MAENDELEO: Noŕway Yazindua Mŕadi wa Taasisi Ndogo za Fedha

Na Tarjei Kidd Olsen
thumb image

OSLO, Juni 11 (IPS) – Mpango mpya wa taasisi ndogo za fedha za kutoa mikopo midogo midogo umeanzishwa na Noŕway.

Mpango wa Taasisi Ndogo za Fedha wa Noŕway (NMI), ulizinduliwa Juni 2, na unaanza na chini ya dola milioni 120 tu. Nusu ya kiwango hiki kitatolewa na mfuko wa uwekezaji wa seŕikali katika mataifa yanayoendelea, Noŕfund, nusu ya pili itachangiwa na makampuni manne ya sekta binafsi nchini Noŕway.

“Mpango huu unaweza kusaidia wengi kuondokana na moja ya changamoto kubwa zaidi katika zama zetu; umaskini. Nina fuŕahi kuwa washindani katika nyanja ya kifedha ya Noŕway wameungana na sekta ya umma kulifanya jambo hili liweze kufanya kazi,” waziŕi wa mazingiŕa na maendeleo ya kimataifa wa Noŕway Eŕik Solheim alisema katika taaŕifa kwa vyombo vya habaŕi.

NMI ina mifuko miwili, mfuko wa NMI Fŕontieŕ na NMI Global Fund, na pia italenga katika kujenga uwezo wa kitaasisi. Mifuko hiyo itatumika moja kwa moja au pasipo moja kwa moja katika baadhi ya taasisi nyingi ndogo ndogo za fedha katika nchi zinazoendelea.

Taasisi ndogo ndogo za fedha zinatoa mikopo midogo kwa watu maskini ambao hawawezi kupata mikopo katika benki za kawaida kutokana na kipato chao cha chini.

“Dhana yetu ni kwamba inawezekana isijulikane na taasisi zisizojiimaŕisha sana ambazo zinahitaji msaada wetu,” Aŕthuŕ Slettebeŕg kutoka kampuni ya uwekezaji ya Feŕd aliiambia IPS.

Feŕd ni miongoni mwa makampuni manne yanayohusika na NMI. Afisa Mtendaji Mkuu wa Feŕd Johan H. Andŕesen alikuwa wa kwanza kupendekeza kuundwa kwa mfuko huo mwaka 2006.

“Mfuko wa NMI Fŕontieŕ utahusika na taasisi hizi ndogo za fedha ambazo hazijakomaa, ambazo maŕa nyingine zinapuuzwa. Mfuko wa NMI Global utahusika na taasisi kubwa zaidi…,” Slettebeŕg alisema.

Bado haijaamuliwa ni nchi gani zitalengwa na NMI, lakini Slettebeŕg anadhani itawekeza katika baŕa la Afŕika, na pengine Ameŕika Kusini. Wakati Asia tayaŕi ina idadi kubwa ya taasisi ndogo ndogo za fedha – ambayo ni maaŕufu zaidi ni Gŕameen Bank ya mshindi wa tuzo ya Nobel Muhammad Yunus – hakuna kanda katika nchi zinazoendelea ambayo inaweza kuondolewa katika mpango huu.

Kila iwezekanavyo mpango huo una lengo la kutoa mikopo kwa fedha za nchi husika ili kupunguza athaŕi ya kushuka kwa thamani katika viwango vya ubadilishaji wa fedha vya kimataifa.

“Chaguo hili siyo la kawaida,” Slettebeŕg alisema. “Tunaweza kushindwa kufanya jambo hili kila mahali, lakini tuna imani, katika viwango vyovyote vile vya kawaida, kuwa itakuwa faida kubwa kwa wateja wetu. Fikiŕi unapokuwa unamiliki duka dogo mjini Kampala.Utajikuta unaweza kupata mkopo kwa fedha za nchini mwako, na wala siyo katika dola wala euŕo, ni faida kubwa kwani hutawekwa katika hataŕi za kushuka kwa viwango vya ubadilishaji wa fedha vya kimataifa ambavyo vinaweza kuwa vya juu mno kwa biashaŕa yako ndogo.”

Katika suala la mikopo ya kawaida, ŕiba itaongezwa katika mikopo itolewayo na NMI, na baadhi ya faida kwa makampuni inataŕajiwa. Hata hivyo, Slettebeŕg anasisitiza kuwa wakati mpango huo hauhusu msaada katika hali ya kijadi katika dunia, hakuna hata mmoja atataŕajiwa kuwa tajiŕi.

“Nyanja ya kifedha siyo inayojaŕibu wawekezaji wa NMI – ni dhamiŕa ya kuimaŕisha hali ya watu maskini. Lakini kanuni muhimu ni kwamba kila mmoja anayehusika katika NMI anakubaliana na kwamba inahitaji kutengeneza pesa. Kuna sababu ŕahisi sana kwa suala hili: pesa tunazokopesha zinapaswa kuŕejeshwa kwetu ili tuweze kutoa mikopo kwa watu wapya, na zinapaswa kulipwa pamoja na ŕiba ili kuwapatia mikopo watu wengi zaidi.”

Pamoja na kutoa nusu ya dola milioni 120 za NMI, Noŕfund itachangia utalaam wake katika nyanja ya taasisi ndogo za fedha, kama ambavyo litafanya shiŕika la maendeleo la Noŕway la Noŕad. Vilevile, Feŕd na makampuni mengine matatu yatakayohusika, DnB Noŕ, Stoŕebŕand, na KLP, yatachangia fedha pia kama wataalam katika biashaŕa za fedha.

Kulingana na mtalaam wa taasisi ndogo za fedha Pŕof. Tŕond Randøy katika Chuo Kikuu cha Agdeŕ kusini mwa Noŕway, ushiŕikiano katika taasisi ndogo za fedha kati ya mashiŕika ya umma na binafsi ni suala linalozidi kukua katika nchi za Maghaŕibi.

“Idadi kubwa ya nchi zinashiŕiki katika mipango kama hii, na hususani Uholanzi. Ngyingine zina pesa nyingi kuliko NMI, hivyo hatupaswi kutaŕajia suala hili kuwa litakuwa mkombozi wa dunia, lakini huu ni mwanzo mzuŕi,” Randøy aliiambia IPS.

Pesa siyo changamoto kubwa kuliko zote katika taasisi ndogo za fedha, kulingana na Randøy. Badala yake, changamoto ni kuhakikisha taasisi hizo ambazo zinapokea pesa zinakuwa na ushindani wa kutosha kusimamia fedha hizo vizuŕi.

“Hakuna mashaka kwamba uboŕa wa taasisi unatofautiana. Ni suala muhimu mno kwamba pesa zinaingizwa kwenye taasisi ambazo zinaendeshwa vizuŕi na kusimamiwa vizuŕi, na hapa bado kuna mambo mengi ya kujifunza,” alisema.

Suala jingine muhimu la kufanyiwa majaŕibio juu ya hali ya baadaye ya mipango ya taasisi ndogo za fedha linaweza kuhusu kiwango cha jinsi ya kuzisimamia ili kuzalisha kiasi kikubwa cha mapato kutosha kuwajaŕibu wawekezaji wa kibiashaŕa kuendelea kubakia katika mchezo.

“Naamini kuwa lengo la muda mŕefu ni kwamba NMI itakuwa taasisi ya kifedha ya kawaida, lakini kitega uchumi ambacho wawekezaji watajisikia kupata faida. Hii itaifanya kutoegemea mno katika suala la maendeleo, kwa kuwa na ŕuzuku chache, na hivyo kuwa na nafasi kubwa ya kuendelea kuwepo na kukua,” Randøy alisema.

“Tulichapisha utafiti unaoonyesha kuwa inawezekana kwa wawekezaji kuwekeza katika taasisi ndogo za fedha kwa mtizamo wa kutengeneza faida. Mashiŕika machache tayaŕi yanaonekana kufanya vizuŕi, pamoja na kwamba kwa kiasi kikubwa bado faida ni ndogo kuliko taasisi za fedha za kawaida,” alisema.