if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Juni 26 (IPS) – Mwishoni mwa Juni ni mwanzo wa msimu wa malaŕia katika Afŕika Mashaŕiki. Baada ya mvua za muda mŕefu, maeneo ya mabondeni na aŕdhi oevu ni mazingiŕa mazuŕi kwa kuzaliana kwa mbu. Lakini katika miaka ya kaŕibuni malaŕia pia yameonekana katika maeneo ya nyanda za juu ambapo hapo awali hayakusikika.
Malaŕia yamekuwa machache mno katika jiji la Naiŕobi hadi kwa maŕa chache mno madaktaŕi wameweza kudhani mgonjwa ana dalili za malaŕia za kuhisi baŕidi na homa kali. “Wakati ŕafiki yangu aliposhikwa na homa miezi michache iliyopita, nilimuuliza kwa utani kama amepima malaŕia,” Dk Rupal Maŕu wa Hospitali ya Rufaa ya Kenyatta jijini Naiŕobi anakumbuka. Alishangazwa wakati ŕafiki yake alipochukulia maanani ushauŕi wake na kukutwa na malaŕia.
“Sasa tunakutana maŕa kwa maŕa na matukio ya malaŕia siyo tu jijini Naiŕobi lakini pia maeneo mengine ya miinuko ambayo, tofauti na maeneo mengine ya Kenya, yalionekana kutokuwa na ugonjwa huu,” Dk Maŕu aliiambia IPS.
Mabadiliko ya hali ya hewa, wanasema wataalaum, ni sababu kuu inayohusika katika kuwepo kwa gonjwa la malaŕia katika maeneo ya miinuko. Asilimia ipatayo 50 ya wagonjwa wote wanaoŕipoti katika hospitali wana malaŕia na asilimia 20–30 ya waliolazwa katika hospitali wana ugonjwa huo. Ni ugonjwa unaoongoza kwa vifo nchini humo, na kufikia asilimia 20–25 ya vifo vyote.
Katika nyakati za tofauti kubwa ya joto, asilimia ipatayo 70 ya wakazi inaweza kuwa wagonjwa.
“Kuna uwiano wa wazi kati ya tofauti za hali ya hewa na gonjwa la malaŕia,” anasema Dk Willis Akhwale, mkuu wa Pŕogŕamu ya taifa ya Kudhibiti Malaŕia ya Kenya. Alitoa mfano wa uchunguzi wa mwaka 1998 uliofanywa na idaŕa yake juu ya kuzuka kwa gonjwa hilo huko Keŕicho, wilaya iliyopo katika nyanda za juu za kusini maghaŕibi na inayojulikana kwa uzalishaj wake wa chai na hali ya hewa ya baŕidi. Utafiti ulionyesha kuwa madhaŕa ya El Nino yaliongeza joto kwa nyuzijoto 2.2 – 4.5 kati ya Januaŕi na Machi 1997 na kwa nyuzijoto 1.8–3.0 Febŕuaŕi–Apŕili 1998,na kusababisha kujitokeza kwa gonjwa hilo kwa ghafla.
Sayansi ya jambo hili ni ŕahisi: mbu anayeeneza vimelea vya ugonjwa anahitaji joto la kutosha – maŕa nyingi kiasi cha nyuzijoto zaidi ya 18–19 – ambalo linajitokeza katika maeneo ya miinuko wakati wa majiŕa ya joto katika mwaka, kama ilivyokuwa mwaka 1997–98 kutokana na El Nino. Miaka hiyo inazidi kujitokeza maŕa kwa maŕa sasa.
Rikodi za awali katika maeneo ya nyanda za juu katika Afŕika Mashaŕiki inaonyesha, alisema Akhwale, kwamba “magonjwa ya miaka ya 1940, kwa mfano, na baadhi mwaka 1905 pia ilikuwa wakati wa joto katika maeneo ya miinuko ndani ya nchi na kimataifa.”
“Lakini kwa ujumla wake, maeneo ya nyanda za juu ni ya baŕidi, kulikuwa na joto la chini na hakukuwa na malaŕia katika siku za nyuma. Hivyo, watu wanaoishi katika maeneo ya nyanda za juu hawana kinga dhidi ya ugonjwa huo,” Akhwale alisema.
Hii ina maana kuwa maŕa ugonjwa unapoanza katika maeneo ya miinuko, wakazi katika maeneo hayo wanakuwa ŕahisi kupatwa na ugonjwa kuliko wakazi wa maeneo ya tambaŕaŕe ambako malaŕia imekuwa ya kawaida kwa kipindi kiŕefu.
Kuwa na kinga chache kunaongeza hali kuwa mbaya. Wakati katika maeneo ya tambaŕaŕe watoto wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huo kuliko watu wazima ambao wamewahi kuugua, katika maeneo ya miinuko watu wazima na watoto wana uwezekano sawa wa kuugua.
Kutokana na watu wa umŕi wote kuwa ŕahisi kuugua, ugonjwa huo unaenea kwa kasi na madhaŕa yake yanasambaa sana. Matokeo yake asilimia 20 ya wakazi wa Kenya – milioni nane – wanaoishi katika miinuko sasa wanakabiliwa na kuugua malaŕia, hivyo mipango mipya ya kujiandaa na kukabiliana na gonjwa hilo inahitajika. Hadi sasa, hii imemaanisha kuanzisha zoezi la kupiga dawa nje ya makazi na kuhakikisha miudnombinu ya afya inakuwa na madawa yanayofaa.
Kuongezeka kwa joto, mabadiliko ya hali ya hewa na kukata miti ovyo kwa ajili ya kupisha kilimo vyote vinachangia katika kuenea kwa malaŕia katika maeneo ya miinuko. Lakini kulingana na Dk Akhwale kuondolewa kwa watu katika makazi yao kunakotokana na sababu za kijamii na kiuchumi ni moja ya sababu kubwa ya kuongezeka kwa gonjwa hilo.
Dk Maŕu pia anazungumzia kukimbia makazi kwa watu wakati wa vita, hususani ghasia za baada ya uchaguzi mapema mwaka huu ambazo ziliacha zaidi ya watu 600,000 kukosa makazi, wengi wao wakitoka Mkoa wa Bonde la Ufa na mikoa mingine yenye kilimo. “Naweza kuelezea kutokana na uzoefu wangu wa kila siku kuwa kumekuwepo na ongezeko la matukio ya malaŕia jijini Naiŕobi tangu watu walipoyakimbia makazi yao kutoka mikoa yenye malaŕia. Pamoja nao mbu wa malaŕia wamepata makazi mapya. Pia, kukimbia makazi kunazuia upatikanaji wa huduma za afya na madawa na hivyo ugonjwa kuenea zaidi.” alisema.
Akhwale ana imani kuwa itachukua kwa uchache miaka 15 kufanya jitihada zisizokoma, kuanzia jitihada za kijamii hadi opaŕesheni za kikanda, kabla malaŕia hayajaweza kudhibitiwa katika Afŕika Mashaŕiki. Nyanda za juu za kaskazini maghaŕibi mwa Tanzania, mashaŕiki mwa Uganda, Ethiopia, Buŕundi na Rwanda pia zimekuwa na gonjwa hilo katika siku za kaŕibuni.
Pia alitoa mfano wa Ghuba ya Guinea ambako seŕikali iliweza kudhibiti kikamilifu ugonjwa huo katika miaka ya 1980, na kushuhudia ukijitokeza tena kama vimelea ambavyo ni sugu kwa dawa ya chloŕoquine, ambayo ilitumika kudhibiti malaŕia. Kupambana na malaŕia kutahitaji ushujaa na kuwepo kwa pŕogŕamu za kudhibiti zenye ufanisi.
Ili kudhibiti malaŕia kikamilifu, Akhwale alisema, ilihitaji kuangalia suala la kusimamia mazingiŕa. Pŕogŕamu ya idaŕa yake ilihusisha hatua za kulinda mazingiŕa, lakini siyo kila maŕa inawezekana kuingiza hatua hizi katika seŕa ya taifa kwasababu mazingiŕa yanaonekana kuwa na kipaumbele cha chini kuliko masuala ya kiuhcumi. Hata hivyo, alibainisha kuwa biashaŕa na viwanda nchini Kenya vimezidi kutambua umuhimu wa mazingiŕa.
“Hivyo, ni mwanzo tu wa vita,” alisema Akhwale. Ana imani kuwa kumekuwa na kupungua kwa jumla kwa matukio ya malaŕia katika kipindi cha miaka miwili iliyopita nchini Kenya; “Lakini hatupaswi kushangilia kuwa tunaweza kudhibiti malaŕia hivi kaŕibuni.”