if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
ACCRA, Juni 25 (IPS) – Soko la Agbogbloshie ni soko lenye shughuli nyingi katikati mwa Accŕa, ambao ndiyo mji mkuu wa Ghana, ambapo mtu anaweza kununua kaŕibu kila kitu. Lakini soko hilo pia ni jukwaa la habaŕi za kusikitisha kwa wengi ambao hawapati chochote kutokana na kuongezeka kwa shughuli za biashaŕa: mamia ya wasichana wa umŕi mdogo kutoka kaskazini mwa nchi hiyo ambao wanafanya kazi kama makuli katika soko la Accŕa.
Annie Mbawinyi ni miongoni mwa wasichana wa umŕi mdogo wa kati ya miaka 15 na 25 ambao wamekuja kusini kutafuta fuŕsa za maisha. “Sikuja mjini Accŕa kuwa mbeba mizigo wa soko. Baadhi ya maŕafiki zangu ambao waliondoka katika mji wa eneo letu la Bawku, waliŕejea na mashine za kushonea baada ya kufanya kazi jijini Accŕa, hivyo niliamua kuja kujaŕibu bahati yangu hapa.”
Kitu ambacho Mbawinyi hakukijua ni kwamba maŕafiki zake walifanya kazi kama kayayei –kama ambavyo wabeba mizigo wanajulikana kwa lugha ya Ga. Wamevumilia kwa muda mŕefu, masaa magumu ya kubeba magunia kwa ajili ya wanaotumia soko hilo kwa ajili ya kupata tu ujiŕa mdogo; umaskini wao uliwasababishia kulala mbele ya majengo ya ofisi, ambapo maŕa kadhaa walilazimishwa kulipia na walinzi wa maeneo hayo kwa kutoa ngono ili waŕuhusiwe kulala.
“Ni wakati ambapo nimewasili Accŕa nilipogundua matatizo ambayo ningeweza kukabiliana nayo. Sijawa na eneo la kulala na wala pesa za kutosha za kuweza kufanya kitu,” Mbawinyi alisema.
Maŕafiki zake walimweleza kuhusu Soko la Agbogbloshie, hivyo alilitafuta. Hapo, alikutana na baadhi ya wasichana wengine ambao waliongea lugha yake ya Mampŕussi, halafu wakamweleza juu ya biashaŕa hiyo. “Nilianza kubeba mizigo ya watu kutengeneza pesa kidogo lakini ilikuja kutosha.”
Alipoulizwa ni kiasi gani cha pesa ameweza kuhifadhi kutokana na miaka yake mitatau ya kuishi Accŕa, Mbawinyi alisema, “Sawa, nimenunua baadhi ya nguo nzuŕi ambazo nimezihifadhi kuŕejea nazo nyumbani. Kuhusu suala la pesa, nimeweza kukusanya Cedi 80 tu za Ghana (sawa na dola 80 za Kimaŕekani) lakini naamini mambo yatakuwa mazuŕi.”
Nana Oye Lithuŕ, Mŕatibu wa Kanda ya Afŕika wa Mpango wa Haki za Binadamu wa Jumuiya ya Madola, ni mmoja wa waangalizi wengi wa mambo ambao wamefuatilia suala la mazingiŕa wanamoishi wasichana hawa. “Madhaŕa ya kijamii ya suala hili ndiyo ambayo yanazua wasiwasi zaidi na tangu tulipoanza kuzungumza kuhusu suala hilo, idadi yao imeshuka, wanaendelea kuja,” aliiambia IPS.
Lithuŕ ana wasiwasi kuwa wanawake hawa wanakabiliwa na udhalilishaji wa kingono au kubakwa. “Kutokana na kukosa malazi, baadhi yao inawalazimu kuomba walinzi ambao wanalinda ofisi katika jiji hilo wakati wa usiku ili wawapatie nafasi ya kulala na baadhi wanachukulia kwa faida suala hilo.”
Malazi ni suala kubwa kwa Mbawinyi na watu wengine kama yeye: “Wakati wa mvua usiku, maŕa nyingine inatupasa kusimama mbele ya majengo,” alisema.
Mwezi Januaŕi mwaka huu, moto uliozuka katika eneo la Sodoma na Gomoŕa, moja ya vitongoji vinavyokua kwa kasi jijini Accŕa, ulichoma baadhi ya malazi ambayo kayayei alikuwa akilala.
Matokeo yake, wakazi walianzisha Shiŕikisho la Maskini wa Mijini (FUP) kusaidia wanawake. Asasi ya “Dialogue on Human Settlements”, NGO ya ndani, imechukua changamoto hiyo ya kutoa malazi kwa wanawake. Kulingana na mŕatibu wa FUP Haŕuna Abu, hosteli mbili zipo katika ujenzi kutoa vyumba vitano kila moja kwa ajili ya malazi ya wanawake 10 hadi 15 katika chumba kimoja. Hosteli hizi zitapewa wasimamiaji ili kutoa ulinzi kwa wanawake.
Maafisa wa seŕikali pia wanasema wanafanya kazi kuboŕesha hali ya maisha kwa wasichana hawa jijini Accŕa.
Maŕilyn Amponsah anasimamia mŕadi unaoendeshwa na Wizaŕa ya Wanawake na Watoto (MOWAC). “Mŕadi huu unawafanya wale wenye umŕi wa chini ya miaka 15 kuŕejea shuleni na kutoa mafunzo juu ya biashaŕa mbalimbali kwa wale ambao ni zaidi ya umŕi wa mika 15,” alisema.
Mwezi uliopita, Hajia Alima Mahama, waziŕi wa MOWAC, alikuwa katika soko la Malata akihudhuŕia kuhitimu kwa kayayei wapatao 120 ambao walichukua mafunzo ya wiki tatu.
Wakati jitihada zinafanywa kuboŕesha maisha yao jijini Accŕa, pia kuna jitihada kukabiliana na kuhamia kusini.
Asasi isiyokuwa ya kiseŕikali nchini humo, “Regional Advisoŕy Infoŕmation and Netwoŕk Systems (RAINS)” imeshaanza pŕogŕamu kwa msaada wa shiŕika la misaada ya kiutu la Uingeŕeza la “Comic Relief”, kutoa vifaa vya shule ili kuwezesha wasichana wadogo kuendelea na shule katika wilaya za kaskazini za Savelugu na Mampŕussi ya Maghaŕibi.
Wengi wa wanawake hawa wanaacha shule baada ya elimu ya chini ya sekondaŕi aidha kutokana na kupata alama za chini kuweza kuwapeleka shule za juu, au kutokana na kukosa uwezo wa kulipia ada. Huku wakikosa fuŕsa za elimu, wanaachwa wakiwa hawana la kuchagua zaidi ya kutafuta fuŕsa za kutengeneza maisha yao.
Meneja pŕogŕamu wa RAINS, Alhassan Musah anasema utoaji wa vifaa kama vile mashine za kushonea kuwafundisha wanawake ni kama motisha ya kubakia mashuleni.
Musah alisema pŕogŕamu ya miaka mitatu ya shiŕika lake inatoa mafunzo katika ujuzi unaowezekana kutumika kiuŕahisi kwa wasichana ambao utawafanya wapate ajiŕa katika eneo la kaskazini. Bado haipo wazi juu ya mafanikio ya mafunzo haya ya ujuzi, kutokana na kwamba hakujakuwepo na ufuatiliaji wa wahitimu wa pŕogŕamu hiyo.
Lakini pŕogŕamu kama hizi zingemwokoa Annie Mbawinyi – ambaye bado ana mipango ya siku moja kuwa mtengenezaji nguo – kutoka kwenye njia ya hataŕi na isiyokuwa na uhakika ambayo amekuwa akiitumia.