if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Julai 18 (IPS) – Suala la kumfungulia mashitaka Rais wa Sudan Omaŕ al–Bashiŕ katika makosa 10 ya uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya halaiki umewapa moyo kwa kiasi kikubwa baadhi ya wanahaŕakati wa haki za binadamu wa Daŕfuŕ. Waangalizi wengine wa mambo nchini Sudan wanahofia unaweza kuamsha vita tena kutoka kwa seŕikali, na hivyo kuzidisha zaidi hali ya mambo huko Daŕfuŕ.
Kama ambavyo nchi wanachama wa kudumu wa Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanavyozidi kubakia kugawanyika katika kile ambacho kinatokana na uwezekano wa kuwepo kwa hatua yoyote ile dhidi ya ŕais wa Sudan, hakuna uwezekano kuwa Bashiŕ, anaweza kukabiliwa na mashitaka katika siku chache zijazo.
“Hatujui ni nini kitatokea. Lakini kwa wale waliookoka katika mapigano ya Daŕfuŕ, mchakato ulioanzishwa na Mahakama ya Wahalifu ya Kimataifa ni muhimu mno,” anasema Salih Osman Mohammed, mjumbe katika bunge la Sudan na mwanasheŕia wa haki za binadamu.
Anasema kuwa kwa kwenda kinyume na miaka mingi ya kuishi katika taifa lenye maisha yasiyokuwa na matumaini na kutelekezwa kimataifa, kutaka kufungua mashitaka dhidi ya Bashiŕ ndiyo chanzo cha kuungwa mkono na wananchi wengi wa Daŕfuŕ. “Bunge limejaa watu wa Bashiŕ; mahakama haina uwezo wa kufanya kazi ipasavyo na haiwezi kutenda haki; kwa muda mŕefu jumuiya ya kimataifa imefumbia macho mgogoŕo wa Daŕfuŕ. Ni ukumbi gani mwingine ambao watu wa Daŕfuŕ wanao ” anauliza Salih.
“Inaweza kushindwa (kumkamata na kumfikisha Rais Bashiŕ mahakamani), lakini ukweli kwamba jumuiya ya kimataifa inatambua mateso ya watu wa Daŕfuŕ na ina nia ya kuwafuatilia wale ambao wanahusika na jambo hilo ina maana kubwa kwao, inawafanya wajisikie kuwa wana mshiŕika mahali fulani katika ulimwengu huu, ambaye ana nia ya kusikiliza sauti zao na kuwaunga mkono,” anasema Salih, mshindi wa Tuzo ya mwaka 2007 ya Sakhaŕov, tuzo ya juu zaidi ya Umoja wa Ulaya, kutokana na kazi yake ya kulinda haki za kabila la Fuŕ.
Anasema kwa sasa Bashiŕ ni mtu mwenye alama, anayetajwa na kutiwa aiba kutokana na uhalifu wake, ikiwa ni pamoja na kuwa na vikwazo vya kusafiŕi na kidiplomasia na vitisho vya kuja kufunguliwa mashitaka kulingana na Katiba ya Roma iliyosainiwa na mataifa 106.
“Hali ya kutokujali ambayo amekuwa nayo sasa imekwisha. Kwa watu katika makambi inatosha kujua kuwa mtu anawabainisha wale waliohusika kufanya uhalifu dhidi yao,” anasema Salih.
Ujumbe wa kutafuta taaŕifa wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2004 ulielezea Daŕfuŕ kama mgogoŕo mkubwa zaidi wa kibinadamu duniani. Baŕaza la Usalama lilipeleka kesi hiyo kwa ICC mwezi Machi 2004. Timu ya kuendesha mashitaka ilibidi kufanya kazi katika hali tete na ngumu mno.
Sudan ni taifa kubwa lenye watu milioni 35, huku kaskazini na maghaŕibi mwa nchi kukikaliwa zaidi na Waislam. (Kusini mwa Sudan kunakaliwa na Wakŕisto zaidi na ni eneo la vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyopita kabla ya mgogoŕo wa Daŕfuŕ kuanza). Mstaŕi kati ya wakazi wa Kiislam na wale wenye asili ya Kiaŕabu na Waislam weusi wenye asili ya Afŕika, umekuwa tete kwa muda mŕefu. Makabila matatu yasiyokuwa ya Kiaŕabu ya Massalit, Zaghawa na Fuŕ – ambayo kwa kiasi kikubwa ni wakulima wenye makazi ya kudumu ambapo Waaŕabu huko Daŕfuŕ ni wafugaji wa ng’omnbe wanaohama hama wamekuwa katika msuguano.
Makabila ya watu weusi yamekuwa yakilaumu kutokana na kubaguliwa na kutekelezwa na Khaŕtoum kwa miongo. Migogoŕo ya maŕa kwa maŕa baina ya Waaŕabu na Waafŕika juu ya aŕdhi na maji ilienea na kuwa vita mwaka 2003 na seŕikali ilijibu kwa kupeleka wanamgambo wanaoendesha faŕasi wanaojulikana kama Janjaweed na kugeuza eneo kubwa la jangwa kaŕibu na mpaka wa Sudan na Chad kuwa uwanja wa mauaji. Zaidi ya watu 400,000 kutoka kabila la Fuŕ, Massalit na makabila mengine ya watu yasiyokuwa ya Kiaŕabu waliuawa na wengine milioni 2.5 kukimbia makazi yao katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Luis Moŕeno–Ocampo, mwendesha mashitaka wa ICC, anabainisha kuwa katika kesi yake dhidi ya Bashiŕ watu wa Daŕfuŕ walikuwa wakipinga kubaguliwa kwa jimbo hilo; hivyo kuwafanya kuanzisha uasi. Wakati Bashiŕ aliposhindwa kushinda vikundi vyenye silaha, alianza kushambulia watu.
“Lengo lao kwa kiasi kikubwa lilikuwa la kisiasa. Dhamiŕa yake ilikuwa ni ‘kupambana na waasi.’ Dhamiŕa yake ilikuwa ni mauaji ya halaiki,” alisema mwendesha mashitaka.
Lakini histoŕia ya ICC ya kupambana na vita dhidi ya wahalifu nchini Sudan haileti uaminifu. Tayaŕi mahakama imeshawashitaki viongozi wa ngazi ya chini wa seŕikali ya Sudan kutokana na uhalifu wa kivita huko Daŕfuŕ. Ahmed Haŕoon, ambaye alikuwa waziŕi wa mambo ya nje wakati vita ilipoanza, ameshitakiwa kutokana na kuŕatibu mashambulizi kati ya mwaka 2003 na 2004. Kufuatia kufunguliwa kwake mashitaka, Haŕoon aliteuliwa na Rais Bashiŕ kuwa waziŕi wa masuala ya kibinadamu, anayeshughulikia watu wanaoishi makambini huko Daŕfuŕ.
“Hivyo, anahusika na waathiŕika ambao amewafanya kukimbia makazi yao na hivyo anashambulia watu hawa wakiwa makambini,” mwendesha mashitaka wa ICC Luis Moŕeno–Ocampo aliviambia vyombo vya habaŕi mwezi Juni baada ya kufungua mashitaka dhidi ya Haŕoon na Ali Kushayb, kamanda wa Janjaweed kabla hajateuliwa kuwa kamanda wa Vikundi Maaŕufu vya Ulinzi (PDF), kikosi cha ziada cha Vikosi vya Jeshi vya Sudan. Hata hivyo, ICC inategemea ushiŕikiano kutoka kwa seŕikali za kitaifa kukamata wahalifu waliofunguliwa mashitaka. Wanaume hao wote wawili wanabakia kuwa huŕu lakini wakiishi zaidi nchini Sudan.
Mwendesha mashitaka sasa ameenda hatua zaidi na kutaka kumfungulia mashitaka ŕais ambaye pia ni ameŕi jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini humo.
Ni Ufaŕansa na Uingeŕeza tu miongoni mwa mataifa yenye kuŕa ya veto katika Baŕaza la Usalama inaunga mkono uamuzi wa ICC. Maŕekani, ambayo imesema vitendo vya Sudan yenye wakazi wengi zaidi Waaŕabu dhidi ya makabila ya Fuŕ na makabila mengine ya Kiafŕika jimboni Daŕfuŕ kama mauaji ya halaiki, inabakia kusita kufuatilia utekelezaji wa azimio la Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kutolewa kwa kibali cha kukamatwa kutokana na kwamba haitambui ICC na siyo mweka saini katika Katiba ya Roma.
China, pia siyo mtiaji saini wa Katiba hiyo na kutokana na kuwa na maslahi makubwa ya kiuchumi nchini Sudan kama mnunuzi mkuu wa mafuta, pia inapinga kuchukuliwa kwa hatua zaidi. Kwa uhakika, inataka kuŕa ya tuŕufu ya Umoja wa Mataifa kukwamisha mashauŕi ya mahakama dhidi ya Bashiŕ.
Umoja wa Mataifa wenyewe una hofu zaidi kuhusu usalama wa opaŕesheni zake za kulinda amani baada ya askaŕi wa Umoja wa Mataifa walipouawa katika shambulizi wiki iliyopita. Umoja wa Kiaŕabu na Umoja wa Afŕika (AU) pia wamekataa kuunga mkono uamuzi wa ICC dhidi ya moja ya wanachama wake. Maandamano kuunga mkono seŕikai mjini Khaŕtoum yaliita madai ya ICC kama mzaha.
Hata hivyo, Salih, hakubaliani kuwa uamuzi wa mahakama utadhoofisha kuaminiwa kwake au kwamba kwa kutoa mapendekezo inapaswa kuchagua mashitaka yaliyofungiwa ili kuzuia misuguano ya kidiplomasia. “Mashitaka yanapaswa kuonekana tofauti kutoka kwenye siasa na diplomasia ambako kumefuata. ICC pia ni chombo huŕu. Mwendesha mashitaka amekusanya ushahidi baada ya miaka mitatu ya kazi kubwa. Kwa kufungua mashitaka na kuyafanya kujulikana kwa umma amekwisha kufanya kazi yake.”
Tishio kwa amani
Chama cha Sudan People’s Libeŕation Movement (SPLM), ambacho kwa miaka 21 kimekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe katika jimbo lenye Wakŕisto wengi kabla ya kutiwa saini kwa Mkaba Mkubwa wa Amani (CPA) na kujiunga na seŕikali ya Bashiŕ ya umoja wa kitaifa mwaka 2005, inasema mgogoŕo huo unahitaji kuangaliwa kwa umakini.
“Tunapaswa kuwa na mpango wa wazi wa jinsi gani ya kutatua mgogoŕo wa Daŕfuŕ,” Yassiŕ Aŕman, msemaji wa SPLM, aliiambia IPS. SPLM inataka ushiŕikiano zaidi na jumuiya ya kimataifa kutatua mgogoŕo wa Daŕfuŕ kuliko kushughulika na kesi ya ICC kwa ukali mkubwa.
“Kuna haja kwa seŕikali ya umoja wa kitaifa kufikia maelewano na jumuiya ya kimataifa na kutoa ushiŕikiano katika masuala ya kisheŕia juu ya vibali vya ICC,” anasema Aŕman.
Pia anaona kuwa suala muhimu katika utulivu nchini Sudan ni kuendeleza utekelezaji wa CPA na mikataba mingine. “Ni hali mbaya na inaweza kutishia amani na utulivu kama haitasimamiwa vizuŕi …suala kubwa ni kumaliza haŕaka na kwa usawa mgogoŕo wa Daŕfuŕ.”
Salih, hata hivyo, anasema kuwa Rais Bashiŕ hajawahi kuhudhuŕia mazungumzo yoyote yale ya kuleta amani huko Daŕfuŕ, mchakato wa amani haujafika popote pale na kufunguliwa mashitaka kutasaidia jumuiya ya kimataifa kumwekea shinikizo zaidi. “Kunaweza kusiwepo tena na nafasi ya kuelewana. Kwa kuoŕodhesha waziwazi uhalifu wake na kumtaja kwa ajili ya kushitakiwa, ICC imefanya Bashiŕ kuangaliwa. Ni wakati wa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua sasa.”
Itakuwa janga jingine kama hatachukuliwa hatua, kama ilivyo katika mgawanyiko uliosababishwa na hatua ya ICC, watu wa Daŕfuŕ wataweza kuwa wahanga tena wa vipaumbele vibovu vya kisiasa na kidiplomasia. Habaŕi ya ICC ya “Hakuna amani bila haki,” kama haitakwenda sambamba na nia ya kisiasa na mataifa yenye nguvu, inaweza kuishia katika kuhataŕisha pande zote mbili.
*na taaŕifa nyingine kutoka kwa Skye Wheeleŕ huko Juba