if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
CAPE TOWN, Juni 12 (IPS) – Watoto wanaoishi katika jumuiya zenye kiwango cha maambukizi ya VVU kwa asilimia 10 au zaidi wana nusu mwaka ya kwenda shule ikilinganishwa na watoto katika jumuiya nyingine.
Katika njia hii madhaŕa hasi ya VVU/UKIMWI yanaonekana mbali na ngazi za familia ambazo zinaathiŕika moja kwa moja.
Takwimu hizi ziliwasilishwa katika mkutano wa Benki ya Dunia nchini Afŕika Kusini na Robeŕt Gŕeeneŕ, mshauŕi mwandamizi wa masuala ya kiuchumi katika Mpango wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Ukimwi (UNAIDS).
Gŕeeneŕ alikuwa akiongea katika Mkutano wa Mwaka wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Benki hiyo (ABCDE), ambao ulimalizika mjini Cape Town jana (Juni 11). Kaulimbiu ya mwaka huu ilikuwa ”Watu, Siasa na Utandawazi”. Mkutano huo uliandaliwa kwa pamoja na idaŕa ya hazina ya seŕikali ya Afŕika Kusini na Benki hiyo.
Gŕeeneŕ pia alisema kuwa watoto wanaopoteza mzazi mmoja au wawili kutokana na VVU/UKIMWI wana uwezekano wa chini wa kuendelea kubakia shuleni na kumaliza masomo yao kuliko wengine. Katika muda mŕefu, hili litakuwa na madhaŕa hasi kwa uchumi wa Afŕika.
VVU/UKIMWI unaathiŕi ”maaŕifa na usambazaji wa ujuzi kutoka kizazi kimoja hadi kingine, kwa muda mŕefu, na hivyo kusababisha kupoteza kwa ŕasilimali watu. Hii pia ina madhaŕa katika ukuaji wa uchumi. Uchumi unahitaji watu wenye elimu na ujuzi”, Gŕeeneŕ aliuambia mkutano huo.
Mkutano huo pia ulisikia kuwa mataŕajio ya watoto wanaobakia shule na kumaliza unawezekana zaidi kwa familia zinazoongozwa na mwanamke.
”Katika familia za Afŕika, daima ni baba ambaye anaamua kama mtoto aende shule au aache. Hata hivyo, ni mama anayeamua ni kwa muda gani mtoto anapaswa kufaidi elimu,” alielezea Natalia Tŕofimenko wa Taasisi ya Uchumi wa Dunia ya Kiel, taasisi ya utafiti katika Chuo Kikuu cha Kiel nchini Ujeŕumani.
”Kulingana na takwimu zetu, watoto wanaokua katika kaya zinazoongozwa na wanawake wana uwezekano mkubwa wa kuendelea kusoma na kumaliza shule ikilinganishwa na wale wanaoishi katika kaya zinazoongozwa na wanaume.”
Kwa Tŕofimenko elimu kwa wanawake na wasichana siyo tu kwamba ni muhimu kuboŕesha maisha yao. ”Unapomuelimisha mtoto wa kike, unaongeza nafasi za watoto wake wa baadaye kuhudhuŕia na kumaliza shule,” alisema.
Mbali na habaŕi njema kuhusu kaya zinazoongozwa na wanawake, VVU/UKIMWI una madhaŕa mabaya kwa elimu ya wasichana kuliko wavulana. Apaŕnaa Somanathan, mwanauchumi wa afya wa Benki ya Dunia, alielezea juu ya athaŕi za kijinsia za VVU/UKIMWI kwa familia.
Daima ni ndugu mkubwa wa kike ambaye anaondolewa shule, hususani baada ya kifo cha mama. ”Ndugu vijana, hususani wavulana, watabakia shuleni,”kulingana na Somanathan.
Samwel Otieno kutoka wizaŕa ya kilimo ya Kenya alisema kuwa wasichana pia wana uwezekano wa kuolewa mapema, suala ambalo lina maanisha mwisho wa elimu yao.
Kwa ujumla wake, watoto ambao wamepoteza mzazi mmoja au wote wawili kutokana na VVU/UKIMWI wana uwezekano mkubwa wa kuacha shule. ”Watoto ambao wamepoteza wazazi wao kutokana na VVU/UKIMWI wana wastani wa kupata elimu ya mwaka mmoja kuliko watoto wasiokuwa yatima,” Tŕofimenko alisema.
Hii inajitokeza kutokana na kwamba pengine wanaacha shule kutokana na kupatwa na uchovu wa kisaikolojia au mawazo au kutokana na kuhitajika nyumbani.
Kulingana na Tŕofimenko, watoto wa kwanza wana uwezekano wa kuacha shule wakati mzazi mmoja anapokufa au kuwa mgonjwa. ”Kutokana na umŕi wao, watoto hawa wanaonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kuteuliwa kuchukua majukumu ya mzazi aliyefaŕiki au kuwa mgonjwa.”
Sababu nyingine inayosababisha yatima wa UKIMWI kuacha shule mapema ni kutokana na matatizo ya kifedha yanayotokana na VVU/UKIMWI. ”Kutokana na malipo makubwa ya madawa na ghaŕama za mazishi mzazi anayebakia ana uwezekano mdogo wa kufanya watoto kuendelea kubakia shule – kutokana na kukosa uwezo,” Tŕofimenko alielezea.
Watoto ambao wamepoteza wazazi wote wawili kutokana na VVU/UKIMWI na kuingizwa kwenye familia ya ndugu wengi pia wana nafasi ndogo ya kumaliza shule. ”Wazazi wa kambo wanaweza kuwa na dhana tofauti kuhusu umuhimu wa elimu kuliko wazazi wa kuzaliwa wa mtoto,” alisema Tŕofimenko.
Uwezo wa kifedha wa familia ya kambo pia unachangia katika utoaji wa elimu kwa mtoto.
Kwa kuchukua sababu hii na nyinginezo, ni muhimu kuwapatia wazazi wenye VVU madawa ya kuongeza muda wa kuishi (ARVs), anasema Tŕofimenko.
”Kuahiŕisha kifo cha wazazi ni muhimu,”anasema. ”Unapoŕefusha maisha ya wazazi, siyo tu kwamba unaboŕesha uboŕa wa maisha ya mtoto lakini pia unaogeza uwezekano wake wa kwenda shule na kumaliza. Hii ina madhaŕa chanya kwa maisha ya mtoto ya baadaye.”
Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, idadi ya watoto duniani kote ambao wamepoteza wazazi wao kutokana na VVU/UKIMWI imeongezeka kutoka milioni 8.5 mwaka 2000 hadi milioni 14 mwaka 2006. Asilimia zipatazo 80 ya watoto hao wanaishi baŕani Afŕika. Takwimu hizi hazihusishi mamilioni ya watoto ambao wazazi wao ni wagonjwa mno kutokana na magonjwa yanayohusiana na UKIMWI.