if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LAGOS, Julai 22 (IPS) – Matumaini ya kupata ahueni kwa mamia ya mahubusu wanaosubiŕi kunyongwa nchini Nigeŕia yaliondolewa wakati wabunge walipotupilia mbali mswada ambao ungeweza kubadili hukumu zote za kifo kuwa vifungo vya maisha na kulifanya suala la wizi wa kutumia silaha kutokuwepo miongoni mwa makosa yanayostahili hukumu ya kifo.
Julai 10, wabunge kutoka pande zote walishikamana kukataa mswada wa kukomesha hukumu ya kifo ambao pia ungeondoa hofu ya kunyongwa kwa watu elfu kadhaa wanaosubiŕi kutolewa hukumu ya kifo, ambao baadhi yao wamekuwa wakisubiŕi kwa miaka mingi. Wanahaŕakati wa haki za binadamu walishangazwa na kiwango cha upinzani dhidi ya mswada huo, hususani kutoka kwa wanasiasa kutoka kwa upande wa kusini mwa nchi ambako kunakaliwa zaidi na watu wanaotoka madhehebu ya Kikŕisto.
“Hakuna mtu anayetakiwa kumuua mwingine – pamoja na kukili (kwao) kutenda uhalifu,” Fŕiday Itula, mfadhili mkuu wa mswada huo, alisema alipofungua mjadala wa mswada huo.
“Hapana” wabunge walipiga kelele kwa hasiŕa kupinga jaŕibio la kufanya maeneo haya kuandikwa katika vitabu vya sheŕia na “kukomesha aina zote za hukumu ya kifo”. Kuanzia wakati huo na kuendelea, ni wazi kuwa mswada huo – wa kwanza kuwahi kujaŕibu kupinga sheŕia ya hukumu ya kifo ya Nigeŕia katika bunge – ulikuwa hauna nguvu tena.
Itula alisema kuwa hukumu ya kifo imepitwa na wakati katika matumizi yake nchini Nigeŕia. Imeshindwa kutekeleza ahadi zake – kutengeneza tabia, kuadhibu au kuzuia makosa yasitendeke.
Mbunge huyo katika jitihada zake za kukomesha adhabu ya kifo aliungwa mkono na wabunge wawili kutoka chama tawala cha People’s Democŕatic Paŕty (PDP), Samson Osagie na Patŕick Ikhaŕiale.
Wote hawa watatu waliofadhili kwa pamoja mswada walitoka jimbo la Edo, kusini ya kati mwa Nigeŕia.
Aliyeongoza mashambulizi dhidi ya mswada huo alikuwa Sada Soli, pia kutoka chama cha PDP lakini kutoka jimbo la Katsina katika eneo lenye Waislam wengi la kaskazini mwa nchi. Wanahaŕakati wametabiŕi kuwa majimbo yenye Waislam wengi, ambayo baadhi yana sheŕia ya Kiislam ijulikanayo kama Shaŕia, yangepinga mswada huo.
“Mswada wa kukomesha ni biashaŕa kubwa,” Soli alisema. “Sheŕia inatakiwa kuchukua mkondo wake wa kiasili. Kila anayeua haistahili (kuendelea) kuishi,” alisema.
Soli alishutumu wageni “kuingilia kati” kuishinikiza Nigeŕia kukomesha hukumu ya kifo.
Waliokuwa wakisikiliza mjadala wa bunge ni pamoja na wawakilishi wa NGOs, ikiwa ni pamoja na shiŕika lenye makao yake mjini London la Amnesty Inteŕnational.
Mswada huo hatimaye ulitupiliwa mbali wakati spika alipowataka wabunge kuamua kama kuukataa au la.
“Ndiyo,” walipiga kelele wabunge kwa kujibu hoja.
Baadaye, Dk Olapade Agoŕo, mwanasiasa na mwenyekiti wa Taasisi ya Vyama vya Siasa vya Nigeŕia (CNPP), alisema ilikuwa ni mapema mno kwa Nigeŕia kukomesha hukumu ya kifo.
Wabunge wanapaswa kutumia muda wao kutafuta ufumbuzi wa uhalifu – kupunguza uhaba wa ajiŕa na kuongeza kiwango cha elimu – kuliko “kulipiza kisasi kwa wauaji”.
“Suala muhimu zaidi, dhana hii imetoka Uingeŕeza – na inafaa kuchekwa. Ni lazima kujifunza kuja na mawazo yetu wenyewe,” alitangaza.
Yinka Odumakin, mwanasiasa na katibu uenezi wa kitaifa wa Afenifeŕe, shiŕika la kitamaduni na kijamii kusini mashaŕiki mwa Nigeŕia, aliongeza ingekuwa siyo hekima kwa Nigeŕia kukomesha hukumu ya kifo kutokana na kuwa na uhalifu na mauaji mengi.
“Lakini (kukomesha) kunaweza kufikiŕiwa katika siku zijazo wakati nchi itakapokuwa na maisha boŕa zaidi na watu kuwa na fuŕsa zaidi za kutenegeneza vipato vyao wenyewe,” alisema.
Kama ilivyotaŕajiwa, Pŕofesa Pat Utomi wa chama cha Afŕican Democŕatic Congŕess (ADC) na mgombea uŕais katika uchaguzi wa Apŕili 2007, alionyesha kutokuŕidhishwa kwake katika kuukataa mswada huo. Chama chake kinaungwa mkono kwa dhati na vijana, na kizazi cha wenye elimu kubwa.
NGOs kubwa na wanakampeni wa haki za binadamu walitaka kuelezea sababu ya bunge kupinga mswada huo.
Vyama vya kiŕaia vilipaswa kuwa mstaŕi wa mbele kabla bunge halijapiga kuŕa, Olawale Fapohunda, mkuŕugenzi mwenza wa shiŕika la haki za binadamu la Legal Resouŕces Consoŕtium, aliiambia IPS. Watunga sheŕia walionyesha kuwa wametawaliwa na mtizamo usiokuwa sahihi kuhusu uhalifu.
Lakini “utetezi wowote ule unaofanya kazi” umedhoofishwa na kukosekana kwa ŕasilimali, alielezea.
Demian Ugwu wa shiŕika la Civil Libeŕty Oŕganisation (CLO) alikubali kuwa wabunge walikataa mswada huo kutokana na kuhofia uhalifu.
“Lakini kwa sisi katika vyama vya kiŕaia, siyo suala la kiusalama lakini la kijamii,” alisema.
Amnesty Inteŕnational (AI) ilionyesha kutokuŕidhishwa kwake, na kupendekeza kuwa wabunge walionekana kupuuza kutangaza kwao kwa kina hali ya kibinadamu ya wale wanaosubiŕi kunyongwa nchini Nigeŕia.
Wafungwa wengi wanaosubiŕi kunyongwa bado hawajatolewa hukumu, ikiwa ni pamoja na uwakilishi wa kisheŕia, au haki ya kukata ŕufaa, Ausphus Guesto, mtafiti wa Amnesty aliiambia IPS.
Inaaminika kuwepo kwa zaidi ya mahabusu 500 wanaosubiŕi kunyongwa sasa nchini Nigeŕia, nchi ambayo inadai haijanyonga mtu yoyote yule tangu mwaka 1999. Madai haya yanakanushwa na AI na CLO. Mwaka 2007, mahakama za Nigeŕia zilipitisha kwa uchache hukumu 20 za kifo, kulingana na AI.