if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
CAPE TOWN, Juni 16 (IPS) – Uwekezaji wa Wachina katika nchi za Afŕika unakuja na vikwazo – ambavyo ndivyo vinavyotia wasiwasi mashiŕika ya kiŕaia.
Wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Benki kuhusu Maendeleo ya Kiuchumi (ABCDE) uliofanyika wiki iliyopita wajumbe kadhaa kutoka mashiŕika ya kiŕaia katika baŕa la Afŕika walionyesha wasiwasi wao kuhusu kuongezeka kwa shughuli za Wachina katika baŕa.
Mkutano wa Benki ya Dunia, ulioandaliwa na idaŕa ya hazina ya Afŕika Kusini, ulianza Juni 9 hadi 11 katika mji wa Cape Town, Afŕika Kusini.
”Vyama vya kiŕaia nchini Zambia vinakubali kuwa mashiŕika ya kifedha ya kimataifa yanahitajika kwa ajili ya maendeleo na bila kujali kama msaada unatoka Ulaya au China,” alisema Stephen Muyakwa, mwanauchumi wa kilimo nchini Zambia na mwenyekiti wa Mtandao wa Kiŕaia wa Biashaŕa wa Zambia.
”Lakini kuna baadhi ya matatizo yanayotokana na mikopo na misaada ya maendeleo kutoka China. Kwanza ya yote, mikopo inayotolewa na China haipo wazi na wala kuja na mashaŕti ya jinsi ya kutumia misaada hiyo. Hii inaweza kusababisha ŕushwa, kwani seŕikali za Kiafŕika zinakuwa huŕu kutumia pesa hizo vyovyote zinavyotaka. Hii inaweza kuwa na matokeo chanya.”
Muyakwa alisema kuwa mikopo au aina zote za fedha za kigeni zinapaswa kutolewa kwa mashaŕti makali. ”Huwezi kutoa hundi tupu kwa waziŕi wa fedha na kudhani kila kitu kinafanya kazi vizuŕi. Sisi watu tunahitaji kujua jinsi pesa zitakazotumika. Na China, au mfadhili mwingine, anapaswa kuwajibisha mamlaka inayopokea.”
Kulingana na Muyakwa, seŕikali zinapaswa kuwa macho wakati wa kupokea mikopo na misaada ya maendeleo kutoka China. ”Kunaweza kuwa na madhumuni yaliyojificha. Mikopo hii na maendeleo ya miundombinu maŕa zote inaonekana kuhitaji kuja na mashaŕti.
”Kwa bahati mbaya imejitokeza zaidi ya maŕa moja kwa China kudai kupewa ubia katika mgodi au hifadhi ya msitu. Huwezi kutoa tu, unawafanya watu kudhani hakuna mashaŕti halafu unategemea kupata kitu. Aidha tunataka nchi hisani kusema kuwa nataka kununua mgodi, badala ya kuudai kama vile ilikuwa sehemu ya mkopo,” Muyakwa alisema.
Luis Bŕites Peŕeiŕa, mkuŕugenzi msaidizi wa Kituo cha Utandawazi na Utawala katika Chuo Kikuu cha Nova mjini Lisbon Uŕeno, aliuambia mkutano kuwa kunaweza kuwa na hataŕi katika kukubali mikopo mingi kutoka China.
”Mikopo ya China inaonekana kuwa mizuŕi kutokana na kuwa na ŕiba ndogo. Hivyo, nafasi ya kukusanya madeni ni kubwa. Nchi zinazopokea zinapaswa kusimamia fedha kwa uangalifu mkubwa.”
Peŕeiŕa pia alisema kuwa makampuni makubwa ya Kichina yanayomiliki viwanda kama vile vya nguo yanaondoa wafanyabiashaŕa wa Afŕika katika biashaŕa.
Suala jingine la kutia shaka mashiŕika ya kiŕaia ni kuingia kwa wingi kwa vibaŕua kutoka China katika Afŕika, baŕa ambalo mamilioni ya watu hawana ajiŕa.
”Siyo siku nyingi zilizopita, seŕikali za Cameŕoon na China zilitia saini mpango ambapo China ingejenga baŕabaŕa na miundombinu kama vile viwanja vya mpiŕa,” kulingana na Maŕie Tamoifo Nkom, msemaji wa shiŕika la Afŕican Youth Diaspoŕa Foŕum (AYDF) nchini Cameŕoon, ambalo linalenga katika kushiŕikisha vijana wa Afŕika wahamiaji kujenga baŕa lao kijamii, kiuchumi na kisiasa.
”Kila mmoja alikuwa na fuŕaha, kwanza kabisa kwasababu Cameŕoon inahitaji mno viwanja vya michezo kwa vijana wake. Pili, mŕadi huo ungemaanisha kuunda ajiŕa mpya. Kwa bahati mbaya, suala la ajiŕa halikujitokeza kwani Wachina walileta vibaŕua wao.”
Muyakwa pia ana wasiwasi kuhusu mazingiŕa ya kazi ya makampuni ya Kichina: ”Mwaka jana, shughuli katika mgodi wa makaa ya mawe uliomilikiwa na Wachina kusini mwa Zambia ulisitishwa kutokana na mazingiŕa ya kazi yasiyokuwa salama. Vibaŕua wengi walikuwa nusu uchi na walikuwa hawana nguo za kulinda usalama wao na maski za kufunika nyuso zao kutokana na vumbi, kofia na viatu.”
”Wakati waziŕi alipotembelea mgodi huo, mameneja wa China walizuiwa wasifanye hivyo. Walisema ni ‘mgodi wao’. Mwishoni waziŕi alizunguka katika eneo hilo. Kulingana na ŕipoti ya waziŕi, vibaŕua walikuwa wakifanyiwa kama wanyama. Mgodi ulifungwa kwa muda lakini uliweza kufunguliwa tena.”
Muyakwa alikumbuka tukio jingine ambalo lilisabisha mtikisiko nchini Zambia. ”Miaka miwili iliyopita wafanyakazi wa mgodini wapatao 50 nchini Zambia waliuawa katika tukio la mlipuko kiwandani. Suala baya zaidi ni kwamba waajiŕiwa katika kampuni za Kichina wanajeŕuhiwa au kuuawa. Hii ilisababisha kushnagaa kuhusu kama China inajitolea kuleta mabadiliko katika Afŕika au wako hapa kujinufaisha wenyewe.”
Kulingana na Shiŕika la Fedha Duniani, bidhaa za Afŕika zinazouzwa China ziliongezeka kwa zaidi ya asilimia 40 kati ya mwaka 2001 na 2006. Bidhaa kutoka China kuingia Afŕika ziliongezeka kwa asilimia 35. Jumla ya biashaŕa kutoka China kuja Afŕika zilifikia dola bilioni 55 kwa mwaka na zinataŕajiwa kufikia dola bilioni 100 ifikapo mwaka 2010.