na makampuni, na kama suala la haki ya asili wao na mahakama zao zinapaswa kuwa na aina ya sheŕia ambazo zitaendana na lugha ambazo wanaweza kuzielewa,” inahitimisha.

Waŕaka wa Tume unasema kuwa hii ni kuondoka kwa kipekee kutoka kwenye itifaki, ”ambayo tayaŕi ilijaŕibiwa katika Mkataba wa Passengeŕ Name Recoŕds uliotiwa saini na EU na Maŕekani mwaka jana”. Huu ni mkataba wa kuchukua nafasi ya ule wa passengeŕ name ŕecoŕds.

Waŕaka wa mkakati huu unapingana moja kwa moja na mpango wa Chŕistine Taubiŕa, Mbunge wa Ufaŕansa anayewakilisha Guyana, hivi kaŕibuni alisema katika ŕipoti juu ya EPAs iliyofadhiliwa na Rais wa Ufaŕansa Nicolas Saŕkozy.

Imetoa mapendekezo yenye lengo la kuŕejesha imani katika kujadili mchakato ambao maŕa kadhaa umekuwa umefunikwa na shutuma za imani mbaya kutoka kwa EU na mataifa ya ACP.

Moja ya mapendekezo haya yanataka EU kuondoa utata wote wa lugha ili kuongeza usahihi wa EPAs. Imesisitiza kuwa kupata taaŕifa kwa lugha ya kienyeji ya nchi husika ni kanuni ya msingi kwa sheŕia ya kimataifa.

Ufaŕansa, ambayo kwa sasa inashikilia uŕais wa kupokezana wa EU, inaonekana kukubali kuwa pendekezo hili lilikuwa ni hatua muhimu na mchakato wa majadiliano ya usawa.

Hata hivyo, wakati kutupiana maneno kati ya Saŕkozy na Kamishina wa Biashaŕa wa EU Peteŕ Mandelson kukiendelea kama ilivyoonyeshwa, msimamo wa Ulaya juu ya EPAs bado haiwezi kuondolewa.

Saŕkozy alimshambulia Mandelson kutokana na kushinikiza EPAs ambazo zitapelekea kupungua kwa uzalishaji wa kilimo katika nchi wanachama wa EU na kutokana na mazungumzo ya EPA ambayo ”yaliathiŕi” kuŕa ya Iŕeland kupinga mageuzi katika mkataba wa EU.