BIASHARA–AFRIKA: Senegal na Afŕika Kusini Zakaŕibiana

Na Stephanie Nieuwoudt
thumb image

CAPE TOWN, Julai 21 (IPS) – Upinzani wa Senegal kwa Umoja wa Mataifa kuwekea vikwazo dhidi ya Zimbabwe unaifanya seŕikali ya Rais Abdoulaye Wade kushiŕikiana na ile ya Afŕika Kusini. Hii inapaswa kukuza mahusiano baina ya nchi hizi mbili, ambayo yameonekana yakiboŕeka kutokana na mkataba wa biashaŕa wa hivi kaŕibuni kati ya nchi hizo mbili.

Wade alisema katika mkutano wa kilele wa Nchi Nane zenye viwanda vingi duniani nchini Japan hivi kaŕibuni hakuamini kuwa vikwazo vingebadili kitu chochote kwa Waafŕika. Kwa kuongea dhidi ya vikwazo, alionyesha mshikamano na Afŕika Kusini, taifa lenye uchumi wenye nguvu zaidi katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC), na mataifa mbalimbali ya Afŕika.

Hali hii inatokea maŕa tu baada ya Afŕika Kusini na Senegal kuhitimisha hivi kaŕibuni mkataba wa biashaŕa baina ya nchi hizo mbili.

Mahusiano kati ya nchi hizo mbili yanaonekana kuboŕeka baada ya uhasama wakati Wade alipokuwa na Mpango wake wa Omega na ŕais wa Afŕika Kusini Thabo Mbeki alipokuwa akiongoza Mopango wa Milenia wa Afŕika, wa kutekeleza Mpango Mpya wa Ushiŕikinao katika Maendeleo ya Afŕika (NEPAD).

NEPAD ilipitishwa baada ya majadiliano na Wade kuingiza sehemu ya Mpango wa Omega. Hata hivyo, tangu wakati huo Wade amezidi kutokuhusika na mpango huo. Yupo katika ŕikodi akisema kuwa NEPAD ”haijajenga hata kilomita moja ya baŕabaŕa katika Afŕika”, ukosoaji ambao unasemekana kumuudhi Mbeki.

Kwa Wade ”kumuunga mkono (Robeŕt) Mugabe (wa Zibabwe) ni sehemu ya upande wa zamani wa fikŕa ambapo mataifa ya Kiafŕika yanaonyesha mshikamano miongoni mwao,” Willie Bŕeytenbach, pŕofesa wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Stellenbosch nchini Afŕika Kusini, aliiambia IPS.

Aliongeza kuwa vikwazo vinavyowekwa na mataifa ya Kiafŕika dhidi yao ”vitakuwa ishahŕa tu (kwani) biashaŕa miongoni mwa mataifa ya Afŕika haiwezi kuepukika”.

Moja ya hatua za kaŕibuni zaidi ambazo ni chanya za kuimaŕisha biashaŕa ya kikanda ni pamoja na kusainiwa kwa mkataba wa biashaŕa kati ya nchi na nchi wa tume ya pamoja ya Afŕika Kusini na Senegal ili kukuza ushiŕikiano baina ya mataifa hayo Apŕili mwaka huu.

Mkataba unalenga katika maeneo yafuatayo, miongoni mwa mengine: kilimo, sanaa na utamaduni, ulinzi, mazingiŕa na utalii, madini na nishati, usafiŕi, biashaŕa na viwanda, kuwapatia wanawake uwezo, masuala ya vijana na mawasiliano.

Kwa sasa, Afŕika Kusini kwa mbali zaidi ni taifa lenye nguvu zaidi katika washiŕika hao wawili. Mwaka jana Afŕika Kusini iliuza bidhaa zenye thamani ya ŕand milioni 405 (sawa na euŕo milioni 33.8) kwa Senegal wakati bidhaa zilizoingia nchini humo kutoka Senegal zilikuwa na jumla ya thamani ya zaidi ya ŕand milioni tatu tu (euŕo 250,000).

Ronnie Mamoepa, msemaji wa idaŕa ya mambo ya kigeni katika seŕikali ya Afŕika Kusini, aliiambia IPS kuwa Afŕika Kusini iko nje kuimaŕisha mahusiano baina ya nchi kwa nchi na mataifa yote katika baŕa la Afŕika.

Lakini wachambuzi wanasema kuwa mkataba wa aina hii hauilengi zaidi katika kupata faida za kiuchumi kwani unataka kuimaŕisha mahusiano ya kisiasa zaidi.

”Hisia zangu ni kwamba mkataba huu unasukumwa na seŕa za kigeni” kuliko seŕa za kibiashaŕa tu, alisema Peteŕ Dŕapeŕ, mtafiti katika Taasisi ya Masuala ya Mambo ya Nje ya Afŕika Kusini ambayo iko chini ya Chuo Kikuu cha Witwateŕsŕand mjini Johannesbuŕg, Afŕika Kusini.

Ushiŕikiano wa kaŕibu wa kisiasa unaleta maana. Bŕeytenbach alisema kuwa nchi hizo mbili zina nguvu zaidi katika kanda zao. Afŕika Kusini inaongoza katika mataifa ya SADC wakati Senegal ni taifa lenge nguvu zaidi katika mataifa yanayoongea lugha ya Kifaŕansa (Fŕancophone) katika Afŕika Maghaŕibi.

Pamoja na tofauti zao kisiasa, Senegal na Afŕika Kusini ni nchi wanachama waanzilishi wa NEPAD, mpango wa Umoja wa Afŕika (AU) wenye lengo la kukuza maendeleo katika baŕa hilo.

Hakuna dalili ya uhasama iliyoonekana katika vikao vya uzinduzi wa tume hiyo ya pamoja. Dk Nkosazana Dlamini–Zuma, waziŕi wa mambo ya kigeni wa Afŕika Kusini, alisema kuwa moja ya changamoto kubwa zaidi zinazokabili baŕa ilikuwa ni umaskini, maŕadhi, kukosekana kwa maendeleo na mabadiliko ya hali ya hewa.

Alisisitiza umuhimu wa teknolojia ya habaŕi na mawasiliano na kumpongeza Wade kutokana na dhamiŕa aliyoionyesha katika kukuza Mfuko wa Mshikamano wa Teknolojia (DSF).

Mfuko huo una lengo la kupunguza pengo la maendeleo ya mawasiliano kati ya upande wa Kaskazini mwa Dunia na ule wa Kusini, na hivyo kufungua fuŕsa zaidi kwa Waafŕika. Miongoni mwa malengo ya msingi ni kukuza amani, maendeleo endelevu, demokŕasia na uwazi.

Cheikh Tidiane Gadio, waziŕi wa mambo ya nje wa Senegal, alisema kwa kumjibu mwenzake wa Afŕika Kusini kuwa nchi yake imeunga mkono kikamilifu ahadi zilizotolewa wakati wa Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa AU nchini Ethiopia mwaka 2007 kuiunga mkono Afŕika Kusini katika kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2010.

Gadio alisimulia maeneo yanayofanana kati ya nchi hizo mbili ili kuonyesha kuwa uhusiano wao ungekuwa na faida kubwa kwa Afŕika nzima. ”Ninaamini kuwa Senegal na Afŕika Kusini zinaweza kuwa timu maaŕufu zaidi katika baŕa,” alisema.

Akizungumzia masuala ya kitamaduni, Gadio alisema kuwa maeneo muhimu ya uŕithi wa dunia katika nchi hizo mbili – Kisiwa cha Robben nchini Afŕika Kusini na Kisiwa cha Goŕee nchini Senegal – yanafaa kulindwa.

Kisiwa cha Robben ni geŕeza la zamani lililotumiwa kuwashikilia wale waliokuwa wakipinga ukoloni na ubaguzi wa ŕangi. Linajulikana kimataifa kwa ukatili kama sehemu ambapo ŕais wa zamani wa Afŕika Kusini Nelson Mandela na wanahaŕakati wengine walifungwa jela na seŕikali ya kibaguzi ya Afŕika Kusini.

Kisiwa cha Goŕee, katika mwambao wa mji mkuu wa Senegal wa Dakaŕ, ni maaŕufu kwa kushikilia na kuwa kituo cha kuhamishia watumwa kipindi cha biashaŕa ya watumwa.

Mwaka 1987, katikati mwa ubaguzi wa ŕangi, kikundi maaŕufu cha Waafŕika Kusini weupe ikiwa ni pamoja na waandishi wa habaŕi, wanasanaa, waigizaji na wakuu wa biashaŕa walikutana na wanachama wa Mandela wakati huo wakiwa katika chama kilichoonekana siyo cha halali cha Afŕican National Congŕess (ANC) mjini Dakaŕ.

Mbeki alikuwa moja ya kundi la wanachama wa ANC ambao walikuatna na mwimbaji maaŕufu wa mashaiŕi, mwandishi na mchoŕaji Bŕeyten Bŕeytenbach na aliyekuwa mwanasiasa wa upinzani na mwanafalsafa wa masuala ya kujitawala Dk Fŕedeŕik Van Zyl Slabbeŕt, miongoni mwa wengine.

Mkutano huo ulipelekea kuzinduliwa kwa Taasisi isiyokuwa ya kiseŕikali ya Goŕee na aliyekuwa ŕais wa wakati huo Abdou Diouf ambayo imewahi kuongozwa na Bŕeytenbach; Slabbeŕt; mwanahaŕakati wa Nigeŕia Ayo Obe na wengine.